Evarist Chahali: Urafiki wetu na RWANDA ni wa mashaka

na Evarist Chahali

Niwe mkweli, sina imani katika "urafiki wetu mpya" kati yetu (au tuseme JPM) na Rwanda (tuseme Paul Kagame). Sababu kubwa ya mie kukosa imani (yes I know haijalishi nikiwa na imani au la) ni mbili.

Kwanza, kiintelijensia, kila nchi - hususan nchi jirani - ni adui. Tishio kubwa la usalama kwa nchi nyingi duniani ni nchi jirani. Kwahiyo tishio kubwa la usalama wetu kimataifa ni Rwanda, Burundi, DRC, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Nchi zote hizo zina majasusi nchini mwetu.

Hiyo haimaanishi tuwe maadui, bali tuwe na "urafiki wa macho wazi" kama ule wa paka na panya. Kimsingi, kitu kinachoitwa "diplomasia" au "uhusiano wa kimataifa" is all about "kutambua na kuzingatia kanuni za urafiki wa mashaka" na kujitahidi "to make most out of it." Players muhimu katika maeneo haya wanapaswa kuwa mashushushu wazoefu au wabobezi kwenye siasa "za maslahi yangu kwanza" za kimataifa. Kwa bahati mbaya, akina sie, kigezo cha uanadiplomasia ni "adhabu" (bwana mkubwa anakuweka "kifungoni" nje ya nchi) au ukada/kujuana/maslahi binafsi na vitu kama hivyo.

Lakini, pili, ninakosa imani kuhusu Rwanda na Kagame kwa sababu nchi hiyo ni "dola ya kiintelijensia." Kwa jinsi Kagame "alivyotengeneza maadui wengi" nchi hiyo inalazimika kuwa kama Israel (na ni maswahiba wakubwa hawa) ambayo inafahamu fika kuwa kuiona kesho kunategemea uhodari wa taasisi za kiintelijensia kuhakikisha usalama wa taifa hilo, adui nambari moja wa mataifa ya Kiarabu. Dola za kiintelijensia zina rafiki mmoja tu wa dhati: zenyewe tu. Na kila kitu katika mahusiano ya kimataifa ni kwa maslahi ya zenyewe.

Na kwa wasiofahamu, Kagame ni shushushu mzoefu, japo sehemu kubwa ya elimu yake ya ushushushu aliipata Tanzania. Shirika la Ushushushu la Rwanda (NISS) ni moja ya mashirika hodari kabisa ya ushushushu barani Afrika. Na mafanikio makubwa ya shirika hilo ni katika kupenyeza majasusi. Inaaminika kuwa majasusi wa nchi hiyo wana ufanisi mkubwa katika "kuwawinda na kuwaangamiza maadui wa taifa" kama Putin anavyofanya kwa wapinzani wake.

Nimeandika haya baada ya kusoma taarifa ya "uhuni" wa Marekani kwa Japan. Kwa muda mrefu, Marekani imekuwa ikiitumia Japan kupata taarifa kuhusu China na Russia. Hata hivyo, wakati Japan ikitoa msaada mkubwa wa kiintelijensia kwa Marekani kufanya ushushushu dhidi ya China na Russia, kumbe Marekani nayo inafanya ushushushu dhidi ya Japan kupitia Shirika lake la ushushushu linalohusika na kunasa mawasiliano, yaani NSA. Stori kamili ipo hapa Japan Made Secret Deals With the NSA That Expanded Global Surveillance

Stori hiyo imenifanya nitafakari tena kuhusu urafiki wetu na Rwanda, ambao pia unahusisha baadhi ya maeneo ambayo hakuna chombo cha habari "chenye jeuri" ya kuripoti. Sina hakika kama JPM anashaurika lakini uswahiba wake na Kagame utatugharimu.Naandika hili kama kumbukumbu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Kuna msemo mmoja upo hivi "nikishamfanya adui yangu kuwa rafiki namteketeza."

Hapa chini ni waraka wa Christopher Mtikila kuhusu Kagame alioutoa wakati wa uhai wake.
Ndugu huwezi kuwatenganisha.
 
Lakini mbona tumeshaanza kuiga mabovu yao?
Leo nko hpa ubungo naelekea mwenge kwenye mataa kuna askari zaidi ya 20 na mabunduki barabara zote zimefungwa mkuu anapita,yani kama unapendwa na wananchi wko hakuna haja ya ulinzi mzito kiasi hichi
 
Hatuna urafiki na yeyote. Sisi tunaangalia maslahi yetu Mkuu. Mazuri ya Rwanda tuyaaige. Mabovu na ujanja wao tuwaachie. Especially umafia wa Kagame kuua wapinzani wake wasiokubaliana na mtizamo wake.
unazungumza haya kwa mamlaka gani mkuu?
 
Wanajeshi wa Rwanda na Tanzania kusaidiana ktk ulinzi huko mipakani kagera.
Chanzo: Radio one Habari SAA mbili usiku 30.10.2018
 
Jana niliangalia video clip ikimuonesha raia mmoja dereva wa magari makubwa ya mizigo aliyewagimea askari wa Tanzania kushuka ili kukaguliwa na kwa kelechi zaidi alikuwa akiwatishia panga........daah...
 
Sordid tale. Lakini I'm sure Magufuli aliyamaliza matatizo yote haya alipokuwa Rais,yàani,uonevu kwa Wasukuma.
Navyofahamu Mimi Ni kwa Kikwete aliwafukuza Wanyarwanda kule, Kagame alikasirika,akasema anataka kumpiga ngumu Kikwete usoni...the rest is history.
Lakini hizi ni confusion tu za wafugaji wanatafuta malisho kwa ng'ombe zao.
Halafu kumbuka hao Wahaya na Waganda wanaelewana lugha. Yaani makabila yao wanaweza kuongea bila mkalimani. Kwa hiyo inawezekana kutokea slight problems with loyalties.
 
na Evarist Chahali

Niwe mkweli, sina imani katika "urafiki wetu mpya" kati yetu (au tuseme JPM) na Rwanda (tuseme Paul Kagame). Sababu kubwa ya mie kukosa imani (yes I know haijalishi nikiwa na imani au la) ni mbili.

Kwanza, kiintelijensia, kila nchi - hususan nchi jirani - ni adui. Tishio kubwa la usalama kwa nchi nyingi duniani ni nchi jirani. Kwahiyo tishio kubwa la usalama wetu kimataifa ni Rwanda, Burundi, DRC, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Nchi zote hizo zina majasusi nchini mwetu.

Hiyo haimaanishi tuwe maadui, bali tuwe na "urafiki wa macho wazi" kama ule wa paka na panya. Kimsingi, kitu kinachoitwa "diplomasia" au "uhusiano wa kimataifa" is all about "kutambua na kuzingatia kanuni za urafiki wa mashaka" na kujitahidi "to make most out of it." Players muhimu katika maeneo haya wanapaswa kuwa mashushushu wazoefu au wabobezi kwenye siasa "za maslahi yangu kwanza" za kimataifa. Kwa bahati mbaya, akina sie, kigezo cha uanadiplomasia ni "adhabu" (bwana mkubwa anakuweka "kifungoni" nje ya nchi) au ukada/kujuana/maslahi binafsi na vitu kama hivyo.

Lakini, pili, ninakosa imani kuhusu Rwanda na Kagame kwa sababu nchi hiyo ni "dola ya kiintelijensia." Kwa jinsi Kagame "alivyotengeneza maadui wengi" nchi hiyo inalazimika kuwa kama Israel (na ni maswahiba wakubwa hawa) ambayo inafahamu fika kuwa kuiona kesho kunategemea uhodari wa taasisi za kiintelijensia kuhakikisha usalama wa taifa hilo, adui nambari moja wa mataifa ya Kiarabu. Dola za kiintelijensia zina rafiki mmoja tu wa dhati: zenyewe tu. Na kila kitu katika mahusiano ya kimataifa ni kwa maslahi ya zenyewe.

Na kwa wasiofahamu, Kagame ni shushushu mzoefu, japo sehemu kubwa ya elimu yake ya ushushushu aliipata Tanzania. Shirika la Ushushushu la Rwanda (NISS) ni moja ya mashirika hodari kabisa ya ushushushu barani Afrika. Na mafanikio makubwa ya shirika hilo ni katika kupenyeza majasusi. Inaaminika kuwa majasusi wa nchi hiyo wana ufanisi mkubwa katika "kuwawinda na kuwaangamiza maadui wa taifa" kama Putin anavyofanya kwa wapinzani wake.

Nimeandika haya baada ya kusoma taarifa ya "uhuni" wa Marekani kwa Japan. Kwa muda mrefu, Marekani imekuwa ikiitumia Japan kupata taarifa kuhusu China na Russia. Hata hivyo, wakati Japan ikitoa msaada mkubwa wa kiintelijensia kwa Marekani kufanya ushushushu dhidi ya China na Russia, kumbe Marekani nayo inafanya ushushushu dhidi ya Japan kupitia Shirika lake la ushushushu linalohusika na kunasa mawasiliano, yaani NSA. Stori kamili ipo hapa Japan Made Secret Deals With the NSA That Expanded Global Surveillance

Stori hiyo imenifanya nitafakari tena kuhusu urafiki wetu na Rwanda, ambao pia unahusisha baadhi ya maeneo ambayo hakuna chombo cha habari "chenye jeuri" ya kuripoti. Sina hakika kama JPM anashaurika lakini uswahiba wake na Kagame utatugharimu.Naandika hili kama kumbukumbu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Kuna msemo mmoja upo hivi "nikishamfanya adui yangu kuwa rafiki namteketeza."

Hapa chini ni waraka wa Christopher Mtikila kuhusu Kagame alioutoa wakati wa uhai wake.
Where is the Ex-spy @Evarist Chahali nowadays who had sought refugee in the UK to escape the whipping rod of the replica bulldozer? He reclaimed his reputation through his edition on 'Usalama wa Taifa ni mtu wa aina gani' and ' 'Shushushu'. What is his views related to DP World saga?
 
Back
Top Bottom