Evarist Chahali: Mbona shoga aliteuliwa kuwa kiongozi wa umma Tanzania?

Mkuu hizi habari za kuulizwa swali mnajibu na swali kwanza tuziache. Nyie nijibuni kwanza mnataka sisi tuweke sheria ya kuwatambua watu wanaofanya zinaa kwa sababu tu wapo?..

Yes, tumestand kwa Uingereza kwa sababu wao wanataka kutulazimisha tutambua ushoga kama vile wakitulazimisha kutambua zinaa tunaweza wajibu hatuwezi kutambua Zinaa ingawa zipo na zinafanyika. Wao ndio wanafiki kwa sababu Cameron akionekana na shoga kesho hana kazi, sisi haya ni maswala ya chumbani serikali haiwezi kuyaingilia unless kuna mmoja aliyedhulumiwa haki yake. Ukim rape shoga utafikishwa mahakamani na sheria inamlinda shoga kama binadamu wengine...

uutambua ushoga wakati shoga haruhusiwi anabaguliwa sehemu za kazi, anabaguliwa jeshini, anabaguliwa kwa kila nafasi ya kujihusisha na jamii ni kutunga sheria za kinafiki na ndicho wanachokifanya nchi za magharibi. Tena nimesema wazi majuzi tu nimeona site ya UK mwnamke akifunga ndoa na mbwa sasa twende huko kwa sababu Waingereza wanasema! Au wanataka tuhalalishe kwa sababu Ghaddaff alishindiliwa jiti na tuone sawa tu!

Binafsi naamini huwezi kutungia sheria za kiutawala kila kitu cha matamanio ya watu, wakati wananchi wako wana imani zao za dini, mila na desturi zao lazima kuziheshimu zile zenye kujenga jamii (diversity) na sii matendo ya kila mmoja wao.. Na huwezi kulazimisha vitu ambavyo havihusiani na Ubaguzi na kuvifanya sheria kwa sababu tu unapenda vitu hivyo. Wewe kama unakula nguruwe kula mimi sili lakini huwezi kunambia tuweke sheria ya kuhalalisha nguruwe ili iwe nini?

Tuna matatizo makubwa na muhimu ya kiuchumi kupambana na Ufisadi sio swala la matamanio ya mtu ambaye hadhulu mtu mwingine isipokuwa starehe yake.
 
Samahini mkuu wangu sikuwepo ubaoni kwa muda naona maswali yamekuwa mengi ila nitajaribu kukujibu yale muhimu zaidi ktk kueleza maana ya swala hili..

Mkuu wangu, Dar mimi sii mgeni na nimeishi sehemu ambazo mashoga ni sehemu ya jumuiya toka kina Ally London, Ibrahim, Kitwana na wengine wengi tu ambao tulikuwa tukiruka nao majoka Africana, Mbowe na wote hawa walikuwa wakifanya kazi maofisini tena nazungumzia wakati wa Nyerere.

Umeyachukua maneno ya Membe kuelezea sheria lakini umeruka haki ya kwanza ya kutambua Ushoga. Bado unaendeleza tatizo lile lile la kutambua kitendo na sii WATU. Haki za binadamu kwa mashoga ni pale wanapotengwa sawa na ubaguzi wa rangi, kabila, dini ndivyo tunavyolitazama swala la Ushoga kama binadamu na sii yale wanayoyafanya tofauti na binadamu wengine kuwa sheria.

Tulicholazimishwa na Uingereza ni kutambua haki za mashoga ambazo tunawapa lakini kwa mtazamo wa vitendo vyao yaani ndoa za jinsi moja kitu ambacho hata Marekani wenyewe hawazitambui kitaifa isipokuwa kwa baadhi ya states. Hii haiwafanyi kwamba hawatoi haki za Mashoga isipokuwa hawatambui vitendo vyao ambavyo ni kinyume cha tafsiri ya ndoa kulingana na tamaduni zetu.

Labda msome vizuri Membe kazungumzia NDOA za jinsia moja na adhabu yake sasa kama wewe unaijua harusi yoyote ilofungwa baina ya mashoga na ikapata sheria tuonyeshe hiyo ndoa. Balozi aliyekuja ni shoga vile vile mbona yeye aliruhusiwa isipokuwa mshirika wake ndiye hakutambuliwa kutokana na sisi kutotambua ndoa za mashoga. Hivyo Balozi kama shoga aliruhusiwa kuingia na angeifanya kazi yake bila taabu tatizo ni sisi kuitambua ndoa yao, tunalazimishwa kuitambua. Sisi tuna sheria zetu, tunatambua ndoa ni baina ya mwanamme na mwanamke sawa na wao hawawezi kutambua ndoa ya Mkandara nikienda UK na wake zangu 10, sheria yao haitambui ndoa hizi japokuwa wananchi wake wanafanya zinaa..Je, niseme UK wanafiki kwa sababu Waingereza wenyewe wanafanya zinaa mbona hawalaani zinaa isipokuwa wanalaani Polygamy!..

Mkuu kuna mambo madogo ambayo hayahitaji sheria, sheria siku zote ipo kulinda mambo makubwa yanayoweza kuisambaratisha jamii na sii kutazama mabo madogo ya chumbani mwa watu. Hiyo utakuja sema serikali inaingilia privacy ya watu kwa sababu haya mambo madogo sii ya kiutawala.

Kwa mfano serikali inaweka sheria ya ndoa na kuzitambua zile zilizofungwa kwa kufuata taratibu hizo lakini haina sheria kuhusiana na relationship za wananchi wake. Unachojaribu wewe kusema ni kwamba serikali ianatakiwa kufuatilia hata relationship ikiwa inataka kutoa haki ya wanandoa..hapana mkuu wangu hatutambui ndoa za jinsia moja na hatuna sheria ya kufuatilia kutambua ama kukataa relationaship za watu kisheria.

Nitarudia tena kusema sheria ya umoja wa kimataifa ni kutambua HAKI za Mashoga kama binadamu wengine na wasibaguliwe kwa sababu tu ni mashoga. Lakini unapokwenda kutambua ndoa na vitendo vyao hilo ni hatua nyingine kabisa ambayo inaingilia tamaduni za wahusika. Kiutamaduni hatuupendi Ushoga ingawa upo na hatuwezi kutambua ndoa zao kisheria.
Saluteeeeeeeeeeh
 
Duuuuh uzi wa kitambo, mweeeeeeh Dunia ina makubwa khaaaaah. JF idumu milele.
 
Comment ilifutwa bahati nzuri waliiquote.

JF nzito sanaaaa

Kuna wawili hapo nimesikia mara nyingi mno
Screenshot_20201223-123733.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20201223-123733.jpg
    Screenshot_20201223-123733.jpg
    51.4 KB · Views: 2
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom