Ewe mfanyakazi, jitahidi kuwatembelea wenzako ujifunze maendeleo wanayofanya

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,645
35,979
Mnapokuwa kazini hasa kada au ofisi moja sometimes mnajisahau na kujiona kama ni kitu kimoja kwa 100%.

Unapomtembelea mwenzako unaweza kuamkwa na akili utakapoona ana nyumba nzuri zaidi, ana projects ambazo hata kibarua kikiisha au akiamua kuacha kazi hawezi kuyumba.

Pia, ukimkuta amelala unaweza kumwamsha kwa kumpa ushauri chanya. Na ikiwezekana mwalike kwako ajifunze kwa macho yake.

Jambo hili la kutembeleana lisifanyike kwa unafiki na umbea. Mwingine akija kwako akiona mjumba anapeleka umbea kazini. Be careful.
 
Mnapokuwa kazini hasa kada au ofisi moja sometimes mnajisahau na kujiona kama ni kitu kimoja kwa 100%.

Unapomtembelea mwenzako unaweza kuamkwa na akili utakapoona ana nyumba nzuri zaidi,
Hapa ndipo umaskini wa watanzania wengi ulipo.Wahindi hawana nyumba wanapanga nyumba za msajili wa majumba na ni matajiri hatari watoto wanasoma kanada nk

Waswahili tunapenda sana kulalia pesa!!! Kazi ya hiyo nyumba nzuri ni nini zaidi ya kulala na kuamka? Hakuna cha kujifunza hapo ujinga mtupu

WAkenya ukimtembelea mgumu sana kukupeleka nyumbani atakuambia twende kwenye biashara yangu na ukifika sio ushangae shangae lazima ununue kitu siuo akupe offer!!! Pale sio sehemu ya utalii !!

Mswahili ukibishana naye kidogo utasikia mimi nina kwangu wewe una nini? Na ukisalimiana naye atakwambia karibu kwangu kumbe lengo lake akuonyeshere hizo pesa alizolaza kwenye matofali badala ya kuwekeza.Anakuonyesha jinsi anavyolalia pesa na kuamka.Jumba hilo mamilioni ya pesa la kulala na kuamka .IDLE CAPITAL invested in beds and siitting rooms!!!

Mleta mada shtuka nyumba nzuri kwa ulimwengui wa sasa sio kitu cha kumbabaishia mtu watu wameshahama huko wamebaki washamba wachache kama wewe
 
Hapa ndipo umaskini wa watanzania wengi ulipo.Wahindi hawana nyumba wanapanga nyumba za msajili wa majumba na ni matajiri hatari watoto wanasoma kanada nk...
Dada mada yako ya kutaka watu wasijenge wawe Kama wahindi umeikomalia kweli, unashindwa kujua wahindi wanaogopa kujenga tangu enzi za nyerere, ila wanajenga kwao na kwa baadhi ya nchi za afrika.

Kwa maisha ya kawaida nyumba ndio kila kitu, familia inakuwa na amani ikiwa kwao, halafu maisha yenyewe mafupi sikuizi, unaweza ukawa na hela ukaacha kujenga,mwishoe ukafa gafla mke na watoto wataanza kuangaika nyumba za kupanga.
 
Wazo ni jema ila wahusika sasa ndio ngoma nzito , mtu unamkaribisha vizuri kwako alafu kesho anaanza kukupakazia kwa boss ilitu mambo yako yasiende
 
Back
Top Bottom