Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Kilichotokea kwenye Mchezo wa Fainali za Euro uliopigwa katika Dimba la Wembley kati ya Italy na England kwa 80% watu walikifahamu ila tu kwa kuwa mpira ni mchezo ambao mara nyingi hautabiriki ndio maana kuna waliokuwa na wasiwasi kuwa England wangeweza pata matokeo.

Kwa maandalizi ya timu Italy waliandalia vizuri sana na ndio maana tangu mchezo wa kwanza dhidi ya Turkey mpaka Fainali dhidi ya England walionekana kupambana kama timu na sio kupata ushindi kwa kubahatisha.

Ukiangalia hata uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ni wazi kuwa Italy walikuwa na timu ya ushindi zaidi ya timu ya England.
Na hata ukiangalia kwenye dakika 120 za mpambano ule utaona wazi wachezaji na Kocha wa England walizidiwa mbinu na Italy walitawala Mchezo kwa muda mwingi sana.

Sambamba na hilo Italy tangu hatua ya robo fainali walipewa Belgium na walionesha kiwango bora na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1.

Kila Mtu anaukumbuka Mchezo wa nusu fainali ambapo Italy alipewa Spain na walifanikiwa kupambana na kupata ushindi.
Hii ilionesha wazi kuwa Italy wapo na timu imara ambayo ingeweza kupata matokeo kwa timu yoyote kwenye mchezo wa fainali.

Uzoefu wa walinzi wa Italy wakiongozwa na Mwamba Giorgio Chielini akiambatana na Leonardo Bonucci huku viungo watatu Joji, Veratti na Barella, ile hali washambuliaji hatari Lolenzo, Cirlo na Federico walionesha kucheza kama timu na pia kuwa tayari kupambana kwa ajili ya taifa la Italia.

Italy kwenye mchezo wa fainali waliingia kwa ajili ya kupambana na kupata matokeo, ile hali England hawakuandaliwa kwa ajili ya kupambana bali waliingia huku akili za wachezaji wao zikiwaza ni jinsi gani watalipuka Insta na Snap na baadhi ya mitandao mingine ya kijamii.

England waliingia uwanjani huku wakiwaza Bata litakuwaje baada ya kupata ushindi, ile hali Italy waliingia huku wakiwaza kupambana kiume hadi kuondoka na kombe kwenye Ardhi ya England.

Hivyo kwa aina ya maandalizi waliopewa timu zote mbili, Italy walipewa maandalizi mazuri kisoka ile hali England walipewa maandalizi mazuri ya sherehe.

Italy walifika fainali kwa uwezo na kujiamini ile hali England walifika kwa bahati mbaya.
Hili limethibitika pale kwenye hatua ya penati kwani wachezaji wa Italy walikuwa na utayari ile hali England wengi wao waliokwenda kupiga walionekana kusukumwa, sambamba na baadhi ya wachezaji kukataa kupiga mikwaju hio ya penati.

Waingereza wamebaki kulaumu baadhi ya wachezaji wao wenye asili ya Afrika waliokosa mikwaju ya penati, lakini swali ni je nani alikuwa tayari kwa ajili ya kupiga Matuta?!

Ukweli na usemwe, japo utawaumiza baadhi ya Watu.
Ukweli ni kuwa Italy walistahili kubeba hili kombe.
Italy ni timu kamili ambayo ina wachezaji imara ndani ya uwanja na hata waliopo kwenye benchi.
Italy ni timu ambayo ilikwenda kwenye mashindano huku inajuwa inakwenda kwa ajili ya kitu gani.
Italy ilikuwa ina wachezaji wenye uwezo wa uongozi ndani ya uwanja na kwenye benchi pia.
Italy wana mwalimu mwenye mbinu na uwezo wa kusoma mbinu za adui yake alizokuja nazo.

Kwa kifupi itoshe kusema Italy walistahili kuwa mabingwa wa Ulaya.
Na ibaki hivyo.

Forza Azzurri.
 
Dah
IMG_20210712_081921.jpg
 
Ifike wakati tujiamini bila kuangalia rangi,ukiwa na mind ya kuhisi kubaguliwa kwa ajili ya rangi hata kitu kidogo utahisi unabaguliwa ,

Ndio uhalisia, watu weusi tunajibagua wenyewe.
Yani ukipewa tusi tu unaanza kuhisi ni kutokana na rangi yako,
Ukienda kuposa ukikataliwa unaanza kuhisi ni kwa sababu ya rangi yako
 
2012: Immobile, Verratti and Insigne win Serie B together with Pescara

2021: Immobile, Verratti and Insigne win #EURO2020
together with #ITA

From the second division to European Champions. What a journey it's been for Italy's three musketeers

@Goal233
IMG_20210713_165520_771.jpg
IMG_20210713_165558_586.jpg
IMG_20210713_165614_222.jpg
IMG_20210713_165618_340.jpg
 
Tuliwambia mapema humu, ila kuna watu walikuwa wabishi sana. ITALIA NDIO TIMU BORA DUNIANI KWA SASA
 
Back
Top Bottom