Evarist Chahali: Mbona shoga aliteuliwa kuwa kiongozi wa umma Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Evarist Chahali: Mbona shoga aliteuliwa kuwa kiongozi wa umma Tanzania?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kipanga mlakuku, Nov 11, 2011.

 1. k

  kipanga mlakuku Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]


  Mwandishi mkongwe, mwanamapinduzi na mwanaharakati Mtanzania anayeishi nchini Uskochi ameibuka na madai mazito dhidi ya jamii ya kitanzania kwa kile anachodai ni kuendekeza unafiki kwenye sakata la ushoga. Mwandishi huyo ambaye pia ni mmiliki wa Blog maarufu ya siasa inayokwenda kwa jina la KULIKONI UGHAIBUNI ameenda mbali zaidi kwa kuweka wazi kuwa mbona "shoga fulani" aliteuliwa na serikali kuwa kiongozi wa shirika la umma mpaka akalifilisi na ingawaje watu wanajua lakini walikaa kimya?

  SOMA MAKALA KAMILI HAPA..................................

  Tatizo ni unafiki wetu, si ushoga

  Evarist Chahali
  Uskochi  MOJA ya mambo yaliyonishitua sana nilipofika hapa Uingereza kwa mara ya kwanza ni jinsi Ukristo ulivyopoteza nguvu yake (hususan mahudhurio kanisani na watu wanaofuata Ukristo). Kilichonishitua ni ukweli kwamba Ukristo uliletwa huko nyumbani na "wazungu" hawa na nilitarajia wangekuwa wacha Mungu wakubwa.

  Dalili za Ukristo kupoteza nguvu yake zinaonekana katika namna makanisa yanavyoishia kugeuzwa kumbi za starehe baada ya kukosa waumini. Kadhalika, asilimia kubwa ya waumini makanisani ni wageni kutoka nje ya nchi hii. Na japo Malkia wa Uingereza ni Mkuu wa Kanisa la Anglikana na Askofu Mkuu wa Canterbury ni mithili ya Baba Mtakatifu (Papa) kwa Kanisa hilo, idadi kubwa ya Waingereza inajitambulisha kama watu wasiofuata dini. Na kuna kundi kubwa tu la wanaojitambulisha kama Wakristo lakini wasiotia mguu kanisani.

  Hakuna jibu jepesi kuhusu kwa nini Ukristo unazidi kupoteza nguvu nchini hapa lakini baadhi ya watu niliowahoji wanadai huenda maendeleo katika nyanja mbalimbali ni chanzo kwa baadhi ya watu "kupuuza" umuhimu wa imani katika maisha ya mwanadamu.

  Lakini pamoja na Ukristo kupoteza nguvu yake miongoni mwa Waingereza, kwa kiasi kikubwa uadilifu katika nyanja mbalimbali za maisha umeendelea kuwa wa kiwango cha juu. Na hapa ndipo unaweza kubaini tofauti kubwa kati ya Waingereza "wanaopuuza dini" na akina sie huko nyumbani ambao dini inaonekana kuwa sehemu muhimu kwa maisha yetu.

  Neno mwafaka linaloweza kuelezea tofauti hiyo ni UNAFIKI. Ni hivi, ni bora kuwa na watu wasio na dini au wasioabudu uwepo wa Mungu lakini wakaishi na kutenda mambo kiadilifu kuliko kuwa na ‘washika' dini wasiokosekana makanisani au misikitini lakini uadilifu wao ni haba kama sio sifuri kabisa.

  Na suala la unafiki linaweza kuchukua nafasi muhimu katika mjadala mkali uliosababishwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza kuwa nchi yake itasitisha misaada kwa nchi zinazokiuka haki za mashoga. Tayari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ameweka bayana msimamo wa Serikali kwamba Tanzania ipo tayari kukosa misaada ya Uingereza kuliko kubadilisha sheria za nchi zinazopiga marufuku ushoga.

  Kuonyesha kuwa tamko la Membe halikuwa la kukurupuka tu, Rais Jakaya Kikwete
  alinukuu kauli hiyo ya Waziri wake na kuirusha hewani (Retweeted) kwenye ukurasa wake (Kikwete) kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

  Lakini kabla sijaingia kwa undani katika kujadili suala hili ni vema nikaweka wazi msimamo wangu. Imani yangu kama Mkristo wa madhehebu ya Katoliki (ambaye almanusura ningekuwa padre iwapo nisingeghairi kujiunga na seminari mwaka 1986) sio tu inapinga ushoga bali pia inauona kama dhambi. Kwa hiyo, naomba ifahamike kuwa lengo la makala hii si kuunga mkono ushoga.


