Eva aliongea mengi na Shetani, sisi tukaambulia tu kulishwa tunda

Huyu shetani ni lini alianza kula mademu..
Hichi kitu akijawahi kuexist kwa namna ya mtazamo wenu au tafsiri...

Eva/Hawa hawajawahi kuexist popote pale, shida haya maandishi mnayasoma kama story za mapenzi...
Hahaha!! Kweli mkuu hizi ni fairy tales tu...
 
Na ndiyo maana YESU KRISTO mwokozi wa Wanadamu hakuwa "uzao" wa mwanadamu, KRISTO hakutokana na mbegu za kiume za kibinadamu sababu mbegu hizi zilishakuwa "corrupted" na tunda alilokula Adamu. Ili YESU KRISTO aweze kumshinda shetani na atuokoe sisi kutoka kwenye dhambi na kifo ilibidi Roho yake ishushwe moja kwa moja kutoka Mbinguni na kuingizwa kwenye tumbo la Maria tena akiwa bikira kabisa.
Hivyo YESU akachukua mwili wa kibinadamu kutoka kwa Maria lakini akiwa na ROHO ya MUNGU. YESU alikuweko Mbinguni kwa MUNGU kabla hajazaliwa duniani. Hili ni fumbo, wenye hekima na akili wataelewa.
Mkuu kama mbegu za kibinadamu zilikuwa corrupted,je Bikira Maria alikuwa uzao wa Nani?
 
Matokeo ya mwisho ndio huwa na taswira halisi ya jambo, na wakati mwingine ndio hupelekea hatua ya mwanzo ya uchunguzi(investigation)
 
WARNING: This thread is highly Critical:

1. Eva aliongea na Shetani ana kwa ana, akatuletea tu Tunda...tukaonekana tumemsaliti Mungu wetu, Je, ni nani Msaliti halisi?

2. Ni wapi nitapata maongezi ya Eva na Shetani ambayo hayajaandikwa kwenye Biblia? Ikumbukwe maongezi yao tulioyonayo sasahivi ni Mrejesho wa mazungumuzo yao na sio Transcript. Kama watu wanaweza kujua Binadamu wa kwanza aliishi Tanzania, kupata maongezi haya sio ishu.

3. Dini, Siasa na Fedha: nani muhusika mkuu wa haya matabaka?

Biblia na vitabu vingine vitukufu vya dini vimeandika yale tu yaliyoonwa rohoni na hadharani na maandishi mengine ambayo kwa nasibu (bahati) yalipatikana hivyo siyo kila kilichotokea enzi za Adamu na Hawa kiliandikwa, na hii ni kwa kuwa wao wenyewe (Adamu na Hawa) hawakujua kusoma na kuandika, kuchonga wala kuchora hivyo hawakuacha maandishi wala michoro yoyote kwa ajili ya kumbukumbu za baadae (Sidhani kama walikuwa na muda huo).

Habari za Adamu na Hawa zimekuja kuandikwa na watu waliofunuliwa kiroho (kiimani). Lakini pia mambo ya mahusiano huwa ni siri ya waliomo humo mpaka pale mmoja wapo au wote wanapoamua kutangaza siri hizo hivyo usitegemee kupata maandishi nje ya biblia zaidi ya kukutana na story za "ONCE UPON A TIME" maana sayansi inasema mtu wa kwanza alikuwa nyani (japo siamini) na pia sayansi inakataa uumbaji.
 
Angalia usije haribu kazi na riiziki za watu.
Mengine ni ya kufumba macho na ya kufunikwa kama huyaoni vile ,ili maisha yaendelee.
 
Hapo ndio tunaanza kusikiliza sauti za nyimbo mbali mbali wakati huooo kashavuliwa mtu
Kwenye mahusiano huwa kuna siri nyingi zisizosemwa kuanzia kutongozana mpaka inapofikia hatua ya kuvuana chupi
Matokeo ya kitendo hicho ndio huwa na sauti kubwa kuliko mengine yote yaliyotokea mwanzoni
 
WARNING: This thread is highly Critical:

1. Eva aliongea na Shetani ana kwa ana, akatuletea tu Tunda...tukaonekana tumemsaliti Mungu wetu, Je, ni nani Msaliti halisi?

2. Ni wapi nitapata maongezi ya Eva na Shetani ambayo hayajaandikwa kwenye Biblia? Ikumbukwe maongezi yao tulioyonayo sasahivi ni Mrejesho wa mazungumuzo yao na sio Transcript. Kama watu wanaweza kujua Binadamu wa kwanza aliishi Tanzania, kupata maongezi haya sio ishu.

3. Dini, Siasa na Fedha: nani muhusika mkuu wa haya matabaka?
Tcra watakuwa wameyahifadhi
 
Back
Top Bottom