EU kutaka kesi ya Freeman Mbowe ifutwe hawajui kuwa Tanzania is a free State?

Ni vizuri hata umeuliza lakini sioni kama umesoma hata sentensi ya mwisho “civic space imepungua”.

Ukweli ni huu, unadhani ni CCM tu ndio wenye nia nzuri (mpaka sasa nchi hii ina maovu mengi na Chadema hakuwahi kutawala). Na sio Chadema wenye mabaya tu!! Lakini cha ajabu hapa ni kuwa wema unahusishwa na CCM na ubaya unahusishwa na Chadema. Watu wengi sio CCM wala Chadema!! Ndio maana nikuzuia usitumie “sisi” kwa sababu hiyo unatufanya sote kuwa CCM au unafanya wengine wote kuwa Chadema.

Civic space ya wale wasiokuwa CCM moja kwa moja inachukuliwa ni ya Chadema na hivo lazima ubinywe. Swala la Mbowe na EU ni swala moja, je Chadema kutaka kufanya mikutano ikazuiliwa kwa pretext ya “usalama” au “magonjwa ya kuambukiza” - ni sawa? Wakati huo huo CCM viongozi wa juu wakifanya ziara!! Wao madhila hayo hayawapati?? Najua utasema ni Polisi na sio CCM wanazuia wapinzani kufanya shughuli zao - mimi nasema CCM ni beneficiary wa matendo ya Polisi.
CCM akili yao wanaijua wenyewe.

Wakati Maza anaxunguka kushoot movie yake watu wakishangilia. Leo wamekazana na Ugaidi. Mikutano inazuiliwa kisa ugaidi... Hivi wanafikiri kuna watalii wanataka kwenda kwenye nchi yenye ugaidi...!!?
 
CHADEMA ni vibaraka siku zote, Hatushangai, Ila wananchi wameshawakacha
Haiizidi ccm kwani ni vibaraka watiifu wa wachina Hadi wanawazawadia gesi yetu na bandari ya bagamoyo Kwa utii na moyo mkunjufu! Una akili yenye makengeza wewe!
 
Kwa kifupi sana uzalendo ni kuipenda nchi yako.

Huwezi kusema unaipenda nchi yako uku unafumbia macho maovu yanayofanywa na kikundi cha watu wachache kinachoua,kutesa na kuonea raia wake,kilichojaa rushwa,dhulam nk

Tetea nchi yako kwa kutetea maslahi ya wengi na hasa ya taifa na sio kutetea kikundi cha waovu na kupata ugali wa siku,Mandela na Nyerere wanakumbukwa na wengi kwa ajili hii sio wachache.
CCM wakinyamaziwa watakuwa kama yule Dictator wa Equatorial Guinea.
 
Sio Tanzania tu nchi zote za Africa hazijawa huru! Usipumbazwe na uhuru wa makaratasi.

Angalia bajeti ya Tanzania ni kiasi gani kinachangiwa na hao mnaoita mabeberu ndio utajua lazima kuna vitu viwe complied ndoa iendelee kuwepo.
Unazungumzia uhuru gani?
 
Lazima tulinde sheria tulizojiwekea,
Ambazo siyo lazima kuzingatia kwani zinaichelewesha nchi kusonga mbele! Hizo sheria ni zile zilizotokana na katiba mnayoivunja Kila uchao au Kuna nyingine mmecopy kutoka Burundi ma Uganda?
Kwa taarifa Yako ni kwamba nchi hii ilishaachana na matumizi ya sheria na katiba badala yake inaongozwa Kwa ilani na matamko ya walio juu!
 
Acha mambo mengi tuchape kazi
 
Lete mfano

Bajeti ya dawa ni 200b+, nenda kachukue taarifa ni kiasi kimefika. Kisha uwahi kurudi tuendelee na mjadala. Kilimo bajeti yake ni chini ya 100b, nenda ukachukue taarifa za kiasi kilichopelekwa na serikali.Usiokoteze taarifa mtaani, bali chukua taarifa kwenye ripoti ya CAG ya bajeti iliyopita. Hapo ndio utajua zama za kudanganya watu zilishapita.

