EURO 2020: Kundi la kifo, Kundi F kuzikutanisha Ufaransa, Ujerumani na Ureno

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Habari!

Tayari baadhi ya timu zimekwisha kupangwa katika makundi kwa ajili ya mashindano ya 'UEFA EURO 2020', droo iliyofanyika mjini Bucharest nchini Romania ingawa bado haijakamilika huku Kundi 'F' likitajwa kama "Kundi la Kifo" litakaloyakutanisha mataifa matatu 'vigogo' wa soka barani Ulaya ya Ufaransa, Ujerumani pamoja na Ureno.

1575237849801.png

Hili ni kundi gumu sana pengine kuliko makundi mengine katika mashindano yajayo ya EURO 2020 na tutarajie soka na ushindani wa hali ya juu kutoka kwa timu hizi tatu au mataifa haya matatu mashuhuri barani Ulaya.

Tayari timu 24 zimekwisha kufuzu na bado timu nne (4) tu ambazo zitapitia mfumo wa 'Playoffs' (UEFA Nations League playoffs) na baada ya hapo droo nzima itakamilika.

Makundi yote katika droo;

Kundi A: Turkey, Italy, Wales, Switzerland

Kundi B: Denmark, Finland, Belgium, Russia

Kundi C: Netherlands, Ukraine, Austria, Mshindi wa Play-off D (A)*

Kundi D: England, Croatia, Mshindi wa Play-off C, Czech Republic

Kundi E: Spain, Sweden, Poland, Mshindi wa Play-off B

Kundi F: Mshindi wa Play-off A (D)*, Portugal, France, Germany

Mechi za 'Play-offs':

A
: Iceland v Romania, Bulgaria v Hungary
B: Bosnia and Herzegovina v Northern Ireland, Slovakia v Republic of Ireland
C: Scotland v Israel, Norway v Serbia
D: Georgia v Belarus, North Macedonia v Kosovo

Matokeo kamili ya 'Playoffs' yatakamilika panapo mwezi March 2020.

Kaa Chonjo!

Always THE GREAT
 
hizi ratiba huwa zinapangwa na waingereza?
mara nyingi sana kila yanapopangwa makundi anaweka sehemu nyepesi...
ok, waswahili wanasema bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi

FIFA world cup 2002
kundi F: england, argentina, sweden, nigeria

FIFA world cup 2006
kundi B: england, equador, trinidad tobago, sweden

FIFA world cup 2010
kundi C: england, algeria, slovenia, marekani

FIFA world cup 2014 (kawekwa sehemu ya afadhali katolewa makundi)
kundi D: england, italy, uruguay, costa rica

FIFA world cup 2018
kundi G : england, belgium, panama, colombia

euro 2000: katolewa hatua ya makundi
kundi A: england, portugal, romania, germany

euro 2004
kundi B: england, france, croatia, switzerland

euro 2008
hawakushiriki

euro 2012
kundi D: england, france, sweden, ukraine

euro 2016
kundi B: england, wales, slovakia, russia

euro 2020

Hahaha!

Bahati si kitu cha kutegemea sana ingawa ni kitu kizuri.

Haohao Waingereza wanatuambia; Goodluck comes with Miracles but not Promise.
 
Mkuu unazungumzia Portugal hii yenye benardo silva,Cr7 bruno, jao felix na vipaji vingine vipya lukuki?
Nahisi hayawafatilia Portugal hapa kati asingetamka hayo maneno kuna watoto wana kiwasha pale babu yao Christiano wamemuweka tu pale mbele wareno km Argentina wameamua kuwaamini vijana game na Brazil nilimuona Messi waliobaki wote hawana majina makubwa game ya nyuma yake kabla hiyo ya Brazil walishinda 4 sikumbuki walicheza na nani nilimfahamu Dimaria tu wengine wote vitoto hao Germany ilikuwa zamani nahisi pia hajawafatilia siku za karibuni!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom