EU waweka rehani trilion 2.182 za Tanzania, wabunge wa Uingereza wataka kukata misaada Tanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Siku chache baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), kufuta Tanzania kwenye nchi wanachama wake na hivyo kuikosesha serikali msaada wa zaidi ya Sh. trilioni moja kutokana na uchaguzi wa Zanzibar, Umoja wa Ulaya (EU), upo hatarini kutotoa Sh. trilioni 1.56 kwa sababu ya suala hilo huku mmoja wa Waziri wa Uingereza, akiitaka serikali yake isitoe Sh. bilioni 622 za msaada kwa Tanzania.

Kwa mantiki hiyo, Tanzania ipo hatarini kupoteza jumla ya Sh. trilioni 2.182 kutoka EU na Uingereza endapo haitaridhishwa na suala la Zanzibar linavyoendelea.

Tangu Juni, 2014, Tanzania na EU ziliingia makubaliano ya msaada wa Euro milioni 100 (sawa na Sh. bilioni 249), kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.

Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa jana na Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Habari, Luana Reale, EU imesikitishwa na namna uchaguzi wa marudio Zanzibar ulivyofanyika Machi 20, mwaka huu, baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Tunarudia wito wetu kwa serikali kuonyesha uongozi na kufanya mazungumzo ya pande zinazovutana katika maoni ya kuhakikisha amani na umoja vinaendelea kuwapo nchini,” alisema.

Alisema Tanzania na EU wako katika makubaliano maalum ya utekelezaji wa miradi kuanzia mwaka 2014 hadi 2020 iliyosainiwa Juni 2014, yenye thamani ya Euro milioni 626 (Sh. trilioni 1.56), ikiwa ni wastani wa Euro milioni 100 (Sh. bilioni 249) kwa mwaka.

Alisema kutoka kwa fedha na utekelezaji wa miradi husika, kunakwenda sambamba na makubalinao maalum ya ushirikiano yaliyojikita katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.

“Maamuzi juu ya ushirikiano wa maendeleo ikiwa ni pamoja na uamuzi wa mwisho wa kiwango cha fedha yatachukuliwa kwa msingi wa matokeo ya mazungumzo,” alisema.

Hata hivyo, haikueleza moja kwa moja kama wataendelea kuchangia bajeti kuu kama ambavyo wamekuwa wakifanya kila mwaka wa fedha.

Uingereza

Waziri wa zamani wa Ulinzi wanchi hiyo, Dk. Liam Fox, alililiambia Bunge la nchi hiyo liinyime Tanzania Paundi milioni 200 ambazo ilitakiwa kutoa kwa sababu ya sakata la uchaguzi wa Zanzibar.

“Walipa kodi wa nchi za Magharibi wanategemea fedha zao kutumiwa kwa njia za kimaadili..Sasa panapokuwa na ukiukwaji wa wazi wa haki za kisiasa au za binadamu, watategemea majibu kutokana na misaada tunayochangia.

“Ukweli ni kwamba Marekani imechukua hatua imara inatoa ishara nzuri…Tunapaswa kuwa tunafanya mapitio ya mchango wetu katika hali kama hiyo,” alisema.

Uingereza imekuwa ikifikia lengo lake la kutenga asilimia 0.7 ya pato lake kila mwaka, kwa ajili ya msaada kwa nchi za nje kutokea mwaka 2013, baada ya Idara kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), kufikia asilimia 32 kwa mwaka mmoja.

“Kuna sehemu nyingi duniani ambako tunaweza kuwa tunatumia msaada wetu kikamilifu kupunguza umaskini."

Kwa upande wake, Waziri wa zamani wa Mazingira na Mbunge Mwandamizi kutoka Chama cha Conservative, Owen Paterson, alisema DFID inapaswa kupunguza misaada yake kwa Tanzania, sambamba na uamuzi wa Marekani.

“Wizara ya Mambo ya Nje inasema uchaguzi si halali na tunaendelea kutumia fedha zetu vilevile, hii haiwezi kuwa sawa,” alisema Paterson.

“Wamarekani wamekiri kuwa njia hii haiwezi kuwa sawa na wamechukua uamuzi na sisi tunapaswa kuchukua uamuzi hapo hapo,”alisema.