NB: Halafu mjulishe Makamba ule utapeli wake kuwa alionana na viongozi wa Tunisia sijui Algeria kuhusu kununua mafuta direct toka kwa mchimbaji, umeishia wapi maana mafuta yanazidi kupanda bei. Au ndio alienda kutuwekea cha juu? Kisha mkumbushe PM ule uongo wake kuwa SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi Nov 2021 tumeustukia tunamchora tu. Umesikia au niongeze sauti?
 
Kama CHADEMA tangu iasisiwe miaka 32 imeongozwa na ndugu wawili tu,

Edwin Mtei
Freeman Mbowe

Unataka Udicteta gani?
Wewe mtoto wa juzi nini. Walau muwe mnagoogle kabla ya kuandika uongo. Mambo ya chama kiachie chama.

Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa chama kwa zaidi ya miaka 30.
 
Kwa Tanzania kuwa nchi ya pili kwa uhuru wa maoni Afrika sio hoja maana unaweza kutoa maoni ya ngono tu na mambo mengine ya kawaida sio uhuru wa kuikosoa serikali.

Kuongoza ktk darasa la wajinga hakukuondolei ujinga
Ukiikosoa kuna watu wasio zidi sita ambao ni kikosi cha wasio julikana wana zunguka Tanzania nzima na ma vx ya walipa kodi kuteka watu na kuwaficha kwenye mahabusu zao bila kuulizwa na mtu. Na kuwafungulia kesi wanayo taka wao. Au kukupoteza. Ati Tanzania tuna IGP!!! Ujinga mtupu. Mahakama nazo zinapokea mashtaka ya kipuuzi. Shame!!! Shame Tanzania!!!!
 
Hao wasiojulikana mwisho wao umefika,hakuna maovu yanayodumu na malipo yao uwa lazima tuyashuhudie kabla ya mauti
 
Hivi mbowe ni malaika mpaka asiweze tenda kosa? Hii tabia ya chadema kujiona wao ni wasafi ila wengne wachafu ni tabia ya hovyo sana ..

mimi binafsi sifufahishwi na uongozi wa samia kwasababu zangu binafsi kiufup simkubali kabisa.

Ila kuhusu mbowe lazima sheria zifuatwe, haiwezekani wengine wahukumiwe alafu yeye et kisa mtu maarufu sijui mwenyekiti wa chadema ndo kesi ifutwe!!! Hili halikubaliki na lazima tuwaambie ukweli nyie mnaoendekeza ushabiki kwa mwenyekiti wenu ..

Sasa tunawaambia waambie hao mabeberu tanzania ni taifa huru linajiendesha kwa misingi yake iliyojiwekea, taifa hili haliwezi kupangiwa na mpuuzi yeyote na hili lazima mabeberu na vibaraka wenu mlitambue.. tunataka haki itendekeze na sio upuuzi wa kushinikiza kuondoa kesi mahakaman
 
Tanzania ni nchi huru tena Uhuru wake ni wa miaka sitini (60) sasa

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine za EU inayo sheria,kanuni na taratibu za kuongoza watu wake ili waishi na kujiletea maendeleo yao kwa amani na Utulivu

Freeman Mbowe na wenzake wanatuhumiwa kutenda kosa la Ugaidi na kesi inaendelea Mahakamani tena mfululizo hili dunia inajua

Utawala wa Sheria duniani kote ikiwemo EU unatamka kuwa "Hakuna aliyejuu ya Sheria " No one is above the law,

Je! Can't it be applied to Mr Freeman Aikaeli Mbowe?

CHADEMA mnataka kusema Freeman Mbowe kwa kuwa ni Mkt wa Chama chenu hawezi kutenda kosa?

CHADEMA na EU mnataka kusema Freeman Mbowe ni malaika wa nuru asiyeshawishika wala kutenda kosa?

