keithevans2685
Senior Member
- Dec 17, 2014
- 110
- 46
"Ushoga ni kutamani kuingilia mtu kinyume na maumbile"Maswali hayo yote aliwahi kuulizwa Yesu Kristo:
Yohana 9:1-3 "Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake."
Hayo yote unayoona kuwa ni udhaifu (ulemavu), Mungu ameyaweka yatokee ili utukufu wa Mungu udhihirishwe.
Sasa basi turudi kwenye hoja ya Ushoga: Dhambi ya shoga ni kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile, na siyo kuzaliwa na homoni za kike (By the way, wengi wao wanahomoni za kiume, ila hujifunza kwa kuiga). Ndio, anaweza akawa amezaliwa na homoni za kike nyingi zilizo zidi homoni za kiume, lakini hii haimaanishi kuwa aliumbwa afanye ngono kinyume na maumbile, la hasha!! Maana yake ni hii, kwa kuwa amezaliwa na jinsi ya kiume lakini hana homoni za kiume, basi hakupewa uwezo wa kufanya tendo la Ngono, hivyo basi yamfaa atulie, asifanye ngono. Maana Mungu alipomuumba Adam,alimuumba na Hawa, kwa hiyo ngono ni kati ya Mtu Mume na Mtu Mke tu. Kwa maelezo hayo, nitakuwa nimejibu na maswali yako mengine, endapo mwanamke amezaliwa bila kizazi, basi si makosa ya Mungu, la hasha!! Lakini Mungu ameruhusu hivyo ili utukufu wake udhirishwe. Tena basi, mwanamke aliyezaliwa na udhaifu huo, haimpi ruhusa kwenda kuiba mtoto wa mwenzake, eti kisa yeye alizaliwa bila kizazi. Pointi ni kwamba, kuumbwa na udhaifu fulani, haikupi ruhusa ya kufanya dhambi!!
Barikiwa Mtumimishi!!
Nope Ushoga ni matamanio ya mtu wa jinsia yako,wapo mashoga kibao ambao wako kwenye mahusiano na hawaingiliana kinyume cha maumbile,kama walivyo wanaume wengi wanaopenda kuingilia wanawake kinyume na maumbile na wapo kibao wasiopenda kufanya mchezo huo,hao sio mashoga bali wanapenda aina hiyo ya ngono.
Wasagaji ni watu wanapenda au wenye matamanio ya mtu wa jinsia yao,sio watu wanapenda kunyonya maziwa au uchi wa mwanamke,ukisema hivyo basi wanaume wote wanaopenda kunyonya uchi wa wanawake pia ni mashoga.
Ushoga na Usagaji ni matamanio ya jinsia fulani sio ya ngono fulani.
Kusema "Mungu anatengeneza mapungufu" kwenye uumbaji wake ili aonyeshe uwezo wake ni swala la ku'justify ujinga kwasababu,Mungu huyohuyo ambaye ni so perfect, omnipotent,omniscient anatengeneza binadamu ambaye ana matatizo,anakuja kuhangaika duniani for what!!?ili adhihirishe "utukufu" wake!!?
Mungu wako wenye nguvu zote na uwezo wote, alikuwa na njia ngapi kubwa na nzuri zaidi za kudhihirisha hayo makuu yake mpaka aweke mapungufu katika mwili wa binadamu ili aje ahangaike hapa duniani!!?eti kukuonyesha ukuu wake!!?
Btw hiyo inaharibu kila msingi wa Msemo mnaopenda wakristo "Mungu ni mtu wa upendo sana"Benevolent God,ambaye ana uwezo wa kupenda creation yake sana mpaka kuiwekea cancer ya ubongo kwa mtoto wa chini ya miaka 5,huo ni ujinga wala si utukufu wa uumbaji.
Lastly kwasababu A,B,C vimesemwa kwenye Bible haimaanishi A,B na C ndio ushaidi(Facts, Evidence)wa kitu fulani,biblia ni kitabu tu cha collection ya maelezo mostly hadithi zilizoandikwa miaka 2000 iliyopita,sio ushaidi wa kuwa kuna Mungu wala huyo Mungu anataka nini.
Ukitaka ku'argue rational,jaribu sana kutotumia biblia bali tafuta Evidence na Fatcs.