Hali Ilivyo

Wiki iliyopita, Wizara ya Fedha na Mipango, ilieleza kuwa wahisani 10 kati ya 14 waliokuwa wanachangia mfuko wa bajeti ya Serikali Kuu wamejitoa na kuweka shakani upatikanaji wa Sh. trilioni 1.37 kwa bajeti ya mwaka huu ambazo zilitarajiwa kutoka kwa wahisani.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Servacius Likwelile, alisema waliobaki ni Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Dernmark na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

Wahisani wengine wa bajeti ya Tanzania ni Uingereza, Canada, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Norway na Sweden.

Dk. Likwelile alieleza kuwa kujitoa kwa wahisani hao kunatokana na changamoto zilizopo katika nchi zao na kwamba mchango wa wahisani katika bajeti ya mwaka 2014/15, ilikuwa trilioni moja, katika bajeti iliyofuata ilishuka hadi Sh. bilioni 800

Chanzo: Nipashe
 
Propaganda za kijinga sana hizi, nani wa kufanya hivyo hata huyo MCC ni mda tu atazitoa hizo pesa.
 
aliyemtuma jecha kuvuruga uchaguzi zanzibar ndiye mtu ambaye magufuli hata kaa amsahau ktk maisha yake yote.

Ukwel upo palepale magufuli ameuziwa mbuzi kwenye gunia
 
Siku chache baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), kufuta Tanzania kwenye nchi wanachama wake na hivyo kuikosesha serikali msaada wa zaidi ya Sh. trilioni moja kutokana na uchaguzi wa Zanzibar, Umoja wa Ulaya (EU), upo hatarini kutotoa Sh. trilioni 1.56 kwa sababu ya suala hilo huku mmoja wa Waziri wa Uingereza, akiitaka serikali yake isitoe Sh. bilioni 622 za msaada kwa Tanzania.

Chanzo:Nipashe
Maskini Nchi yangu tumekosea wapi?
 
Isue sio uchaguzi wala sheria ya mitandaoni,hivi ni vivuli tu wanavitumia baada ya kuona Rais hawashobokei wazungu,i am sure it will take time this way but we will come out STRONGER,by the way hii misaada yote ni hela zetu wenyewe wanazozichuma kwa kukwepa kodi kwenye rasilimali zetu na vile vile kutorosha rasilimali zetu.

Hakuna nchi iliwahi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nje.When life gives you lemons, make lemonade. It is time for Tanzanians to stand by our government. We must ensure that taxes are paid and ask for proper receipts when purchasing items to enable the government collect more revenue.

To show the world that we can stand on our own feet, we must produce more and stand by the president and his government in the resolve to take Tanzania to a different level of development.

Let us takes these moves as a ‘stab in the back’ impressing upon the government to forge ahead using domestic resources and fund our own development.

VIVA TANZANIA.
 
Jecha kawaponza na yule mliyomtuma kwa Jecha sasa subirini muanze kuisoma number na nyie wacheni kujitetea kwa ujinga
 
Turudishe kodi ya kichwa na mifugo....ili tuweze kujiendesha..
Mkuu Mwanga Lutila, serikali ianzishe kodi ya kujamiiana! Kwa kodi ya kujamiiana peke yake, serikali inaweza kuziba pengo la hizo trillion tatu tutakazonyimwa kwa kituko cha kuunga mkono ufedhuri wa Jecha.
 
magu sasa ataelewa kwann mkwere alikuwa anaenda nje zaidi ya msoga
 
Isue sio uchaguzi wala sheria ya mitandaoni,hivi ni vivuli tu wanavitumia baada ya kuona Rais hawashobokei wazungu,i am sure it will take time this way but we will come out STRONGER,by the way hii misaada yote ni hela zetu wenyewe wanazozichuma kwa kukwepa kodi kwenye rasilimali zetu na vile vile kutorosha rasilimali zetu.

Hakuna nchi iliwahi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nje.When life gives you lemons, make lemonade. It is time for Tanzanians to stand by our government. We must ensure that taxes are paid and ask for proper receipts when purchasing items to enable the government collect more revenue.

To show the world that we can stand on our own feet, we must produce more and stand by the president and his government in the resolve to take Tanzania to a different level of development.

Let us takes these moves as a ‘stab in the back’ impressing upon the government to forge ahead using domestic resources and fund our own development.
VIVA TANZANIA.

Una akili za kipuuzi kama Jecha!
 
kwa wale wenye mishahara mamilion ya pesa. hawatadhurika na lolote hata misaada yote ikatwe. Na ndio wanaotoa kauli kama hizi
 
Back
Top Bottom