Uchaguzi 2020 Ewe Jaji Mkuu wa Mahakama na Enyi TAKUKURU

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,668
2,000
Nikiwa Kama Mtanzania, naomba kutoa ombi na ushauri wangu kwako Jaji Mkuu wa Tanzania. Mahakama Ni Taasisi takatifu mahali popote Duniani. Kuna habari zinaandikwa humu mitandaoni kuwa Kuna njama kutoka watu wa CCM kumhujumu Lissu akiwa mahakamani ili asifaulu kuendelea na harakati zake za kugombea Urais. Ombi langu kwako Jaji Mkuu naomba usafishe tuhuma hizo, iepushe Mahakama na mambo machafu na ya haramu Kama kweli yapo.

Kwako Mkuu wa TAKUKURU, nikiwa kama Mtanzania ili kuleta imani kwa wananchi naomba uwachunguze Shibuda na Lipumba Kuna manenomaneno yanapita huku mitandaoni kuwa wamepewa rushwa na watu wasiojulikana ili wamwekee pingamizi mgombea wa CHADEMA.

Maana yake,
Wao hawana shida na mgombea huyo ila kwa kuwa wameshawishiwa kwa kupewa rushwa hili ni kosa la jinai. Kutoa rushwa kwa sababu yeyote ile Ni kosa. Naomba muwachunguze ili kuleta imani na amani.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,850
2,000
Takukuru Leo wameniacha hoi sana. Eti mgombea wa Chadema katoa rushwa apitishwe na msimamiz wa uchaguzi wa CCM. Yani kuna watu wanaandika script ila Takukuru script zao hadi Bongo Movie wamewashinda
 

nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,932
2,000
Huyo jaji boya hawezi fanya kitu.Ni hasara kubwa nchi kuwa na mtu wa aina yake kwenye nafasi nyeti kama hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom