Eti wewe unazingatia nini? nyumba, gari, kipato, mapenzi.........???

ha bari za wikiend JF!
Jamani mimi mwanzoni nilidhani/nilichukulia kua uchumi ndio kigezo kikubwa cha
kuahakikisha nimefaulu kabla ya kuoa. Yaani, angalau hata kama sio kujenga au
kua na mahela mengi lakini angalau niwe na convinient source ya income.
Pamoja na kigezo hiki kubakia na uzito mkubwa lakini kwa sasa nimekiweka cha pili.
cha kwanza kwa sasa ni kuwa au kumpata mtu wa kumwoa.
sikuwah kufikiri kua hii ni bahati, au baraka na si kila mmoja anae/ataepata.

Hivi kwa wewe mJF kigezo kikubwa unachozingatia kabla ya kuoa ni kipi??

Mi kabla ya kuoa nazingatia mapenzi kwanza nisije oa garasa bure
 
Tungekuwa pamoja ungesema ninakuiga! Mimi nimejaribu kusoma soma vitabu na kugundua umuhimu wa hili suala naomba nisharee nawewe ifuatavyo:-

1. Maisha ya ndoa pia huandaliwa kama unavyoandaa hayo mapesa, magari na majumba. Ukisema ukija kupata hayo ndiyo uoe kuoa siyo kuoa tu kama unavyodhani kwa ulimwengu wa sasa ni kazi tete sana hasa kupata wa moyo wako! so unahitaji kuliandaa hili pia kwa wakati huhuu ambao unajipanga na kipato.

2. Ukiangalia katika maandiko ya Mungu kuna mstari unasema hivi: APATAE MKE APATA KITU KILICHO CHEMA, TENA ANAKUBALIKA NA BWANA (MUNGU) Unaweza ukafanya vitu vingi sana peke yako na visiende kabisa, ila ukija kuoa tu tayari mambo yanawiva kila kitu kinaenda sawa bin sawie!

3. Ni nzuri kuja kuyatafuta wote hayo mafanikio unayoyatafuta wewe, kwani mkiyatafuta wote lazima mtayatunza wote, ukiyatafuta peke yako mwenzio akija atatumia vibaya jambo ambalo litaleta ugomvi kwenye ndoa.

4. Ndugu yangu mke ni muhimu sana ukioa wa kwako i mean mnayeshabihiana kwa kila hali. Mimi mwenyewe nalia mno sasa hivi, nahaha kutafuta mwenza lakini sipati kabisa wa kufanana naye. yaani unalia unakuwa kama chizi. Halafu kumbuka ukioa utatulia hata kiakili, watu watakuheshimu zaidi, credibility itaongezeka, tamaa na miwasho itabadilika na kama ni mtu wa Mungu basi njia ya mfanikio kwako ni huyo mke!

Oa kaka na mimi natafuta mke nikimpata tu hata leo naoa soon!

kaka unadhani mkua jitihada yoyote unayoweza kufanya ili kupata huyo mke wako (wakufanana nae)
me naona kama hhakuna jitihada za kibinadam zinazowezekana labda za kiroho na hii ji kwa wale waaminitu.
sasa kwa wasio waamini sijui inakuaje!
katika hili nakusihi usinitie majaribuni ee mwenyezi Mungu.Amen.
 
At least niwe na source nzuri ya income!!

katavi unjua kua unaweza kua na sos nzuri ya kipato na bado usione mtu wa kumwoa??
na hili ndilo linalowatokea wengi. huoni mtu moyo wako ukampenda na kuridhika nae kwa dhati.
na me nafikiri we tyari ushakua kiasi cha kuweza kuona ni jinsi gani ilivyom hatari kuingia katika ndoa bila
kua na uhakika na unalolifanya.
 
Kijana aangalie mapenzi hela na nyumba ni matokeo tu ya huko mbeleni unaweza kuwa nazo au usiwe nazo

Hahaha!! Mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani
kwa hiyo unakubaliana na mimi.
na uli/utafanya hivy katika kuoa!! right?
 
katavi unjua kua unaweza kua na sos nzuri ya kipato na bado usione mtu wa kumwoa??
na hili ndilo linalowatokea wengi. huoni mtu moyo wako ukampenda na kuridhika nae kwa dhati.
na me nafikiri we tyari ushakua kiasi cha kuweza kuona ni jinsi gani ilivyom hatari kuingia katika ndoa bila
kua na uhakika na unalolifanya.
Naweza nikawa na mpenzi tayari lakini siwezi kuingia katika ndoa kama sina uhakika na kipato cha kuniwezesha kubadili mlo...
 
kwa hiyo unakubaliana na mimi.
na uli/utafanya hivy katika kuoa!! right?
Yah!! Lakini itabidi uhakikishe una kipato cha kujitosheleza cha kuwakidhi nyie wawili sio unamuoa mtoto wa watu unaenda kumlaza njaa
 
You have to make sure your in love with the one you want to marry, mengine yataflow yenyewe
 
Binafsi.. vyote, mke na utafutaji vyaenda sanjari.. Ila nachorea mstari yafuatayo:
- Kuoa/kuolewa ni utayari kamillifu wa mwili.. akili.. uchumi na kiroho... kikipungua kimojawapo lazima mwanaume utapata tabu tu(ya kimwili au kiakili..).

-Ni rahisi kubadili mwonekano ma mlima kilimanjaro kuliko kubadili tabia ya mtu. mabadiliko ya tabia ya mtu huanza na mtu mwenyewe. Hivyo mwezi wa maisha(awe changudoa au bikira) inabidi azingatiae namba 1 hapo juu na awe na utayari wa kuwa na tabia anayopaswa kuwa nayo kama mwandoa.

- Hakuna mwanaume..asilani... ambaye anaoa halafu hana uhakika na "KESHO". Mwanaume hapendwi, ANAHESHIMIWA (kama uongo nisahihishe). Moja ya heshima yake ni kuwa na uwezo kwa kujenga nafasi yake(kama mume) na mkewe katika jamii inayomzunguka (hapa unaongelea vyanzo imara vya mapato.. makazi na mengineyo.) na katika hili ndipo juhudi ya mtu na viwango mbalimbali vya mafanikio vinaonekana hapa( maisha bora na bora maisha).

Nakubali kusahihishwa... Ni hayo tu kwa sasa..
MMU
 
Ahahahaaaah!! Sio pesa nyingi kama za mapedeshee, mimi nikiwa na kiasi kidogo tu cha kuniwezesha kubadili mboga....

Angalia usimzoeshe nyama,kuku,bata we mzoeshe tembele, kisamvu, mchicha na maharagwe kwa wingi
 
Yanini kujipa tabu na raha zipo telee!

Utaona atakupa tabu achana nae tafuta Wa size yako
 
Yah!! Lakini itabidi uhakikishe una kipato cha kujitosheleza cha kuwakidhi nyie wawili sio unamuoa mtoto wa watu unaenda kumlaza njaa

kaka we upo na m9imikabisa, ndo sababu nikasema kigezo cha pili niuchumi ila cha kwanza n mapenzi
 
Back
Top Bottom