Ukitaka kuwatawala masikini, wafarakanishe

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
671
Ameandika ndugu Christopher

Ukitaka kuwatawala masikini, unawagawa tu. Unahakikisha wale masikini wajingawajinga unawapa mamlaka ya kipolisi, unawapa bunduki, au upendeleo kidogo tu, halafu unawaambia hawa wenzenu (masikini wenye akili akili) ni wachochezi hawaitakii mema nchi yetu. Halafu unawaacha wapambane wenyewe kwa wenyewe.

Historia ya ubaguzi wa rangi kule Marekani ya kusini ilianza hivyo; watu weupe waliambiwa wao ni bora kuliko weusi, sheria zikawekwa kupiga marufuku watu weupe na weusi kupata huduma sawa mahali popote. Masikini weupe, hata wenye utapiamlo wakajiona bora kuliko watu weusi. Lakini lengo la watawala lilikuwa kudhibiti vuguvugu la kundi la watu walioitwa 'Populist' ambao walikuwa weusi kwa weupe, wakidai nyongeza za mishahara kwenye mashamba ya mabepari.

Afrika kusini nako ilikuwa hivyo; sheria ziliwekwa kwa ajili ya kumdunisha mtu mweusi na kumpendelea mtu mweupe. Hata hivyo, hao weupe sio kwamba walipendwa sana, la! walipunjwa pia. Lakini hawakudai chochote kwakuwa waliambiwa wao ni bora kuliko weusi. Hilo liliwaondolea kabisa fikra za kupambana na mabepari kwa kuwaona ni 'wazungu wenzao'.

Wakati wa uvamizi wa wakoloni wa kijerumani kwenye ardhi iliyokuja kuitwa Tanganyika, Wajerumani waliunda jeshi la watu weusi walioitwa Askaris. Hao ndo walitumika kupambana na Mkwawa, Isike nk. Watu wengi wanadhani Wajerumani walikuja na jeshi lao kutoka Ulaya, hapana. Jeshi la Mjerumani liliundwa na makamanda wachache wa kizungu lakini asilimia 99 walikuwa watu weusi wa Afrika waliopewa pesa (mercenaries) kupambana na waafrika wenzao. Ni dhana ileile ya kuwagawa na kuwatawala.

Wakati wa utawala wa mkoloni Muingereza, mishahara ya wafanyakazi ilitolewa kwa kuzingatia rangi hata kama wafanyakazi walikuwa na elimu na nafasi sawa ofisini. Walimu wazungu walipewa mshahara mkubwa, walimu wahindi wakapewa mshahara wa kati, na walimu waafrika (akina Cecil Matola walioanzisha chama cha AA) walipewa mshahara wa chini hata kama walikuwa na elimu sawa na wenzao. Wahindi na Waafrika walikuwa wenyeji zaidi ya Waingereza, lakini walilazimishwa kujiona wanyonge, lakini wahindi wakapewa upendeleo kidogo ili kuwagawanya. Hata makazi yao yaligawanywa; wahindi wakaambiwa nyie kwa sababu mnafanana kidogo na sisi mtaishi Upanga, halafu hawa nyani wataishi Kariakoo (makazi mapya ya waswahili) na Ilala. Posta na Oysterbay yakawa makazi ya Wazungu. (Masaki yote ni eneo la Oysterbay, jina la masaki lilikuja baadae).

Pamoja na ubaguzi huo waliofanyiwa wafanyakazi weusi, bado walijiona bora kuliko waafrika wengine. Walikuwa wajivuni, wenye dharau na kujifanya wamestaarabika. Mathalani, kaka yake Mwl. Cecil Matola, aliyeitwa Samwili Chipombe, Padre wa kianglikana aliyefukuzwa huko Zanzibar na baadae kuwa Mwalimu katika shule ya serikali ya Dar es salaam (leo DIT), alinukuliwa akisema; "Ni ukweli kwamba mwafrika akiishi maisha ya kimagharibi ndio anaonekana amestaarabika)". Hao ni waafrika waliodharauliwa na wazungu lkn kwa sababu ya kuwa waajiriwa wa serikali ya kikoloni wakajiona bora kuliko wengine waliokuwa wakipigwa, kuwekewa sheria za kibaguzi na kunyimwa fursa za kujiendeleza ndani ya nchi yao. Hata chama cha AA, kwa wasiojua kilikuwa chama cha kuratibu shughuli za starehe za waafrika wenye kipato (ingawa katiba yao ilisema ni chama cha waafrika wote). Ni zao la dhana ileile ya kugawanywa na kutawaliwa

Hata wakati wa harakati za kutafuta uhuru wapo baadhi ya waafrika, hasa waajiriwa wa serikali ya kikoloni waliwaona akina Nyerere kama wasumbufu. Wengine walimdharau Bibi Titi Mohammed kwa sababu ya uanamke wake, wakamuona kama binti aliyekosa adabu kwa kuzurura hovyo huku na kule eti anatafuta uhuru. Wengine walimuita malaya.

Na leo wapo. Wapo watu wanaamini kupambania demokrasia ni usumbufu na uchochezi kwa sababu wameajiriwa mahali wanapata kamshahara mwisho wa mwezi. Hawajui faida kubwa ya demokrasia inayotafutwa kwa ajili ya taifa kuliko hivyo vimishahara vyao. Wapo watanzania, kwa sababu ni wanaCCM tu, wanaamini wao ni bora kuliko wanaChadema kwasababu ukiwa CCM haubugudhiwi na polisi, hausumbuliwi na mamlaka, haubambikiwi kesi. Hata kama mtu huyo huyo ana watoto wenye utapiamlo, hatajali kusinyaa kwa matumbo ya watoto wake, anajali kuwa bora kuliko mwanaChadema.

Mfano mzuri wa watu hawa ni Polisi. Mengi yamesemwa kuhusu maisha magumu ya Polisi. Lakn kwa sababu wamepewa marungu na bunduki, wanasahau shida zao. Wakirudi vibandani mwao, wakikutana na sura za kimasikini za wake zao na watoto wao, wanajiuliza kwa muda tu, halafu punde wanakumbuka kumbe wao ni askari ambao 'wakitumwa kuua mtu wanatumia risasi moja tu'. Wakitumwa kumkamata Mbowe hawashindwi, wakitumwa kuwadhibiti wasumbufu wa Chadema hawashindwi... wao ni watabe kwelikweli. Basi wakikumbuka hayo wanasahau kabisa umasikini wao na familia zao.

Lakini magumu ya maisha yetu hayafichiki. Tazama huyu, yupo bize kukamata 'wasumbufu wa Chadema', na serikali anayoitetea imemsahau - hata kusitiri matako yake hawezi masikini ya Mungu. Lakini anajiona bora kwa sababu tu ya rungu aliloshika. Ajabu na kweli.
 
Serikali ya ccm inachoweza kwa ufanisi na bidii zaidi ni kumkamata Mbowe na sio kupambana na shida za watz.
 
Hawa wananua ndege zinaenda kupark watoto masikini kama hawa hawaoni future yao hali wazazi wao wanalipa kodi

IMG_20210722_170209.jpg


IMG_20210805_224932.jpg
 
Uko sahihi, hiyo ndiyo mbinu inayotumika duniani kote
 
Back
Top Bottom