EU yakanusha taarifa ya Balozi Van de Geer kutakiwa kuondoka nchini Tanzania

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Umoja wa Ulaya (EU) umekanusha taarifa zinazodai Balozi wa umoja huo nchini Tanzania, Reoland van de Geer ametakiwa kuondoka nchini Tanzania.

"Kiukweli ameitwa makao makuu kwa ajili ya kushauriana, juu ya siasa na uhusiano wa baadaye wa EU na Tanzania".

Imetolewa na Msemaji wa EU Tanzania.

••••••••••

Hapo awali kulikuwa na taarifa inayosema, Serikali imempa masaa 24 Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Reoland van de Geer kuondoka nchini Tanzania.

Van de Geer anatakiwa kutokuwepo ndani ya mipaka ya Tanzania ifikapo saa sita usiku wa kuamkia Novemba 4, 2018.
IMG_20181103_004306.jpeg
 
Ha ha..Aliyelianzisha amekosea kidogo plani, tungeshuhudia mengi yatakayojiri
 
Van de Geer anatakiwa ndani ya mipaka ya Tanzania ifikapo saa sita usiku wa kuamkia Novemba 4, 2018.

Anatakiwa kutoka wapi!?

Mbona hii habari inataka kuwa tata kama ya upatikanaji wa MO
 
Anatakiwa kutoka wapi!?

Mbona hii habari inataka kuwa tata kama ya upatikanaji wa MO
Sorry mkuu..anatakiwa kutokuwepo hapa nchini Tanzania saa 24 amepewa awe ametimua kwao
 
Asije kuwa alifadhili upatikanaji ea zile FORD RANGER!
Kwa vyovyote kosa wanalofanya hawa mabalozi ni kuingilia masuala ya siasa za ndani. Tuombee isiwe kweli maaana hao EU nao huwa wana visasi sana.
 
Hao wadachi wanakuwaga na roho ngumu sana subiri part two yake #jiwe unatakiwa ujipange
 
Umoja wa Ulaya (EU) umekanusha taarifa zinazodai Balozi wa umoja huo nchini Tanzania, Reoland van de Geer ametakiwa kuondoka nchini Tanzania.

"Kiukweli ameitwa makao makuu kwa ajili ya kushauriana, juu ya siasa na uhusiano wa baadaye wa EU na Tanzania".

Imetolewa na Msemaji wa EU Tanzania.

••••••••••

Hapo awali kulikuwa na taarifa inayosema, Serikali imempa masaa 24 Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Reoland van de Geer kuondoka nchini Tanzania.

Van de Geer anatakiwa kutokuwepo ndani ya mipaka ya Tanzania ifikapo saa sita usiku wa kuamkia Novemba 4, 2018.
View attachment 919524
Hii ninlugha ya kidiplomasia tu.
 
Back
Top Bottom