EU yammwagia sifa Rais Samia

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la ulaya akataa ripoti iliyoonesha matumaini ya mabadiliko ktk utawala wa awamu ya sita

David James McAllister MEP ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Ulaya ametoa hotuba nzito na kuwalaumu wataalum wa Umoja wa Ulaya waliotoa ripoti mbele ya kamati hiyo ya Bunge yenye ushawishi mkubwa pamoja na kuaminika kusimamia values / desturi na makubaliano ya kuheshimu haki za binadamu na utawala bora .

Mwenyekiti David James McAllister MEP akakumbushia barua yake aliyoandika kuwaonya wataalamu wa Umoja wa Ulaya EEAS mwaka jana mwezi November 2020 kuhusu "kuubeba" utawala dhalimu usiofuata haki za msingi za kibinadamu. Ripoti hiyo ilisema kuna maendeleo 'makubwa' nchini Tanzania mbali ya changamoto ndogo ndogo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya akakumbushia hicho kinachoitwa 'changamoto ndogo ndogo' kwa hakika ni kikubwa na hakipaswi kutupiliwa mbali ikiwa watu wanakamatwa ovyo, kutupwa mahabusu, kufunguliwa mashtaka, kutishiwa haki ya kuishi n.k mambo ambayo ndiyo msingi mkubwa wanaousimamia Umoja wa Ulaya wakati wa kutoa msaada kwa nchi yoyote ulimwenguni
EEAS - European External Action Service - European Union External Action
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya amesema mfano wataalamu hao je wameweza kukutana ndani ya Tanzania na mwenyekiti wa CHADEMA au makamu mwenyekiti wa CHADEMA? Ambao ni viongozi wa chama kikuu cha upinzani, mmoja akiwa rumande kwa kesi ya kutunga huku mwingine akiwa uhamishoni Belgium halafu wataalamu hao wanasema ni changamoto ndogo ndogo?

Pia kuna raia wanaoshiriki siasa Tanzania wenye mtizamo mbadala walio wanachama, wapenzi na wafadhili wazalendo wa KiTanzania wanabaguliwa kushiriki ktk vyombo vya maamuzi ngazi zote, wanaoozea ktk jela mbalimbali Tanzania au biashara zao kuhujumiwa je hayo ni mambo madogo ? Amehoji David James McAllister mwenyekiti huyo makini wa kamati ya Bunge la ulaya.

Hivyo amewataka wataalamu hao waliotumwa na bunge la Umoja wa Ulaya kuwabebeleza watawala wa Tanzania kuacha ukandamizaji, kujitathmini kama wanataka kulimwa barua nyingine kali ya karipio kuhusu ripoti yao iliyozua maswali mengi ndani ya Bunge la Ulaya na miongoni mwa wabunge wa Bunge hilo la Ulaya mwaka 2020 na vivyo hivyo pia mwaka huu mwezi November 2021 inayojadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la ulaya amewataka wataalamu hao kuja na majibu mujarabu ya kuibana serikali ya Tanzania kwa kuwa inatumia misaada ya Umoja wa Ulaya itokanayo na kodi za raia wa nchi wanachama zinazoamini katika utawala bora, haki za binadamu kulindwa na demokrasia hivyo haiwezekani nchi viongozi wa nchi walio wakandamizaji kama wa Tanzania kufaidi jasho na nguvu wa walipa kodi wa Ulaya wanaoamini katika uhuru, haki na Maendeleo ya kweli ya watu ktk demokrasia inayozingatia utu.

amesema yeye na wajumbe wabunge wa kamati ya mambo ya nje wanajiandaa kupendekeza hatua "kali" dhidi ya utawala unaoendekeza udhalimu waziwazi na kwa kificho.

David James McAllister mwenyekiti wa Kamati Ya Bunge la Ulaya ya Mambo ya Nje anasema mbali na ripoti hiyo ya wataalamu wake pia wanapata habari kupitia balozi za Marekani, Canada , Uingereza na balozi wa nchi wanachama wanaohudhuria kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya tuhuma nzito za kupikwa dhidi ya Mbowe na wenzie 3, na kesi hiyo ni kichekesho dhidi ya Umoja wa Ulaya na raia wa wa Umoja wa Ulaya ambao wote wanaamini ktk haki mbele ya sheria, demokrasia na kutokuwepo ugandamizaji wa haki za kibinadamu za aina yoyote.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge anataka kuona wataalamu hao wanakuja na mkakati gani wa kuibana serikali ya Tanzania inapotaka misaada na mikopo, kwani sasa siyo muda tena wa maongezi / dialogue yasiyo na kikomo kuhusu hali hii mbaya ya kisiasa nchini Tanzania, bali ni wakati wa Umoja wa Ulaya kufanya matendo kwani muda wa maneno umekwisha, ili ujumbe uwaingie watawala dhalimu.

