Every woman's dream or is it?

Jamaa katoka kazini, bado ana tai, halafu ndo kuosha vyombo. Safi sana. Husbands, love your wives, ..... as yourself.

UKIMALIZA, KASONGE UGALI.
 
Huo ni mvao sahihi kabisa mkuu! Jamaa yupo kazini na kazi yake ni babysitter!! Na anatakiwa kuwa smart na kufanya house chores zote, kifupi analisha familia yake kwa kazi hiyo usikute!! Akifika home kwake hagusi hivyo vitu hata kwa mangumi!!




Haaaaaa......! Mambo ya ulaya hayo, babysitter. Jamani acheni mmmh.........................
 
Mimi ni kati ya wanawake ambao hawadream hayo. Mwanaume ndani ya nyumba inabidi awe mwanaume sio housegirl au baby siter. mwanaume anatakiwa kucheza na mtoto, sio kubeba mtoto huku anaosha vyombo kama yupo kwenye adhabu.
kama kuna mwanamke anayedream hayo basi sijui anataka nini, au ameshamchoka huyo mume; maana huwezi ukawa na mume unayemfanya hivyo halafu ukawa unampenda.

Sawa, ila vipi kama wewe unaenda kazini na yeye anakaa nyumbani, labda ndio anatafuta kazi so muda mwingi yuko nyumbani?
 
Bw. AB,

Tatizo la hii 'model' ni kwamba huku kwetu uswazi nyumba za kupanga, vyombo vyaoshewa nje upenuni watu wote na wapita njia wakuona, maana hamna haya mambo ya ndani kwa ndani.

Hivo mwanamume unapoamua kufanza kama haya inabidi uwe na moyo wa chuma kwelikweli, maana kila mtu mtaani atajua.

Halafu watasema LIMBWATA hilo, na siyo mapenzi.
 
Kwangu mimi I would say no, its not my dream afikie level hii jamani. Hizo ni kazi mbili kwa mpigo, they can be shared between the two. Ila kama wadau walivyochangia, huyo baba haonyeshi furaha, something must be very wrong!
Kuli, usimtukane huyo baba kwa ubebaji wake wa mtoto, hiyo ndiyo shughuli inayotukuta pale mtoto anapolia, hataki kuwekwa chini na kazi nyingine lazima zifanyike!

Ila sijui hao watumiaji wa hizo sahani zote wote wako wapi!
 
Mtoto nabeba, kuosha vyombo sioshi
kupika ntapika - ninachoweza na kupenda best - kuchoma nyama, michemsho ya kufa mtu, misupu supu, mitambi kwa maini! sio maugali na mawali ya nazi! na mamichuzi, hapo siwezi.
 
hata kama hana kazi, nasisitiza kuwa hizo sio kazi za Mume

Hapana haiwezekani FP. Kwa hiyo utaenda kazini na mtoto na ukirudi nyumbani jioni uanze kazi za nyumbani maana mchana mzima mume wako alikuwa anasoma magazeti na kuangalia TV? Ina maana yeye mume haruhusiwi kukusaidia kazi za ndani japo kidogo? Kazi za wanaume ni zipi kwani? Hebu nifafanulie
 
Jamaa katoka kazini, bado ana tai, halafu ndo kuosha vyombo. Safi sana. Husbands, love your wives, ..... as yourself.

UKIMALIZA, KASONGE UGALI.

Bwana Harusi wetu mtarajiwa... Geoff

Tafadhali fuata nyayo!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom