ETI Zanzibar Uhuru 12/10/63 uliibiwa Jan 64 na Makucha ya Dodoma

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Kwanini Wazanzibari wanachukia Tanganyika? na bado tunaikumbatia hiyo nchi?
December 10 1963 Ni Uhuru Wa Nchi Lakini Hausherekewi...

Soma Jarida Hapo Chini

Disemba Kumi, Siku Adhimu Kwa Wazanzibari

Kwa Rehma za Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Ta’aala, saa kama hii, siku kama hii, Disemba Kumi, 1963 Zanzibar ilipata Uhuru wake baada ya utawala wa Muingereza wa miaka sabiini na tano. Muhimu la kukumbuka hapa ni kwamba muda wote huu wa utawala wa Muingereza juu ya Zanzibar, iliendelea kuwa “Zanzibar ni Nchi”, yenye kila lake la kidola kaamili; haikufika kufanywa kuwa“Zanzibar si Nchi”,kama ilivyofanywa na mvamizi mkoloni Tanganyika kwa mbinu za huu wenyekuitwa muungano. Taadhima ya siku hii adhimu, ilifunguliwa pia na khutuba ya historia ya kiongozi wa Afro-Shirazi Party (ASP), Mzee Abeid Aman Karume kwa kusema:
“Leo mwezi 10 Disemba, 1963, ZANZIBAR imekuwa Huru. Hii leo sisi watu wa visiwa hivi tumepata haki ya kuchukuwa mahala petu kuwa ni Dola sawa na nyengine katika umoja wa Nchi za Dola zaCommonwealth. Kwa uchache, kuwa mwanachama katika umoja huo, kuna maana kwamba nchi hii ni huru chini ya mpango wa serekali ambayo msingi wake umejengwa juu ya kuendeleya kwa ridhaa ya wananchi.

Ili kufikiliya matarajiyo yetu hayo tunayo moja katika Katiba zenye msingi madhubuti iliyohusika na shuruti za haki za binadamu, haki za mambo ya siyasa na uhuru wa dola yoyote nyengine. Ni wajibu wa watu wote wa dola yetu mpya, kila mmoja katika sisi bila ya kujali fikra zetu za siyasa au madaraka yetu kusaidiya kweli kweli Katiba yetu iweze kufanya kazi. Pamoja na manufaa, haki na uhuru ambayo yote hayo yamepatikana baada ya nchi kuwa huru.
Tuliyoyapata leo mwezi 10 Disemba, 1963 ni mipango ya mwanzo tu ya kuweza kufanya juhudi kwa ukamilifu dhidi ya maadui zetu, nao ni ujinga, umasikini na maradhi na kuweza kuleta imani penye khofu na shaka na kuleta masikilizano mahala ambapo hata hivi sasa adawa ipo,
na kuleta mapenzi mahala ambapo pana chuki, ili dola yetu mpya ichomoze katika neema, umoja na furaha.

Zanzibar Inajiunga Na Umoja Wa Mataifa

Baada ya kupata Uhuru wake Zanzibar, taarikh 14 Disemba, 1963 ilijiunga na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (UNO) ikiwa ni mwanachama kamili wa Jumuiya hiyo ya kilimwengu. Kwa munasaba huu nina inukulu hapa (tena) khutuba ya Waziri Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Muhammad Shamte katika Umoja wa Mataifa (UNO) taarikh 16 Desemba, 1964 ikikaribishwa Zanzibar kuwa ni mwanachama wa Jumuiya hii muhimu ya kilimwengu.

Kumezwa Dola ya Zanzibar

Uhuru na dola hii ya Zanzibar mpya ulidumu siku thalathini na tatu tu, yaani tangu Disemba kumi, 1963 mpaka Januari kumi na moja, 1964 kwa kuvamiwa na mvamizi mkoloni Tanganyika. Sote tunafahamu ya kwamba mara baada ya mavamizi ya Januari 1964, mwaka huo huo; mwezi wa Aprili, Zanzibar ilitiwa chini ya makucha ya Dodoma kwa kisingizio cha wenyekuitwa “muungano”.Kutokana na “Articles of Union, 1964”, Zanzibar ilipoteza Dola yake na kuwa ni koloni la Tanganyika. Mengi yamesemwa juu ya suala hili la huu wenyekuitwa muungano. Ya hivi karibuni yaliosemwa ni haya walioyasema wao wenyewe, wavamizi wakoloni Tanganyika, katika kitabu chake; “The Political Plight of Zanzibar”, Profesa Maliyamkono katika ukurasa wa 198 – 199 ametueleza haya:
 
Back
Top Bottom