EU, USA should ban CCM leaders and their families ....

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,681
8,233
Tutoe shinikizo kwa EU na USA kuwapiga mkwala wa kwenda ulaya na marekani viongozi wote wa CCM pamoja na familia zao kwa wizi wa kura. Haiwezekani watuibie kura halafu waende kujichana kwa pesa zetu.

CHADEMA huu ni wakati wa kuanza kampeni kwa mabalozi na nchi zote marafiki ili hawa wanoko wakione cha mtema kuni.
 
Wenzao akina Brown na leo Obama wamekubali kushindwa lakini Mkwere hataki, tuone kama wataendelea kum-support...
 
Hayo ndiyo mambo yalikuwa yanafanyika ZNZ, ktk muda wote huo wa kupinga matokeo, na matokeo yake ZNZ iliwekewa vikwazo fulani vya uchumi. Nani anaeumia? ni MTZ na siyo CCM.
Tuache mambo ya kwenda kwa Wazungu kudai haki zetu. Sisi wenyewe WTZ tunaweza kufanya mambo yetu bila ya hao Wazungu.
 
haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. mabadiliko yako mikononi mwetu,tukiamua kama krgstan walivyoamua watang'oka, wataondoka na tutawasahau kabisa
 
Hayo ndiyo mambo yalikuwa yanafanyika ZNZ, ktk muda wote huo wa kupinga matokeo, na matokeo yake ZNZ iliwekewa vikwazo fulani vya uchumi. Nani anaeumia? ni MTZ na siyo CCM.
Tuache mambo ya kwenda kwa Wazungu kudai haki zetu. Sisi wenyewe WTZ tunaweza kufanya mambo yetu bila ya hao Wazungu.

Ndugu yangu Shamu acha mawazo mgando. Nchi yetu si maskini ndio maana tumemkubali Dr. wa kweli ili tuondokane na ombaomba. Ahadi nyingi za JK zinategemea bakuli la kuomba omba hii misaada na mikopo mingi tunayoomba haijaleta mabadiliko makubwa. Ogopa mtu anayeenda kuomba msaada wa kujengewa vyoo na neti za mbu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ukweli ni kwamba serikali corrupt kama ya CCM kamwe haitaendesha uchaguzi huru na wa haki wala kuikubali katiba itakayowaweka wanaojiita chama tawala sawa na vyama vingine.

Hili linawezekana tu kupitia mbinyo wa vikwazo toka kwa wakubwa wa ulaya na Marekani wanaoabudiwa sana na viongozi hawa ombaomba. Viongozi wengi wa kiafrika ni wala rushwa, ving'ang'anizi wa madaraka hata kama kuwepo kwao uongozini ni mzigo na hasara kwa wananchi wao na ni wepes mno kulindana.

Hebu chukua mifano ya kina Mugabe, Museveni, Kibaki na sasa Kikwete anayeitumia serikali kubadilisha matakwa ya umma uliomkataa kwenye sanduku la kura. Ni rahisi kwa viongozi hawa kuwasikiliza wakubwa wa Ulaya na Marekani kuliko wananchi wanaodaikuwatumikia.

Ni kweli vikwazo vinaweza kuumiza lakini ndiyo njia pekee ya kuwashughulikia viongozi wala rushwa hawa ambao ni ving'ang'anizi wa madaraka mithili ya nyani ambao wakishapanda mitini ni vigumu kuwatelemsha labda baada ya nguvu kutumika.

Wote tumeyaona matokeo bada ya uchaguzi yakiwa yamebandikwa kwenye vituo nchi nzima na hesabu ya nani alipata kiasi kipi tunaijua lakini hizi takwimu zinazosomwa na tume zinatoka wapi kama si za kughushi kwa nia ya kumbeba kiongozi huyu ambaye waziwazi amepoteza mvuto aliokuwa nao miaka mitano iliyopita alipoingia madarakani!

Ni kweli Tanzania ni kisiwa cha amani, lakini kama serikali itaendelea na siasa za kibabe na kidikteta kama inakoelekea sasa, ni bora ulaya watusaidie kuwakumbusha kwa kuwawekea vikwazo angalau ya kwenda kuzurura huko ili ujumbe uwafikie na wajirekebishe.
 
Tutoe shinikizo kwa EU na USA kuwapiga mkwala wa kwenda ulaya na marekani viongozi wote wa CCM pamoja na familia zao kwa wizi wa kura. Haiwezekani watuibie kura halafu waende kujichana kwa pesa zetu.

CHADEMA huu ni wakati wa kuanza kampeni kwa mabalozi na nchi zote marafiki ili hawa wanoko wakione cha mtema kuni.

Mimi kama Mmarekani sioni sababu ya viongozi wa Tanzania kupigiwa mkwala. Uchaguzi umefuata katiba yenu. Ni katiba yenu inayosema kuwa rais ateue mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, na watu wengine wanaoweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi. Hivyo mtu aliyopo madarakani akishinda kwa kutumia madaraka aliyopewa kikatiba, hayo ni matatizo yenu.
 
- Great Thinkers tunatakiwa kuandika na evidence, pamoja FACTS hasa ishu nzito sana kama hii ya kuiba kura na huku wasimamizi toka nje wakiwepo au?

William.
 
Mimi kama Mmarekani sioni sababu ya viongozi wa Tanzania kupigiwa mkwala. Uchaguzi umefuata katiba yenu. Ni katiba yenu inayosema kuwa rais ateue mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, na watu wengine wanaoweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi. Hivyo mtu aliyopo madarakani akishinda kwa kutumia madaraka aliyopewa kikatiba, hayo ni matatizo yenu.