  Kwa upande mmoja, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alikuwa na haki ya kuweka masharti katika misaada wanayotoa. Ifahamike kuwa misaada hiyo inatokana na fedha za walipa kodi wa Uingereza na inatarajiwa ielekezwe kwa nchi zinazoonekana machoni mwa Waingereza kama zinazoendana na maadili yao. Na moja ya masuala yanayopewa kipaumbele na nchi hii ni haki za binadamu (ikiwa ni pamoja na haki za mashoga).

  Kwa hiyo basi si kwamba Cameron alikurupuka tu na tamko hilo ambalo baadhi ya wenzetu wamelitafsiri kama ajenda ya kueneza ushoga, bali anawakilisha hisia za wananchi wake ambao kimsingi ndio chanzo za fedha tunazopatiwa kama misaada.

  Ni wazi kuwa kiongozi yeyote yule anayejua anachofanya atahakikisha anasimama upande wa wananchi wake. Kwa mantiki hiyo wananchi wake wanapotaka fedha yao wanayotupatia kama msaada ielekezwe tu kwa nchi zinazojali haki za binadamu (ikiwa ni pamoja na haki za mashoga) tu basi hana budi kufanya hivyo.

  Japo siungi mkono ushoga lakini ninaelewa mantiki ya Cameron kutoa tamko hilo linaloakisi matakwa ya wananchi wake. Lakini kwa vile matakwa ya Waingereza kuhusu haki za binadamu hayaishii kwa mashoga pekee, ingeleta maana zaidi iwapo tishio la kukata misaada lingeelekezwa pia kwenye tatizo sugu la rushwa (na ufisadi kwa ujumla) ambalo si tu linakwaza haki za binadamu za masikini (ambao ni wengi kuliko mashoga) bali pia linaweza kusababisha wanyonge kupoteza maisha (kwa mfano rushwa inayowezesha vyombo vya usafiri vyenye hitilafu kuendelea na kazi na hatimaye kusababisha ajali).

  Sasa nigeukie unafiki unaoandamana na jinsi tamko la Cameron lilivyopokelewa. Haihitaji utafiti wa kina kubaini kwamba si tu Tanzania (na nchi nyingine zinazolengwa na tishio hilo la kukatiwa misaada) ina mashoga lakini pia ushoga unazidi kuongezeka. Hivi nani anayesoma magazeti ya burudani au blogu hajamwona shoga mmoja aliyejipachika jina Seduction ambaye ni kama yupo kwenye kila shughuli za mabinti maarufu jijini Dar?

  Nilipokuwa huko nyumbani mwaka 2005 na niliporejea tena mwaka 2008 nilishuhudia idadi kubwa tu ya mashoga katika maeneo mbalimbali ya burudani jijini Dar es Salaam. Na uchunguzi usio rasmi ulionesha kuwapo kwa mashoga kwenye kitchen parties ni kama suala la kawaida tu. Nilibaini kwamba kumbi za muziki wa mwambao zilikuwa ni chaguo kubwa la mashoga.

  Lakini jambo moja la wazi ni kwamba hakukuwa na upinzani, chuki au hasira dhidi ya mashoga hao. Na sijawahi kusikia kuna shoga amekamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani na hatimaye kufungwa kwa "kosa" la kuwa shoga. Na ukidhani hilo la kutokamatwa kwa mashoga ni la kushangaza sana, basi kubwa zaidi ni uteuzi wa kigogo mmoja (mstaafu sasa) wa shirika la umma ambaye kila aliyemjua alikuwa anafahamu tabia yake ya ushoga (kwa maana ya tendo la ndoa na watu wa jinsia yake).

  Nina hakika aliyemteua alikuwa anafahamu hilo lakini haikuzuia kigogo huyo kupewa nafasi ya kufisadi shirika hilo hadi alipoondoka huku akijimwagia sifa za vichekesho.

  Tuache unafiki, hivi maadili tunayodai ni haya ya wengi wa vigogo wetu kutumainia waganga wa kienyeji katika kila wanalofanya? Maadili haya ya "wachunga kondoo wa Bwana" kuishi maisha ya kifahari kama matajiri wakubwa ilihali waumini wao hohehahe wakihimizwa kuongeza kiwango cha sadaka? Au maadili haya ya Wakristo na Waislamu wasiokosekana kwenye nyumba za ibada lakini ndio wahusika wakuu wa ufisadi? Au haya ya ushirikina kuwa muhimu kuliko kumtumainia Mungu?

  Au maadili tunayodai kuwa nayo ni haya ya majambazi wanaotupora utajiri wetu kisha kuibukia makanisani au misikitini na kutoa sadaka au zaka kubwa (iliyotokana na fedha ileile waliyotuibia)? Au maadili tunayodai Waziri Mkuu Cameron anayapuuza ni haya ya wengi wa wasanii wetu wa kike kwenye fani ya filamu ambao licha ya kupendelea kuvaa nusu uchi, hawana mishipa ya aibu kutangazia umma uchafu wanaofanya katika maisha yao? Maadili haya ya wasanii wa Khanga Moja na Kitu Tigo wanaoigiza u-Sodoma na Gomora hadharani kwa kisingizio cha burudani lakini hakuna wa kuwachukulia hatua?

  Ni maadili gani anayozungumzia Kikwete na Waziri wake Membe ilihali katika hotuba yake iliyogusia mafisadi wa EPA alikumbushia umuhimu wa haki zao za binadamu (na ikambidi aliyekuwa Spika, Samuel Sitta, amkumbushe Rais kuwa haki za wananchi ni muhimu kuliko za mafisadi)?
  Mbona hakukuwa na maandamano ya kumlaani Kikwete kwa kutetea haki za binadamu ambao ni mafisadi lakini leo tunawalaani Waingereza kwa kutishia kutunyima fedha zao kama tusipofuata matakwa yao?


  Lakini unafiki mkubwa zaidi ni huu: viongozi hawa hawa ambao licha ya kukiri hadharani kuwa hawajui kwa nini nchi yetu ni masikini (labda pia hawajui kwa nini waliamua kutuongoza) pia ni washiriki wakubwa wa ufisadi unaotufanya tuishi kwa kutegemea fadhila za wafadhili kama Uingereza, wanatuhadaa kuwa ni bora tunyimwe misaada kuliko kukiuka maadili yetu. Lakini wababaishaji hawa hawatuambii jinsi watakavyofidia pengo litakalotokana na kukatwa misaada hiyo.


  Na hawatuambii kwa sababu hajui watafidia vipi na hawajali kwa vile wao hawataathiriwa na kukatwa misaada hiyo. Na kama ambavyo tatizo la umeme linavyodumishwa na mafisadi ili kujaza akaunti za vijisenti huku nje, si ajabu tukikatiwa misaada mafisadi watapata kisingizio kipya cha "imebidi mabilioni haya ya shilingi yatumike kufidia pengo lililotokana na uamuzi wa Uingereza kutukatia misaada."

  Nimalizie makala hii kwa kutamka bayana kuwa kama ambavyo sipingi uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa vile hainihusu mie Mkristo, sina tatizo na kurekebisha sheria za ushoga kwa vile si tu mashoga wapo na wanazidi kuongezeka (na hakuna anayewachukulia hatua kwa kuvunja sheria) lakini pia sheria hizo hazinihusu mimi au yeyote yule asiye shoga.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tuache tumche mungu km na wewe ushaiga ya wazungu dont spoil us please!!!
   
 3. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Tuichukulie kama tetesi tu, kwasababu mtoa taarifa ameshindwa kutaja hata shirika tu analodai kuongozwa na shoga, achilia mbali kumtaja shoga mwenyewe.
   
 4. k

  kipanga mlakuku Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hii taarifa imeandikwa kwenye gazeti makini Tanzania la Raia Mwema na inasemekana kuwa Chahali alimwaga mtama kwenye kuku wengi mambo yalikuwa hadharani sema kwa busara za mhariri ndiyo maana hakutajwa lakini Mbaraka Islam si yupo humu jamvini? aje hapa atueleze ukweli au yeye mwenyewe Chahali yupo humu aje hapa atueleze ukweli
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Jamani mbona anajulikana tu! Na kulikuwa na thread iliyomhusu yeye hapa hapa JF.
   
 6. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Eeeeeeeeeeeeehhhhhh maweeeee..infact nasaini out kwa kweli...narudi zangu kanyigo.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,436
  Likes Received: 22,352
  Trophy Points: 280
  David Cameroon Mataka alimkameruni Defao hadi akalazwa.
   
