Ewe mwanaume wa kibongo kwa trend hii ya dada zenu... Sijui!

mikila miwili

JF-Expert Member
Dec 14, 2021
563
555
Leo hii nani asiyejua kuwa wanapenda tamthilia mno hawa dada zenu wa kibongo? Wanajua majina yote ya wasanii wa kikorea, kifilipino na hata wa kizungu.

Hali hii wanaihamishia mpaka kwenye maisha halisi, wanataka wanaume wa hivyo. Nenda kwa Mwamposa na mitume wengine hapa mjini uone walivyojazana kutafuta waume wa kuwaoa huko.

Wengine mpaka wanalala kwenye mahema, tena ni wadada wazuri hatari mpaka unajiuliza iweje akose wa kumuoa? Kwamba hatongozwi au?

Kumbe jipu linaanzia kwa hawa akina dada wenyewe, wanachagua mno hawa dada zenu, wanachagua to the excess, wanaringa mno, dharau, viburi n.k, yaani unaweza kuwa na hela ila akakujibu anavyotaka na pesa zako.

Hawa ndio aina ya wanaume wanaowataka sasa, wewe mwenzangu mwenye pua fupi nene kama inang'aa kama kisosi hawakutaki, wewe mwenzangu mfupi mwenye kichwa kifupi, kikubwa kinene kama Gentamycine huna chako.

Hali ni mbaya, warembo wengi mno zaidi ya 500 wanakwenda kwa manabii kutafuta wanaume wa kuwaoa, Mwamposa, Mwingira, Mwakasaks n.k, mna kazi sana!!! Ningekuwa mimi ningekuwa nawatimua, sababu nimeshaieleza hapo awali.

Jamani wenye sura zenu pasono hamna chenu, wataishia kuwadanga tu kweli gaps hazitokwisha duh. Na huu ndio mfano wa wanaume wadada wengi wanapenda wawaoe!

Nawasilisha,
FB_IMG_16437261967886687.jpg
 
Time factor mkuu. Ukijua wanawake wanakimbizana na mda wala huwezi jisumbua. Mwanaume anaanza kuishi maisha akiwa na 35 yrs old. Wanawake anakuwa "product of value" akiwa na miaka 20-28 na ndo umri wengi uolewa na kuzaaa. Sasa hao wanaozinguka kwa Mwamposa hawajajua kitu ya Mda.

Mwanaume tulia ishi anza kuwaza oa ukiwa na miaka 30+ hutakuja kusumbuka. Hawa wanawake wanaochagua waache wachague ndo umri wao. Ila siku wakishtuka mda umewatupa usishangae mtu wa kawaida anaoa uyo anayempend mkorea
 
Back
Top Bottom