Eti.....wawekezaji wengi huja kuchuma na kuondoka!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti.....wawekezaji wengi huja kuchuma na kuondoka!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kuti kavu, Apr 16, 2010.

 1. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Baada ya kuchomwa na jua mpaka jasho kukauka katika harakati zangu za kujenga taifa letu 'changa' pia ikiwa kama niia ya kupata mkate wa kila siku,hatimae nabahatika kupata msamaria mwema anaekubali kuniazima walau ukurasa wa gazeti la leo la Nipashe,ni kaukurasa ka 5, nakapembua na kukutana na kichwa cha habari kimoja kisemacho "waekezaji wengi huja kuchuma na kuondoka".

  Katika kupitia nakuja ona ni kauli iliyotolewa na mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha cha Dar es salaam Dk. Haji Semboja wakatiwa kongamano la biashara kati ya China na Bara la Afrika. Semboja anendelea kulalamika kuwa wawekezeji hao wanakuja Tanzania wakiwa na lengo moja tu la kuchuma na sio kuendeleza Nchi yetu.

  Kauli ya Semboja imenipa maswali mengi ambayo labda wana JF wenzangu mnaweza kunisaidia kuyajibu...

  Hivi lengo kuu la mwekezaji yeyote ni lip zaidi ya ukupata faida???.....

  Kati ya mwekezaji na yule anaemkaribisha huyo mwekezaji ni nani mwenye jukumu la kuhakikisha mikataba ya ki-uwekezaji haitamnufaisha mwekezaji bali iwanuafaishe na wale wenye rasilimali zilizomvutia mwekezaji huyo???....

  Ni Nchi gani hapa duniani ambayo ilipokea wawekezaji waliokuja nchini humo kwa lengo la kuto kujinufaisha ila kuleta maendeleo ya nchi hiyo husika???....

  Na je si jukumu la wasomi wa fani ya uchumi kama Dk Semboka kutusaidia sisi wanyonge kutengeneza mazingira ambayo hatamnufaisha muwekezaji ila na sisi pia ambao tunanyonywa na wawekezaji hao???...

  Nionavyo mimi kauli hii ya Dr Semboja ni sawa na baba mwenye nyumba kuwaambia watoto wake wadogo kuwa lengo la njaa siku zote ni kuua,ilhali ni jukumu lake kuleta chakula nyumbani!!!!
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wasomi wengi wa Tanzania hawaelewi jinsi ya kutumia elimu waliyopata kusaidia nchi na wametawaliwa na mawazo ya kikoloni. hebu tuangalie Mkapa alivyoshupalia kuuza NBC Bank wakati ule!!..... alikuwa hataki hata kusikilza ushauri kwa sababu ile benki ilikuwa inapata faida lakini badala ya kuiboresha wao wakauza sasa leo utamlaumu vipi mwekezaji wakati ni wewe mwenyewe umemuuzia kwa bei ya kifisadi???

  Tatizo kubwa la uwekezaji wa Tanzania ni kuingiza siasa ktk masuala muhimu ya uchumi pamoja na rushwa kubwa kwenye mikataba.
   
Loading...