iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Nadhani suala hili ni kipimo cha akili kwa watanzania.
Ili kujikimu,kila mtu anafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kujiingizia kipato.
Wapo mama lishe,mafundi ujenzi,wakandarasi,machinga,wamiliki wa baa,grosari,duka,genge, shule,stationery,mabasi,bodaboda,mgahawa,hoteli,mafundi seremala na kila aina ya shughuli za kiuchumi.
Siku hizi kuna kauli maarufu "fedha zitakauka mfukoni" na kuna kundi la watu wakisikia kauli hii,hushangilia mpaka wanapatwa kiu ya maji.
Hivi tunaelewa maana ya kauli hii?
Wewe mama lishe unayeshangilia pesa kukauka mfukoni,hao Wateja wako watanunua chakula chako kwa kutumia nini? Wasiponunua hata kwa wiki moja,je hutafunga biashara?
Wewe bodaboda unayeahangilia na kumshangilia anayesema anakausha pesa mfukoni,mwisho wa wiki utampelekea hesabu gani bosi wako? Na kama ukishindwa kumpelekea hesabu si utanyanganywa hiyo bodaboda?
Ewe mkulima unayeshangilia na kumshangilia mkausha fedha mfukoni,hayo mazao yako nani atayanunua?
Ewe mmiliki wa baa na grocery unayemshamgilia mkausha fedha,hizo bia utamuuzia nani na hao wahudumu utawalipaje,pamoja na kodi ya pango,umeme na maji.
Ewe mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi unayeshangilia mkausha fedha,hayo mabati na simenti utamuuzia nani?
Ewe fundi ujenzi unayeshangilia mkausha fedha,utapata wapi kazi ya kujenga kama watu hawana
Ewe mmiliki wa duka la nguo unayeshangilia mkausha fedha,nani atanunua nguo zako kama kakaushwa mfukoni
Ewe mmiliki wa hotel I unayemshangikia mkausha fedha,utapata wapi Wateja wa vyumba na chakula hotelini kwako.
Ewe TRA utapata wapi mapato kama watu hawafanyi transaction baada ya kukaushwa mfukoni.
Ewe mfanyakazi unayesubiri mshahara upande,upandishwe daraja kazini,utapandaje mshahara kama serikali haina mapato ya kodi ya kutosha kutokana na wafanyabiashara kukaushwa fedha mfukoni hivyo kushindwa kuendesha biashara zao na wengine kuzifunga na hivyo TRA kukosa mapato?
Ewe serikali ya masikini na wanyonge,je umasikini na unyonge utaondoka kwa kukausha fedha mfukoni ?
Ewe mmiliki wa shule (sio st mary international)unayemshamgilia mkausha fedha,hao wanafunzi wa kujilipia ada za mamilioni utazipata wapi?
Ewe mzazi unayemshamgilia mkausha fedha,huyo mwanao utamlipiaje chuo kikuu wakati sasa mikopo imesitishwa na wewe mfukoni umekaushwa.
Ewe mkulima,utanunuaje mbegu na pembejeo za kilimo wakati umekaushwa mfukoni,mvua hakuna lakini bado unamshangilia mkausha fedha.
Ewe muuza chipsi unayeshangilia Wateja wako kukaushiwa fedha,hizo chips utamuuzia nani?
Ewe bongo muvi unayemshangilia mkausha fedha hizo muvi utamuuzia nani eti?
Ewe bongo fleva unayemshangilia mkausha fedha,hizo show zenu nani ataingia?
Ewe,mwandishi, mtangazaji wa radio na TV unayetangaza kwa mbwembwe matamko ya kukausha fedha,unajua mshahara wako unategemea bosi wako kuwa na fedha mfukoni
Kutangaza unakausha fedha mfukoni ni sawa na kutangaza nia ya kuongeza idadi ya watu masikini nchini,kadri unavyokausha,ndivyo masikini wanavyojaa kila kona ya nchi.
Tunaamini kazi ya serikali sio kuongeza idadi ya masikini,bali kuongeza idadi ya matajiri na tabaka la kati
TAFAKARI,