David James McAllister political career started in 1998 becoming a Member of the State Parliament of Lower Saxony (until 2014) in Germany. He was also the Mayor of his hometown Bad Bederkesa from 2001-2002, Secretary-General of the CDU in Lower Saxony from 2002-2003, and Chairman of the CDU Group in the State Parliament from 2003-2010. He was Party Chairman of the CDU in Lower Saxony from 2008-2016. He served as Prime Minister of Lower Saxony from 2010 till 2013. Member of the CDU Executive Committee since February 2014. MEP since July 2014. Since November 2014 Vice President of IDU (International Democrat Union). Since October 2015 Vice President of the EPP (European People's Party). In the European Parliament, McAllister is Chair of the Committee on Foreign Affairs, substitute member of the Committee on International Trade and the Sub-Committee on Security and Defence, member of the Delegation for Relations with the USA and the Delegation for Relations with the NATO Parliamentary Assembly and substitute member of the EU-Serbia Stabilisation and Association Parliamentary Committee
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

<<<Sikiliza mpaka mwisho >>

Ukiendelea kudanganya tuka kufungia hapa
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

<<<Sikiliza mpaka mwisho >>

Hakika Rais Samia ni ngazi nyingine. EU inammwagia sifa kibao. Rais Samia oyeeeeeee. Watanzania tuko pamoja nawe
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

<<<Sikiliza mpaka mwisho >>

Spanner za EU hzaikuacha salama.

Haki, usawa, uhuru na demokrasia linabakia kuwa dukuduku kubwa la EU na serikali hii.

Uzi wako wa pili huu kwenye clip hiyo hiyo.

EU kutaka kesi ya Freeman Mbowe ifutwe hawajui kuwa Tanzania is a free State?

Uzi huu 180° out of phase. How possible?

Hiiiiii bagosha.
 
EU wanasema kweli kinyume kabisa na propaganda mfu za DAVID Mc ALISTER swahiba wake Tundu Lissu na yule Robert Amsterdam......

David Mc Alister mbunge wa chama Cha CDU kilichoshindwa uchaguzi huko UJERUMANI alipangana na wenzake pale BUNDESTAG kuupinga mradi wa UFUAJI UMEME pale MWALIMU NYERERE kwa kigezo dhaifu cha UHARIBIFU WA MAZINGIRA ilihali UNESCO ilijiridhisha pasi na shaka kuwa Tanzania itatumia tu 3% ya eneo lile......

Mjerumani huyo ana makasiriko makubwa dhidi ya Tanzania na serikali ya CCM........

#Siempre JMT
#Kazi Inaendelea Kwa Kasi & Weledi Zaidi
Unafahamu Kiingereza vizuri?
 
Wadau wenu wa maendeleo wamenza kuishtukia ccm juu ya uovu wao! Mataga yanashangilia TU huku hayajausikiliza mdahalo mpaka mwisho!
Mataga hiyo lugha iliyotumika imewakimbiza kabisa hapa jf! Acheni kuwabambikia watu wa cdm kesi za kubumba kwani mtakosa kusaidiwa kwenye bajeti zenu! Kuna barua Kali itawafikia hivi punde ambayo itanakiliwa A.S.A Kwa utekelezaji.
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

<<<Sikiliza mpaka mwisho >>

Kwa video hii, ndio maana Chief Hangaya leo aliwatembelea Warioba na Msuya...
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

<<<Sikiliza mpaka mwisho >>

Kwan hawa c ni mabeberu!
 
3019662_Mbowe_EU_Samia.jpg
 
Madhila aliyobainisha mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya wanayopitia wapinzani nchini Tanzania ni pamoja na hili huko Sumbawanga Tanzania :

02 December 2021

CHADEMA MKOA WA RUKWA KUMSHITAKI MKUU WA MKOA JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI

Source : CHADEMA MEDIA TV
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

Beberu siku zote ni lafiki ya watawala wanaolinda masrahi yao
 
02 December 2021

RAIS SAMIA AFIKA NYUMBANI KWA MAWAZIRI WAKUU WASTAAFU, JAJI WARIOBA na CLEOPA MSUYA!

Rais Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 2 Dec 2021, amewatembela mawaziri wakuu wastaafu jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa David Msuya hivi karibuni pia walijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuzungumzia hali ya kisiasa nchini na suala nyeti la watanzania wote wapate nafasi ya kuhusishwa katika ngazi za maamuzi na kutunga sheria bila kujali vyama au itikadi zao .

Source : Global TV online
KatibaMpya

24 Nov 2021 — WAZIRI Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya, amesema suala la marekebisho ya katiba haliepukiki Tanzania kwani Katiba sio jiwe au amri za torati

Toka Maktaba :

https://www.ippmedia.com › habari
Msuya: Marekebisho ya Katiba hayaepukiki - IPPMEDIA

24 Nov 2021 — WAZIRI Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya, amesema suala la marekebisho ya katiba hayaepukiki ... mahojiano na Kipindi cha ITV dakika 45

https://www.theeastafrican.co.ke › tea
Katiba is a must, says Tanzania's Warioba - The East African

13 Jul 2021 — Tanzanian constitutional reformist judge Joseph Warioba says President Samia Suluhu Hassan's government must implement changes in
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

Kama hujui kiingereza si ungemuuliza Polepole Mkuu wa chuo cha Uzezeta akufafanulie kuliko kujiaibisha hivi?
 
===
EU imemmwagia sifa kedekede Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania hasa kwenye Covid-19

EU inasema hali ya hewa kisiasa na Asasi za kiraia ni nzuri na imetengemaa na kila kitu kinakwenda vizuri nchi Tanzania,

EU imeahidi kuendelea kuifuatilia kwa karibu Tanzania na kuendelea kuisaidia katika nyanja mbalimbali,

<<<Sikiliza mpaka mwisho >>

Mama kamaliza kila kitu EU
 
Back
Top Bottom