 8. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45

  Hapa namkumbuka kigogo mmoja wa Shirika la ndege aliyestaafu na kujifu kuwa amealiacha shirika ndege likiwa na nembo yake. I am just speculating!!!!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 10. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwani neno Mataka limekua gumu kutamkwa mpaka mzunguuuuke!
   
 11. r

  rutakolwakolwa Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahahaahah,mie simo!!
   
 12. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 180
  Hii ndio JF! Hakuna siri hapa
   
 13. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ingawa siungi mkono kuhalalisha ushoga TZ, lakini hii habari is an eye opener na ningefurahi kama ingeaandikwa kwenye magazeti ya Tanzania.

  Kwanza tumefahamu kwamba Cameron alikuwa anawakilisha mawazo ya wananchi wake ambao ndio pesa zao zinatumika kutupatia misaada, Cameron ni kiongozi mzuri kwa Waingereza because anawakilisha masilahi yao.

  Pili tunaomba viongozi wetu including Membe na JK, watuambie kama UK itatunyima hiyo misaada je hilo pengo watalifidia vipi? Haya ni maswali magumu ambayo inabidi tuwaulize viongozi wetu.

  Tatu huyo kigogo anayesemwa na Chahali aliwahi kuwa mkurugenzi wa PPF, baadaye ATC na amestaafu mwaka huu tu kwa majivuno makubwa, anafahamika sio SIRI.

  Mwisho na mimi nitaficha identity yangu kwa kutotaja majarada ya kisayansi. Lakini niliwahi kufanya utafiti wa Men having Sex with Men (MSM) na Heterosexual Anal Sex (HAS) hii ya pili haihusiani na ushoga. It is known scientifically that MSM and HAS fuel transmission of HIV. Tulitaka kujua incidence ya vitendo hivi Tanzania ili TACAIDS iweze kupanga intervention strategies targeting those "special" groups. Tulitumia method inayoitwa SNOW BALL. Believe it or not tulikuta MSM and HAS was more prevalent mikoa ya Pwani na Zanzibar and respondents said that, those practices are common in those areas (Read TACAIDS reports). Hakuna mtanzania ambaye hajasikia, banda la uwani, TIGO, Ma-Aunty Moddy etc

  Hivyo vitendo vipo na serikali imevibariki kimya kimya. Kama kweli serikali inapinga ushoga to which I support basi ipinge kwa vitendo sio kwa maneno ya majukwaani.
   
 14. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #14
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Mataka alikuwa shoga mmegaji sio mmegwaji? Duh! Tushazoea tetesi za mabinti kupata kazi kwa kutoa tunda kwa bosi sasa wale vijana waliopata kazi kwenye hlo shirika enzi za Mataka....dah! I don't mean anything.
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,684
  Likes Received: 21,947
  Trophy Points: 280
  Ayaaa! Safari ni safari umeua bendi mkuu.Lol
   
 16. mwenyenchi

  mwenyenchi JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Haahaahaaa! JF inatisha! Kumbe kweli!
   
 17. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,076
  Likes Received: 7,566
  Trophy Points: 280
  The yule waziri wa affairs of 'outside' anadanganya watu kuwa mkuu alimkataa balozi aliyefunga ndoa na mwanaume mwenzako?
  Kama ningine za kitoto sana yule waziri ni kama Comical Ally.
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Kweli nimeamini JF ni buyu kavu halifichi mbegu. Si na Macheni naye jamaa alikuwa anam-Cameroni?
   
 19. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #19
  Nov 11, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ufedhuli wao huko huko
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  mwandishi, tafadhali simama na uangalie nnyuma, mbele kushoto pia kulia....

  ni kweli na hakuna aliyekataa kuwa kundi hili la watu lipo tanzania....

  lakini ishu ni kwamba nchi za dunia ya tatu zina chamgamoto nyingi za kutatua kiuchumi na kijamii na sio hilo la ushogo...

  in fact haijawahi kuwa changamoto kama inavyodaiwa...........

  hapa kuna mambo mawili Cameroon alikuwa anafanya....

  1. kutest zali la mwitikio wa mziki wa ulaya barani afrika hasa baada ya anguko la tawala conservative za kiarabu

  2. anajua wazi kuwa hana hea za kutupa sie wa dunia ya tatu hivyo anatafuta kijisababu cha kujustify hilo!

  3. i am personally worried that he him self is a gay......

  but always history has shown that Africa saves the world always. because we aere the kings.....

  even Jesus our lord found his salvage in Africa when Pharao wanted to sneak his head out!

  we also read that its the black man who helped jesus with his cross

  chao!
   
Loading...