- Mkuu mwezi wa Sita, nilikuwa bungeni siku ya Bajeti nikamuuliza Waziri wa Sheria, vipi kuhusu katiba kubadilishwa maana wabunge wa Upinzani wakiwa nje ya bunge wanalia sana na katiba, akasema kwamba hata siku moja hawajawahi ku-raise hii ishu ndani ya bunge officially, never!

- Wasimamizi wa kimataifa wa huu uchaguzi wamesema kwamba Tanzania tunasumbuliwa na katiba yetu ya zamani sana iliyoundwa specifically kwa ajili ya utawala wa chama kimoja!

William.
 
- Mkuu mwezi wa Sita, nilikuwa bungeni siku ya Bajeti nikamuuliza Waziri wa Sheria, vipi kuhusu katiba kubadilishwa maana wabunge wa Upinzani wakiwa nje ya bunge wanalia sana na katiba, akasema kwamba hata siku moja ku-raise hii ishu ndani ya bunge, never!

- Wasimamizi wa kimataifa wa huu uchaguzi wamesema kwamba Tanzania tunasumbuliwa na katiba yetu ya zamani sana iliyoundwa specifically kwa ajili ya utawala wa chama kimoja!

William.

WJC:

Umeleta point moja nzuri sana. Hiyo ya ku-raise issue siku zote namlaumu Mrema kwa kukubali kujiingiza kwenye uchaguzi wa 1995 bila kusoma katiba. Simba na Yanga hawachezi mechi kama mmoja wao anapewa competitive advantage.

Anyway, wataalamu wanasema watu wenye oral traditions, mara nyingi wanatumia kauli za midomoni kuendesha shughuli zao. Mgombeaji wa uchaguzi akiona kwenye kampeni kakusanya watu wengi sana, basi anaamini kuwa atashinda.

Uchaguzi ukimalizika ndio anatambua kuwa wanaohesabu na kusimamia ni watu walioteuliwa na mpinzani wake. Lakini haya mambo yote yapo kwenye katiba.
 
Nchi yetu inaelekea pabaya kama mabadiliko ya lazima yasipo fanyika, watu wanaleta usanii katika kuongoza mambo muhimu ya nchi.
 
Mimi kama Mmarekani sioni sababu ya viongozi wa Tanzania kupigiwa mkwala. Uchaguzi umefuata katiba yenu. Ni katiba yenu inayosema kuwa rais ateue mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, na watu wengine wanaoweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi. Hivyo mtu aliyopo madarakani akishinda kwa kutumia madaraka aliyopewa kikatiba, hayo ni matatizo yenu.

Rubish...Nani kakuuliza wewe mmarekani? sema mimi ni mzamiaji ambae sina hata haki ya kupiga kura marekani....nonsense
 
Tutoe shinikizo kwa EU na USA kuwapiga mkwala wa kwenda ulaya na marekani viongozi wote wa CCM pamoja na familia zao kwa wizi wa kura. Haiwezekani watuibie kura halafu waende kujichana kwa pesa zetu.

CHADEMA huu ni wakati wa kuanza kampeni kwa mabalozi na nchi zote marafiki ili hawa wanoko wakione cha mtema kuni.
Hivi hujui wazungu ni wanafiki zaidi yetu? wakikumbuka wana migodi wamepewa bure ukiwashauri hivyo hawakusikilizi labda siku almasi na dhahabu zetu zikiisha watakuelewa
 
Wapigwe marufuku tuu waliwaonea wazenji enzi zile wakadhani bara tutakaa kimyaaaaaaaaa
No way
 
Tutoe shinikizo kwa EU na USA kuwapiga mkwala wa kwenda ulaya na marekani viongozi wote wa CCM pamoja na familia zao kwa wizi wa kura. Haiwezekani watuibie kura halafu waende kujichana kwa pesa zetu.

CHADEMA huu ni wakati wa kuanza kampeni kwa mabalozi na nchi zote marafiki ili hawa wanoko wakione cha mtema kuni.

Ndoto za alinacha!!! wakati anaapishwa rais wa znz Dr. mohd S.. walikuwepo!
 
WJC:

Umeleta point moja nzuri sana. Hiyo ya ku-raise issue siku zote namlaumu Mrema kwa kukubali kujiingiza kwenye uchaguzi wa 1995 bila kusoma katiba. Simba na Yanga hawachezi mechi kama mmoja wao anapewa competitive advantage.

Anyway, wataalamu wanasema watu wenye oral traditions, mara nyingi wanatumia kauli za midomoni kuendesha shughuli zao. Mgombeaji wa uchaguzi akiona kwenye kampeni kakusanya watu wengi sana, basi anaamini kuwa atashinda.

Uchaguzi ukimalizika ndio anatambua kuwa wanaohesabu na kusimamia ni watu walioteuliwa na mpinzani wake. Lakini haya mambo yote yapo kwenye katiba.

:doh: The spoken relation and preservation, from one generation to the next, of a people's cultural history and ancestry, often by a storyteller in narrative form.
 
Hebu acheni ujinga hapa,Ebo kwenda ulaya na Marekani mnaona ni issue ya kuandika humu ama kweli hii sasa inapoteza mwelekeo,mtu ukishuka hapo chini bondeni si unapata yote yanayopatikana huko mnakoita majuu? tena issue za visa kwishney!!!nimetembea sana hiyo ulaya kuanzia miaka ya 8o, sina sehemu ambayo unaijua wewe siijui,lakini kuanzia 1995 sijawa na matamanio ya kwenda huko na i dont miss anything wallah.
 
Back
Top Bottom