Elections 2010 EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,657
3,035
Wednesday, 03 November 2010
Elias Msuya

MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

"Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

"Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema Martins.

Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

"Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.

Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

"Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.

Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema Ndelcheva.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Sure, tume sio huru, hilo ni jambo la kusikitisha sana ambalo JK wetu na viongozi waliopita wamelifumbia macho!

Akina Tundu Lissu wapeleke muswada binafsi Bungeni ili kurekebisha Katiba kuifanya NEC kuwa huru!
 
Wanayoyasema jumuia ya ulaya ni kweli, pia lipo moja ambalo lilijitokeza wazi nalo nikutofautisha msafara wa rais na msafara wa mgombea ccm, nathan kimantik lazima mbeleni hili liangaliwe sababu kwa jinsi msafara wao ulivyokua huwez tofautisha na mtu ambae ameshatangazwa kuwa rais tofauti na wagombea wa vyama ambavyo havijashika dola.Nimejiuliza tatizo nikatiba au ni nini? Je wapinzani hawalioni hili?
 
Wanayoyasema jumuia ya ulaya ni kweli, pia lipo moja ambalo lilijitokeza wazi nalo nikutofautisha msafara wa rais na msafara wa mgombea ccm, nathan kimantik lazima mbeleni hili liangaliwe sababu kwa jinsi msafara wao ulivyokua huwez tofautisha na mtu ambae ameshatangazwa kuwa rais tofauti na wagombea wa vyama ambavyo havijashika dola.Nimejiuliza tatizo nikatiba au ni nini? Je wapinzani hawalioni hili?
 
MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.

“Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri,” alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.

“Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza” alisema Martins.

Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.

“Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,”alisema.
Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

“Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi,” alisema.

Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

“Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais,” alisema Ndelcheva.
 
"Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.

Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.

Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.

Katika mambo JK yatamuuma ni uraisi wake kubezwa na waangalizi wa jumuiya za ulaya.................Hawa ndiyo anawategemea kwa misaada sasa hapa ni mushkeli mkubwa..............wahisani hawa kamwe hawatakuwa tayari kuibeba CCM wakati siyo chaguo la wengi...........
 
Tumeisha wazoea nyie wazungu, ili uchaguzi mseme ulikuwa huru na wa haki ni lazima chama tawala kishindwe.
 
Hawa jama wapeleke ujumbe EU watunyime misaada CCM watatia akili bse nimegundua kaisema mzungu ndo wanaelewa
 
hawana jipya!! washazoea watu washike mitutu ya bunduki .. waje wachukue rasilimali zetu kiulaini... " tushasikia maoni yenu.. tatizo wa tanzania WALIO WENGI WAMEONGEA .. ondokeeenii .. :doh:
 
Katika mambo JK yatamuuma ni uraisi wake kubezwa na waangalizi wa jumuiya za ulaya.................Hawa ndiyo anawategemea kwa misaada sasa hapa ni mushkeli mkubwa..............wahisani hawa kamwe hawatakuwa tayari kuibeba CCM wakati siyo chaguo la wengi...........

Obama nae sasa atafahamu kuwa Good Governance imefikiwa Tanzania!
 
Back
Top Bottom