Eva Spegiel: Ukimuigia huyu jamaa na wewe unaweza kuwa bilionea

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,444
ad7317f033fe0e5d8790d4ed0bae7b32.jpg


Kwa zamani, dunia ilionekana kuwa kubwa, labda kwa sababu hakukuwa na mitandao mingi, kulikuwa na ugumu wa kupata habari kutoka sehemu nyingine za dunia, yaani kama upo Tanzania, ilikuwa vigumu kupata taarifa kuhusu Marekani.
Sasa hivi dunia ni kama kijiji, tukio linatokea Marekani, ndani ya dakika tano, na wewe uliyepo Tanzania unaliona, tena wakati mwingine kuangalia moja kwa moja.

Watu wenye kuthubutu, watu wasioogopa kupoteza pesa, wenye kutaka mabadiliko na kuwa mabilionea wakathubutu kuleta mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Beashare, ila kwa leo tunakwenda kumfahamu zaidi jamaa aliyeanzisha mtandao wa Snapchat ambao umempa utajiri wa dola bilioni 4.9 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 10.
Huyu ndiye Evan Spiegel

Jamaa alizaliwa mwaka 1990. Ni kijana mdogo tu ambaye ameonyesha mabadiliko makubwa katika masuala ya mitandao ya kijamii. Wazazi wake ni wanasheria, mama yake anaitwa Melissa Ann Thomas na baba yake anaitwa John W. Spiegel.
Alikulia huko Los Angeles, California nchini Marekani. Miongoni mwa watu wanaosadikiwa kuwa na akili nyingi basi yupo huyu jamaa ambaye alisoma masomo ya sayansi katika shule Crossroad, shule ambayo hufundisha masomo ya sayansi na sanaa hukohuko Los Angeles.




AJIUNGA NA CHUO, AFANYA KAZI BURE.
Japokuwa wazazi wake walikuwa wanasheria lakini anasema kwamba hakuwahi kufikiria kuwa mwanasheria. Alitaka kuwa injiania kwa kuwa aliamini huko kuna pesa nyingi.
Alipomaliza shule, akajiunga na Chuo cha Stanford ambacho ni maarufu sana nchini humo. Hata kabla hajamaliza, akaamua kuongeza ujuzi mwingine katika kichwa chake, alitaka kuwa mbunifu wa masuala ya mitandao mbalimbali. Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa hivyo kuamua kwenda kufanya kazi katika kinywaji cha Red Bull ambapo huko aliamua kufanya bure kabisa.


AONDOKA CHUO, ATENGENEZA SNAPCHAT.
Mwaka 2012, jamaa aliamua kuondoka katika Chuo cha Stanford na kuamua kuanzisha mtandao wake. Lilikuwa wazo la kipindi kirefu ambalo muda huo alitaka kulifanyia kazi kwa haraka sana.
Aliangalia mitandao mingine kama Facebook, Twitter, aliona kabisa jinsi jamaa walivyokuwa wakitengeneza pesa, hivyo akaona kwamba kama na yeye angetengeneza mtandao wake, angepiga pesa.
Mwaka huohuo wakati akiwa amekwishafanya utafiti, akaanzisha mtandao huo. Mbali na Facebook ambao ulikuwa ukipatikana zaidi kwenye kompyuta kipindi hicho, mtandao wake akauweka kwenye simu, ulikuwa na mvuto na kila mtu aliyeuona kipindi hicho alivutiwa nao.


MARK ZUCKERBERG ALIJARIBU KUUNUNUA, AKASHINDWA.
Mwaka 2013 baada ya kuona Snapchat inakua kwa kasi, mmiliki wa Facebook, WhatsApp na Instagram, Mark Zuckerberg aliweka dola bilioni 3 (zaidi ya trilioni 6) kuununua mtandao huo lakini Spiegel na Murphy wakakataa.




AAMUA KUCHUMBIA.
Japokuwa mwanzo mwa mwaka 2016 mshikaji alihusishwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki, Taylor Swift, ikumbukwe kuwa mwaka 2015 aliamua kumchumbia msichana Miranda Kerr ambaye yupo naye mpaka sasa.





TUNAJIFUNZA NINI KUPITIA SPIEGEL?
Kitu ambacho mshikaji alikifanya ni kuangalia fursa. Alijua kwamba dunia ilikuwa ikiendelea, aliwaangalia vijana wenzake walivyokuwa wakiingiza pesa kupitia mitandao ya kijamii, hakutaka kuchelewa, naye akaingia humohumo, kweli akatusua.

Hebu angalia hapo unapokaa kuna fursa ngapi unaziacha. Wengine wanaogopa kupata hasara, kupoteza pesa, ndiyo! Unapoamua kufanya biashara ni lazima upate hasara kabla ya kupata faida.
Mbali na furasa, ni lazima kuwe na ubunifu katika biashara yako kwa ajili ya kuleta upinzani. Jamaa aliangalia mitandao mingine, alichokifanya ni kutengeneza mtandao ambao aliweka ubunifu ambao haukuwa ukipatikana Facebook kama kuweka Filter na vitu vingine.

Unapoanzisha biashara hivyo ni vitu vya kuangalia sana. Hukatazwi kufanya biashara kama fulani, unaruhusiwa japokuwa unatakiwa kuongeza ubunifu ili uonekane kuwa tofauti na wengine na utengeneze pesa.



 
Wayahudi wanabebana wewe, unaweza kutengeneza solution yako nzuri mno, lakini media zinazomilikiwa na Wayahudi zikaipa promo ya mwenzao ikawa maarufu kukushinda!!.

Kabla ya Facebook ilikuwepo myspace, Hi5 ziliishia wapi?
 
Elimu, Mazingira, na hata pale tunapoanza matumizi ya kimtandao, bhasi akili na ukomo wetu unaishia ku create groups za whatsapp! tu swala zima la kujitambua ni muhimu kwa kila Mtu, Lakini hua nakuja kuishiwa nguvu kwenye suala zima la support kwa kile ambacho unaonekana kukipenda na kukifanya maishani hili ni tatizo sana kwa nchi za kiafrika.
 
Back
Top Bottom