Eti wanaume sio wenzetu??na je wanawake si wenzenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti wanaume sio wenzetu??na je wanawake si wenzenu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by FirstLady1, Apr 26, 2011.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Jeez mwenzenu katika hali ya mshangao nikiwa gereji nasubiri bajaji yangu ifanyiwe marekebisho madogo madogo
  Kulikuwa na kina baba pia kina mama na ndoa zao,pia kulikuwa na vijana ambao wako ktk mahusiano g/F na b/F ilianzishwa topic ya ndoa na mahusiano kwa ujumla ,kila mmoja akitoa lawama upande wa mwenzie kama wanawake siku hizi hawashikiki na hawaheshimu ndoa zao,wanawake nao wakatoa lawama nyingi kwa wanaume kuwa wamekuwa wanyama na wanafanya maamuzi ya kikatili sana pasipo kuwa na hekima ,
  Ndipo baba mmoja anayeonekana wa makamo kidogo akatoa neno lililowaacha watu midomo wazi ,huku likiungwa mkono na wanaume wengine .Eti na nyie wanawake mkoje mnawaamini hao wanaume kwani ndugu zenu ,mmezaliwa nao tumbo moja ?Tumieni akili zenu za ziada sio kulia ooh nimeachwa bila kitu tumejenga nyumba pamoja ,tumefungua miradi pamoja siku hizi akili kichwani sio kulia lia ovyo..kwani nyie kulwa na dotto ??

  "tukamuuliza kwa hiyo unataka tufanyeje ?
  tukajibiwa na wanaume aaah akili zenu sasa sio kila kitu mtafuniwe

  wapenzi hebu tudadavue swala hili kwa ujumla ..haijalishi umewowa ama umeolewa mradi tu wote tunatarajia kuingia huko maana kila mmoja anavutia upande wake

  JAMANI KWA HALI HII TUTAFIKA?VIZAZI VYETU TUTAVIFUNDISHA NINI JUU YA NDOA NA MAHUSIANO KWA UJUMLA
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ndoa za cku hizi ni za kuoteana sana, atakaemuotea mwenzie twende, kuaminiana/kushirikianao kwa uaminifu kumepotea kabisa, ndoa za cku hizi unatakiwa uwe na akili za ziada kabisa.
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180  Nakubaliana na huyo baba na kurudi kule kule kua Men are from Mars and women from Venus....
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ha ha haa!

  Haya maongezi kwa asilimia 90 yanaonekana yalikuwa ni ya watu wasio na huruma au kumjua Mungu!
  Japo mi ni mwanaume siwezi kuyashusha thamani mahusiano yangu na mke wangu kwa kiasi hicho!
  Watu mnapoingia katika mahusiano ya ndoa maana yake ni kuanzisha familia mpya na umoja mpya ambao baadhi tunaamini hautavunjwa na hali yoyote, isipokuwa kifo!
  Sasa kama mwanamke anaambiwa atumie akili zake, kwangu mimi natafsiri kwamba atumie akili kuhakikisha kuwa analinda nyumba yake na kuifanya isisambaratike daima kwa kuongeza upendo hata katika hali inayokatisha tamaa!
  Pia maana ya mwanaume si ubabe na ukatili ndani ya mahusiano...ni akili na kuipenda familia yako!
   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  kaa kwa akili...usiolewe ukabweteka kuwa umefika...kuwa tayari kwa maamuzi magumu wakati wowote....huolewi na malaika bali mwanadamu mliyekutana kila mtu akiwa na maisha yake na ambaye hata mkiachana maisha lazima yaendelee.....
   
 6. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi nakubaliana na huyo baba kwa asilimia mia ni wachache sana wenye hofu ya mungu kwa dunia ya leo ,kila mtu amegeuka mmnyama ,pia nadhani nguvu za giza zimeingia kwa kasi sana kwenye mahusiano ,mungu atuhurumie sana ,mwenyewe ni muathirika wa sakata hili,hivyo sishangai sana
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  cku hizi mambo mengi kwenye ndoa yamebadilika kutokana na ndoa zenyewe za cku hizi zilivyo, mambo yamekuwa vululu vululu sana...kwa kweli mie najihami na nitaendelea kujihami hata nicpoona kasoro.
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Thanx. Umenisemea maneno yangu.
   
