Ewe msichana, utaolewa na nani kati ya hawa?

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,488
3,263
Ifuatayo ni hadithi ya mapenzi, ikimhusisha msichana Mwasiti na watu wanne wa taaluma tofauti; mwimbaji, mvuvi, mganga na mwindaji. Waliishi kijijini kando ya mto.

Mwasiti kijijini alipendwa kwa tabia yake nzuri. Siku moja akiwa anafua aliteleza na kutumbukia mtoni, kukamatwa na mamba na kuzamishwa majini. Mwimbaji aliekuja kuteka maji aliimba wimbo nzuri ukamwibua mamba kusikiliza. Mwindaji aliekuwa jirani katika harakati zake akamlenga mamba kwa gobole lake na kumuua.

Mvuvi aliekuwa mtoni akivua aliogelea na kumfikia Mwasiti aliekuwa anatapatapa baada ya kutoka kinywani mwa mamba na kumvusha hadi nchi kavu. Mwasiti alikuwa na majeraha yakivuja damu nyingi. Mganga akifika eneo la tukio na kumtibu na baada ya wiki moja alikuwa mzima wa afya.

Ilikuja bainika kumbe kwa nyakati tofauti watu wote hawa wanne waliwahi kumchumbia Mwasiti, lakini alikuwa hajatoa jibu. Tathimini ya Mwasiti anawapenda wote, anawiwa na deni la kuokoa maisha yake. Akubali kuolewa na nani?
 
Umenisahau mimi dereva wa bajaji niliyemwahisha hospitali mana tungemchelewesha robo saa tu angeenda zake nami istoshe alishakubali vokol zangu hyo siku alifata maji ya kuoga tukutane gest nitesti kama yaliyomo yamo.

Achana na mabwabwa hayo madomo zege,mpaka waoe
 
Back
Top Bottom