Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,772
- 30,046
EVERTON VS SAIGON 1967
Rafiki yangu Mohamed Abdulrahman kutoka Ujerumani leo asubuhi kaniandikia kitu kilichonirudisha nyuma sana udogoni.
Soma stori:
"Baada ya kuundwa Saigon Everton ilibaki na tulicheza mechi mbili.
Ya kwanza nilicheza inside right pembeni yangu alikuwa Mkwanda Ingemar Johansson.
Kitu cha ajabu kilitokea.
Mwanzo wa game tu tunaanza nimepokea pasi nikamgongea Mkwanda na yeye akapiga shuti golini kutoka centre na akafunga goli.
Mnazi Mmoja hapo mbele ya Kibarua Bar.
Mechi hii nilikatika jino la chini mbele.
Alama ninayo hadi leo.
Lile goli liliwakasirisha sana Saigon.
Jumanne Masimenti ambae alikuwa akicheza Centre Half Saigon akawa ana overlap kuja mbele kusaidia mashambulizi.
Na hii ilikuwa style ya Everton tulipokuwa hatujagawanyika na lazima goli litapatikana.
Sisi kumuona Jumanne anakuja mbele ikabidi tujazane nyuma kulinda goli.
Hapo ndipo nilipovunjika jino.
Masimenti "Guu la Ngamia," marehemu Harudiki Kabunju akipenda kumwita hivyo, akakutana na loose ball ndani ya box akapiga shuti kali golini.
Nikaweka kichwa nimesimama katikati ya "goal line."
Taya ya juu na ya chini zikaumana jino likakatika.
Jumanne alikuwa na tambo kapanda juu vizuri sana kamchukua baba yake.
Lakini juu ya mwili huu Jumanne alikuwa mpole sana na wababe wakimuogopa hawathubutu kumchokoza.
Ukigongana na Jumanne hewani wewe utaanguka chini yeye atatua na miguu yake miwili kisha akupe lile kono lake kubwa kukunyanyua.
Jumanne alikuwa na mdogo wake Twaha mguu wake wa kushoto mfupi kidogo hivyo akichechemea lakini alikuwa left winger hatari kwa mashuti na mbio.
Akicheza Young Kenya club kali katika club za mitaani.
Wenzake katika timu hii walikuwa Kirk Douglas (Kitwana Douglas), Kesi Kibuda, King Kodo, Denis Law (Jamil Hizam) kwa kuwataja wachache.
Hupita Mnazi Mmoja na wanangu nikawaambia udogoni tumecheza sana mpira kwenye viwanja hivi.
Jumanne alipokwenda Cosmopolitan Coach Mansur Magram ndiyo akambadilisha position na kumchezesha Centre Forward.
Mechi ya pili sikucheza.
Nimerudi shule St. Joseph's Convent School haraka nikafika nyumbani kubadili nguo nawahi kutazama mechi hapo Mnazi Mmoja.
Tukiishi Libya Street jumba la Posta karibu na Mnazi Mmoja.
Nimekuta vurugu kumetokea ugomvi Mkwanda kampiga kichwa Mrisho Wanted kampasua.
Mrisho kuniona mimi naingia kanifata damu zinamvuja usoni.
Mimi maisha yangu yote sikuwa mtu wa ubabe na hata hao wababe wakimuogopa Mrisho sembuse mie kitoto kidogo.
Basi akafika hadi mbele yangu nami "I cooly held my ground."
Nadhani kwa ile heshima niliyokuwanayo na kule kutulia kwangu nikimwangalia aliona aibu hakunigusa.
Wanted siku ile alikuwa ameadhirika kupigwa na Mkwanda mtoto mdogo juu ya ubabe wake wote.
Akamfuata Mkwanda nyumbani kwao.
Mkwanda akatoka ndani kwao kumkabili barabarani.
Mrisho akampiga Mkwanda ngumi ya tumbo.
Mkwanda hakumrudishia alirudi nyuma kashika tumbo lake.
Ugomvi ukaisha Mrisho akaondoka.
Mrisho akajakuwa mtu aliyekuwa na mapenzi makubwa sana na mimi kila akiniona atanipigia kelele, "Eusobio njoo nipe hela niingie kwa Gersan."
Pale Mchikichi na Sikukuu Amani Gersan alifungua mgahawa wake akiuza pilau mchana.
Gersan mwenyewe mbabe unaogopa hata kumwambia kachumbari haikukolea ndimu.
Hii ilikuwa hoteli ya wababe.
Mandava ndiyo wanakutana hapo mchana kula.
Mimi nikiingizwa hapo na Ali Ugaga (Uri Gagarin) mbabe mwenzao tukitokea bandarini.
Siku nyingine tunakwenda kula kwa Matataiwa kisha tukahamia Msimbazi na Kiungani kwa Amiri Ali Mchawi.
Hoteli zote hizi walikuwa na wapishi hodari sana.
Matataiwa akipika hadi mseto na papa.
Allah awarehemu ndugu zetu wote waliotangulia mbele ya haki.
Utoto una raha zake."
PICHA: Kulia ni Mwandishi na Victor John.