Tunafahamu bifu kubwa lilokuwepo baina ya aliyekuwa Mbunge wa Hai Freeman Mbowe na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya

Miamba hii miwili ya kisiasa ilikuwa ikipimana nguvu pale Wilaya ya Hai kwa njia halali na zisizo halali,Hili wote tunalijua na CHADEMA mnalijua zaidi

Tukubaliane kuwa njia alizotumia Freeman Mbowe kutaka kumdhibiti Lengai Ole Sabaya ziliwafanya Mbowe na Sabaya kuvunja Sheria za nchi na wanaoweza ku-approve au ku-disapprove hili ni mahakama pekee kama chombo cha juu kabisa cha kutoa haki na wala sio Rais Samia

Kitendo Cha CHADEMA kuanza kuisiliba nchi yao kimataifa licha ya Juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan katika kuirejesha nchi kidiplomasia halikubaliki na halitakubalika kamwe

Tujiulize, CHADEMA wanaogopa nini kama kweli Freeman Mbowe hana hatia Mbele ya Sheria?

Sote tunafahamu, CHADEMA ndio Chama chenye Mawakili wengi na nguli wa Sheria hapa Tanzania

Je? wamekwama wapi au nawao wamebaini ni kweli mteja wao anamakosa wanaamua kuigeuzia kesi hii Kisiasa kisa Freeman Mbowe ni mwanasiasa?

Kwanini leo wakimbilie kulichafua Taifa Kimataifa hata kabla ya hukumu yenyewe? Nini kimewasibu kwenye jicho la Sheria?

CHADEMA acheni kulichafua Taifa letu Kimataifa,mlisingizia Magufuli Leo tena Samia lazima mtambue Sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya hii

Mnatuumiza sana sisi watu wa chini

Sisi hatuna uwezo wa kuishi huko Ughaibuni Ubelgiji,Canada wala Scotland kama ninyi na familia zenu

Mnanenepa na kung'aa kuwazidi hata Wazungu kwa gharama za nchi yenu hakika hii ni mbaya sana brothers

Hiyo misaada mnayotaka tunyimwe na EU ndio inawafanya watoto wa Shangazi zenu wajengewe madarasa elfu 15 na Rais Samia Suluhu

Plze Brothers & Sisters STOP IT

WAAMBIENI "EU" TUTASIMAMIA SHERIA ZETU KWA GHARAMA YEYOTE,TAIFA HILI NI KUBWA KULIKO MISAADA YA EU,.

Pia, soma=> Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

View attachment 2030228

View attachment 2030229

EU yajibu kuwa inaridhika na mwelekeo wa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kisiasa na kiuchumi na itaendelea kutoa misaada Tanzania
 
Attachments

  • VID.mp4
    15.5 MB
Hivi mbowe ni malaika mpaka asiweze tenda kosa? Hii tabia ya chadema kujiona wao ni wasafi ila wengne wachafu ni tabia ya hovyo sana ..

mimi binafsi sifufahishwi na uongozi wa samia kwasababu zangu binafsi kiufup simkubali kabisa.

Ila kuhusu mbowe lazima sheria zifuatwe, haiwezekani wengine wahukumiwe alafu yeye et kisa mtu maarufu sijui mwenyekiti wa chadema ndo kesi ifutwe!!! Hili halikubaliki na lazima tuwaambie ukweli nyie mnaoendekeza ushabiki kwa mwenyekiti wenu ..

Sasa tunawaambia waambie hao mabeberu tanzania ni taifa huru linajiendesha kwa misingi yake iliyojiwekea, taifa hili haliwezi kupangiwa na mpuuzi yeyote na hili lazima mabeberu na vibaraka wenu mlitambue.. tunataka haki itendekeze na sio upuuzi wa kushinikiza kuondoa kesi mahakaman
Maskini Hana Uhuru, mbowe ashitakiwe kwa makosa alotenda na si kwa makosa alosingiziwa.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom