Ewura approves 18 pc power tariff hike from January 1

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Tuesday December 21, 2010 Local News
Ewura approves 18 pc power tariff hike from January 1
12_10_qsnzgr.jpg






By MARIAM SAID, 20th December 2010 @ 05:25, Total Comments: 0, Hits: 304

The Energy and Water Utility Regulatory Authority (EWURA) has slashed the proposal by Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) to hike electricity tariffs from 34.6 per cent to only 18.5 per cent. The new tariff will take effect from January 1, 2011.

Tanesco had requested Ewura to increase the tariff from 34.6 per cent in 2011; 13.8 per cent in 2012 and 13.9 per cent in 2013, which the regulatory has refused.

“After a meeting with the Tanesco board of directors, it was decided that a wide electricity tariff adjustment system, to cover three years from January 1, 2011 to December 31, 2013, should be deferred until when a credible cost of service study is carried out by an independent expert to be engaged by us,’’ EWURA Director General Haruna Masebu told a news conference in Dar es Salaam on Monday.

He also cited several conditions for the approved tariffs, including one ordering TANESCO to submit to Ewura a detailed report of technical and non-technical loses within one year.

Furthermore, Ewura has abolished a special rate for the utility company’s staff, whereby they will now be subjected to tariffs as other general use customers.

According to TANESCO, the requested tariffs will enable to demonstrate its bankability to donors, increase capacity needed to meet system peak demand and to adequately fund repair and maintenance programme to ensure a stable supply of electricity.
 
Tanesco had requested Ewura to increase the tariff from 34.6 per cent in 2011; 13.8 per cent in 2012 and 13.9 per cent in 2013, which the regulatory has refused.

"After a meeting with the Tanesco board of directors, it was decided that a wide electricity tariff adjustment system, to cover three years from January 1, 2011 to December 31, 2013, should be deferred until when a credible cost of service study is carried out by an independent expert to be engaged by us,'' EWURA Director General Haruna Masebu told a news conference in Dar es Salaam on Monday.

Maisha bora kwa kila Mtanzania sasa ni ndoto ya alinacha.....................................
 
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

And yet hakuna hata Mtanzania mmoja atakayepinga hili ongezeko!
 
12_10_gc9qva.jpg


Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, Haruna Masebu,(kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya kuongezeka kwa gharama za umeme Januari mosi mwakani. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Umeme, Anastas Mbawala. (Picha na Yusuf Badi)
 


Mgawo waanza tena, bei ya umeme juu


Imeandikwa na Lucy Lyatuu na Maulid Ahmed, Kilwa; Tarehe: 20th December 2010 @ 23:59

WAKATI Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ikiamuru wafanyakazi takribani 5,000 wa Tanesco kulipa viwango sawa vya bei za umeme kama ilivyo kwa wananchi wengine, na ikiridhia kupandisha bei ya umeme kuanzia Januari mosi, mgawo wa umeme unaanza tena leo.

Mgawo wa umeme uliositishwa wiki moja iliyopita, umetangazwa jana mjini Kilwa mkoani Lindi ikiwa ni kutokana na Kampuni ya Pan African Energy inayozalisha gesi asili katika kisiwa cha Songosongo kupunguza uzalishaji kwa ajili ya kufanyia matengenezo kisima kimoja kati ya vitano ilivyonavyo.

Mahitaji ya matengenezo ya kisima hicho yaligundulika Septemba mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema Tanesco imelazimika kuanza tena mgawo tena kutokana na upungufu wa megawati 40, akisema "tunalazimika kupunguza uzalishaji katika mtambo wa Ubungo ambapo baada ya kuzalisha umeme wa megawati mia moja, sasa tutalazimika kuzalisha megawati 60, na ratiba tutartoa baada ya kuipanga."

Mramba alitangaza mgawo huo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja wakati alipotembea Kilwa Kisiwani kunakozalishwa gesi asilia kwa ajili ya kuiuzia Tanesco na Kampuni ya Songas.

Akitoa taarifa kuhusu kukifanyia matengenezo kisima hicho, Naibu Meneja Mkuu wa Pan African Energy, William Chiume alisema kutokana na matengenezo hayo, watapunguza uzalishaji kwa asilimia 16 kutoka futi za ujazo milioni 86 hadi 76, ambazo ni sawa na megawati 40.

