EU vs Tanzania: Zijue sababu za EU Kuuma na Kupuliza

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,227
35,151
Ifahamike kuwa EU kama watu wana maslahi yao yaliyo wazi kwenye mahusiano yao na nchi yoyote.

Ya muhimu zaidi kwenye kuihusu Tanzania ni:

1. Usalama wao hasa dhidi ya Corona
2. Umuhimu wa uhuru, haki, usawa na demokrasia (kiutu).

#1 kwao ni kipaumbele. Kauli mbiu ya kuwa hayupo aliye salama hadi kila mtu awe salama ndiyo ulio msingi mkuu wa hitaji hili.

Kwa msimamo wa awamu ya tano kuhusiana na Corona, ni maoni ya EU kwamba Tanzania ilikuwa inaiweka dunia (ikiwemo EU) hatarini.

"Ikumbukwe kuwa (kitaaluma) jamii ya watu wasiochanjwa ndiyo ulio uwanja muafaka zaidi kwenye uzalishaji wa variants zingine za Corona ambapo Delta na Omicron ni mfano wake."

#2, EU kama binadamu mwingine aliyestaarabika hawezi kupendezwa na manyanyaso ya awaye yote kwa sababu tu ya umadhubuti wa musuli wa nguvu awaye yote anaweza kuwa nao.

EU wanakemea udhwalimu uliopo nchini kana wanavyokemea kwingine kokote. Wangependa kukemea zaidi. Ila wasingependa kuhatarisha kipaumbele chao (hapo kwenye #1) ambacho ni la muhimu zaidi kwao.

Katika maslahi mawili haya EU wamechagua kuuma na kupuliza:

Kuhusu Corona wasingependa turejee tulikotoka. Kwa hilo serikali inapewa incentives.

Kwenye haki za binadamu serikali inaaswa kidiplomasia mategemeo yakiwa kuwa iione busara yenyewe.

#2 si kipaumbele kwa EU japo ni muhimu. Hili ni suala la kiutu (humanitarian) zaidi.

Jitihada zetu za kujinasua kutoka katika ukandamizwaji wetu ni muhimu ilikuwa kuweza kufikia suluhisho la mapema zaidi.

Kwamba pia sympathizers wapo, hilo ni added advantage.

----------
Asanteni EU, asante McAllister na asante Tundu Lissu kwa kusimama pamoja nasi katika dhiki.
 
Tanzakiza
JamiiForums-289452902.jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom