beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Burundi imemuapisha rais mpya wa taifa hilo , Evariste Ndayishimiye, katika hafla iliofanyika mbele ya raia wa taifa hilo na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti.
Katika kiapo chake rais huyo ameapa kulinda katiba ya Burundi, kuheshimu umoja wa raia wa taifa hilo, kutoa haki kwa wote mbali na kutetea mipaka ya taifa hilo.
Kiapo hicho kinatokana na kifungu cha 107 cha katiba ya nchi hiyo
Sherehe hiyo iliofanyika katika uwanja wa kandanda wa Ingoma katika mkoa wa Gitega imefanyika wakati ambapo taifa hilo limeathirika na mlipuko wa vurusi vya corona.
Rais Evariste baada ya kumaliza kula kiapo alkagua gwaride la kijeshi na baadaye kutoa hotuba.
Muda mchache kabla ya kula kiapo rais Evariste aliombewa na baadhi ya maaskofu ambao walimtaka kufungua milango ya uhusiano mwema na mataifa mengine.
Mbali na kwamba baadhi ya wageni hawakuvalia barakoa, raia wengi waliohudhuria hafla hiyo hawakuvaa kifaa hicho cha kuwalinda dhidi ya corona.
Hatahivyo shirika la msalaba mwekundu liliandaa maji na sabuni kwa raia wote waliokuwa wakiingia katika uwanja huo kuosha mikono yao.
Maelfu ya raia wa Burundi wamefurika katika uwanja huo wakisubiri kuapishwa kwa rais huyo kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza.
Makamu wa rais wa Tanzania bi Samia Suluhu na aliyekuwa rais wa taifa hilo jakaya Mrisho Kikwete wamewasili nchi humo.
BBC Swahili