Ewe Jasusi uliyenikataza nisimtwange ngumi Paulo Makonda mbona humlindi tena?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,014
8,368
Ndugu zangu hakuna kitu Cha kuheshimu kama Muda na technolojia ndugu zangu.

Zaidi ya hapo, Sina mengi zaidi ya kukutaka wewe msomaji wa Uzi huu kuwa heshima dhidi ya watu wanao kuzunguka na hata wasio kuzunguka lazima nikusihi juu ya Ili.

Niliwahi andika Uzi mmoja kupitia jukwaa hili nikilaumu jinsi nilivyomshuudia Paulo Makonda akimtandika NGUMI Waziri Mkuu na mwanasheria Mkuu wa serikali Mzee wetu Warioba .

Nikiri nilikuwa sehemu ya mkutano huo, kimsingi haukuwa mkutano, lilikuwa ni jukwaa la kujadili ile iliyokuwa inaitwa rasmu ya Warioba, enzi hizo tulikuwa tumeitwa wanafunzi wa vyuo vikuu twende nasi tukatoe maoni yetu na hasa tuchangie Ile rasmu Mzee walioba hakupenda kitendo kilichofanywa na umoja wa vijana ccm waliojazwa wanafunzi wa shule ya msingi Osterbay na shule ya msingi Mbuyuni kitendo kile kilimkera sana Mzee Warioba na alichukia kweli kweli.

Nikiri katika ukumbi ule kulikuwa na Kambi mbili toufauti kwa maana umoja wa wanafunzi ambao ni wanachama wa chadema na ccm kwa mantiki hiyo vijana wa chadema waliweza kujenga hoja nzito nzito, ila wa ccm kama tunavyo waona leo hii ugonjwa wa fikra zao haujaanza leo.

Ilikuaje Makonda akampiga Mzee Warioba?

Mzee walioba alikerwa na wanafunzi wa shule ya msingi walio jazwa ukumbini na Makonda, Sabaya na yule bwana Sasa hivi na mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Happy, hawa vijana walikuwa vijana wa ovyo tangu zamani.

Wale wanafunzi wa shule ya msingi, wakiongozwa na Makonda walipoona vijana wa upinzani wamepewa MiC kuchangia walikuwa wakipiga kelele mithili ya vichaa kwa namna ya kuzomea.

Warioba baada ya kuona Hali ile Kuna kauli aliyoitoa na kuwachafua vijana wa ccm ndipo Makonda alipomfata Mzee na kumpiga Kofi zito huku nyuma yake akiwa na ulinzi wa kijana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Jasusi na alikuwa pale kumlinda Makonda asiguswe na mtu.

Je Mimi nilijuaje?

Niliumizwa na kitendo kile cha Makonda kumpiga Mzee kibao nikishuka kutoka jukwaani na kwenda kumvaa Makonda nilivyonyanyua mkono nikitaka kumtwanga ngumi mkono wangu ulizuiwa na huyo bwana aliyejitambulisha yakuwa ni usalama wa taifa na alikuwa akimlinda Makonda Sasa nisidiriki kumgusa

Nikiri yakuwa niliogopa na sikuendelea na Nia Ile nilitoka nje na kukimbia nisiko kujua.

Miaka nane baada ya hapo Makonda anakuwa mkuu wa wilaya niyokuwa naishi, kisha mkoa niliosomea na kukulia niliamua kuamishia shughuli zangu mikoa mingine sikutamani hata mara moja kukutana na Huyu kiumbe.

Ndani ya miaka kumi nilienda ofisini kwake na alinikumbuka vyema na alinizuia nisifanye kilichokuwa kimenipeleka ofisini kwake, maana nilienda kujitambulisha na kumjulisha yakuwa Kuna kazi natakiwa kufanya mkoani kwake, alinizuia NAMI nilinyanyuka na kuondoka na kutoa RIPOTI yakuwa nimezuiwa nae, kilichojili akiangaika kunitafuta yeye baada ya kutekenywa kidogo.

Nyie mwajua Alikuwa yupo juu ya Kila mtu ila Kuna Wana walikuwa wanamkalisha na anakaaa

Kumbukizi hii nakusihii wewe Jasusi uliyenitisha Sasa nenda kamlinde ukiweza mweke uvunguni.

Mwanaume wa Dar unaogopa Mende? yaan unaogopa machoko bob!
 
Unasema kweli!??
emoji32.png
emoji32.png
 
Chai tu.....

Waziri mkuu mstaafu na makamu wa rais Warioba huwa anatembea na walinzi ...yaani walinzi wake waruhusu ndugu Makonda amshambulie?!!!!

Uongo mtupu huu....

Hata Kama mtu mnamchukia ila si kwa CHUMVI HIZI......

#Siempre JMT🙏
 
Askofu Mwingira aliwahi kunena kuwa Ikulu aliishi shetani. Ni sahihi kabisa kwa 100%.

Fikiria Rais ayateua majitu ya hovyo kabisa Makonda, Sabaya na Happy kuwa viongozi. Huyo anayewateua watu wa hovyo namna hii, alikuwa anataka kupata nini kutoka kwa hawa baradhuli?

Shetani alikuwa yupo safarini kusimika utawala wake dhulumati, lakini Mungu aliwaonea huruma Watanzania.
 
Askofu Mwingira aliwahi kunena kuwa Ikulu aliishi shetani. Ni sahihi kabisa kwa 100%.

Fikiria Rais ayateua majitu ya hovyo kabisa Makonda, Sabaya na Happy kuwa viongozi. Huyo anayewateua watu wa hovyo namna hii, alikuwa anataka kupata nini kutoka kwa hawa baradhuli?

Shetani alikuwa yupo safarini kusimika utawala wake dhulumati, lakini Mungu aliwaonea huruma Watanzania.
Kwa hiyo hapo mlipo mko vizuri sana baada ya mungu wenu kuwaonea huruma?
 
Inaonekana kipindi hicho cha kikweta ulikuwa kijijini ndani kabisa huko nakapanya

Sawa....

Nilikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu nami nilihudhuria mkutano huo pale ubungo plaza kama kijana wa UVCCM kupitia kundi la vyuo vya Dar es salaam nikiwa mwenyekiti wa tawi la CCM chuoni kwangu .........

Mh.Ally Salum Hapi ananijua vyema kwani niligombea naye uongozi wa juu uchaguzi wa makamu mwenyekiti shirikisho la vyuo vikuu vya jijini.....

Ok

#Siempre JMT🙏
 
Back
Top Bottom