Alisema matengenezo hayo yatachukua kati ya wiki nne na tano kuanzia sasa. Hata hivyo, alisema waathirika wakubwa ni Tanesco, kwani Songas wataendelea kupata gesi kutokana na mkataba walionao. Songas pia wanaiuzia umeme Tanesco.

Songas inaiuzia Tanesco megawati 182 za umeme kwa siku na wakati mitambo ya Tegeta inazalisha megawati 45, Ubungo megawati 100, yote ya gesi asili wakati mahitaji ni megawati 833 kwa siku.

Wakati mgawo huo ukitangazwa Kilwa, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Ewura, Haruna Masebu alitoa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura wa maombi ya Tanesco ya kubadilishiwa bei za umeme, na kueleza kuwa Bodi imekubali ombi hilo na imepandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari mosi.

Masebu alisema wafanyakazi hao wamekuwa wakilipia viwango maalumu, hivyo Bodi imeamuru walipe kama ambavyo wananchi wengine wanalipia na endapo hawatotekeleza itaonekana wakati wa ukaguzi.

Akifafanua zaidi, Mkurugenzi wa Umeme wa Ewura, Anastas Mbawala alisema wafanyakazi wa Tanesco wanakadiriwa kufikia 5,000 na wamekuwa wakilipa Sh nne kwa kila uniti ya umeme, ingawaje kwa wale ambao ni mke na mume, alikuwa anapewa mmojawapo na sio wote.

Kuhusu bei ya umeme, Masebu alisema maombi ya Tanesco yalitolewa Mei 28, mwaka huu na mchakato ulianza mara moja wa kukutana na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili kwa kina suala hilo ili kila mmoja aridhike na hatua zitakazofuatia.

Masebu alisema mikutano ilifanyika Agosti katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Tabora na Dar es Salaam, na kwamba "baada ya kukutana na wadau mbalimbali na kujadili kwa kina suala la kubadilishiwa bei hizo, Ewura iliona kuna hoja ila hawawezi kukubali maombi hayo kama yalivyoletwa na Tanesco."

Alisema Tanesco waliomba kuwe na mpangilio wa kubadilisha bei ya umeme kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2011 kwa asilimia 34.6, asilimia 13.8 na asilimia 13.9 ili waboreshe huduma zao na kuwa endelevu wakati wote.

Kadhalika alisema Tanesco waliomba pia mabadiliko hayo yaende pamoja na kuwa na uwezo wa kurekebisha viwango vya umeme wakati wowote, kuruhusiwa kubadilisha bei ya umeme katikati ya kipindi hicho kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta na kubadilika kwa viwango vya umeme kadri ya matumizi.

Alisema ni kweli Tanesco wanahitaji zaidi ya Sh bilioni 691 ili itoe huduma endelevu, hivyo Ewura imekubali ombi lao kwa asilimia 18.5 ikiwa ni pungufu ya asilimia 16.1 huku gharama nyingine kutokubaliwa hadi hapo watakapopata mtaalamu mshauri atakayefanyia kazi suala hilo na kuona kama viwango hivyo vinafaa.

Alisema kwa marekebisho hayo, bei ya umeme kwa watumiaji wadogo wanaotumia umeme usiozidi kilowati 50 watalipia Sh 60 kwa kila uniti kutoka Sh 49 za awali huku watumiaji wa kawaida watalipia Sh 157 kutoka Sh 129.

Kuhusu kufungua akaunti maalumu, alisema baada ya kukusanya fedha hizo za viwango vipya, Tanesco wanatakiwa kufungua akaunti ya fedha hizo na kuagiza kuwa zielekezwe katika kazi husika ambapo Ewura watakuwa wakikagua kila baada ya miezi mitatu.

Masebu alisema kutokuwakubalia Tanesco kupandisha umeme wasingekuwa na uwezo wa kujiendeleza na vilevile hatua hiyo inatoa nafasi kwa wawekezaji wengine kujiingiza katika sekta hiyo.
 
Back
Top Bottom