 9. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  watu hawataki kuwa wavumilivu...mwanamke tu kajifungua,mtu anachukua house girl.....mama ana mapungufu,badala mtu amsaidie kubadilika,amvumilie,ashirikishe wazee na kumuombea....anaona house girl hapo ana lala nae....watu wana simplify maisha kupita kiasi...kwa mtindo huo yabidi kukaa kwa akili,kama elimu huna na kuna nafasi ya kusoma,kufungua biashara fanya hivyo.....nyumba kama unaweza jenga kwa akili.....kikinuka,ondoka si mpaka uje uwekewe sumu na mke mwenzio house girl hapo ndani ukijidai kutaka heshima na mwanamke uvumilivu.....au unasemaje Nyamayao?
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1,

  Huyo babu kichwani pametulia. Hayo maneno yake ni mazito sana. Labda alichokosea ni kuwataka wanawake tu watumie akili zao. Mimi naamini wote tunatakiwa kutumia akili sana katika ndoa za siku hizi...Hakuna tena mambo ya kutafuniwa. Hata hivyo ni muhimu kuchanganya akili, busara na hekima. Ukivipata hivyo hata kwa level ya C ya kuchechemea (just above 50%) basi ndoa itandunda kama haina akili!


  Hapo (red) ulimaanisha nini? Au una utani na majirani zako?

  Mzee DC
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu naomba kutofautiana na wewe. Mimi naona Great thinking kwenye hayo maongezi!!

  Mzee DC.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280

  Nyamayao naona siku hadi siku mambo yanaenda yakibadilika sana,heshima imepotea katika ndoa ni kweli akili ya ziada inahitajika sana na nguvu za mungu zituongoze
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  PJ wewe ni mmoja kati ya wale wachache wenye akili kama yako,kuna mmoja nafanya nae kazi ana tabia ya kurudi home asubuhi kuoga na kubadilisha nguo ,akiulizwa anasema mke mke nini kwani hali akashiba ,havai,watoto hawaendi shule ...ndio matatizo kama hayo
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hahaha Asha D kwa nini unakubaliana na huyo baba? mie sikutegemea maneno mazito kama hayo toka kwake ,kwanza yuko very aged na kidoleni alikuwa na pete yake ya ndoa ikionyesha kabisa ni baba wa family amekata tamaa mpaka kusema hayo?
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1,

  Ni kweli mambo yanabadilika ila watu wanataka kubaki kama walivyo na kutegemea kuwa kila kitu kitakuwa poa. Huo ni upuuzi na ni mtazamo potofu. Kama mambo yanabadilika basi na sisi inatubidi tubadilike.

  Zamani ndoa zililindwa sana na mila zetu...Kuachika lilikuwa neno gumu sana kulisikia. Ila sasa hivi kuachana ni kitu cha kawaida sana kama kwenda dukani kufanya shopping. Kwa nini tusijiandae kwa vitu kama hivyo?

  Mimi binafsi naamini my wife ni independent body (kama sovereign state vile) na sisi siyo cojoined twins. Kwa hiyo kama mambo hayaendi sawa lazima tutumie akili zetu na busara kujaribu kuyaweka sawa. Ikishindikina tunaanza maisha mapya without each other. Naamini hatujakosea kuwa katika alert 24/7!

  Mzee DC
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1,

  Binafsi sioni ubaya wa hayo maneno na naamini hayana chembe ya usanii. Ila ukiyachukulia juu juu itakuwa ngumu kumuelewa.

  Hata mimi nakubaliana naye kwa zaidi ya 50%. Ningempa 100% kama angeangalia pande zote 2 za shilingi!
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hahaha thanx DC hapo kwenye red nilimaanisha hata wale ambao hawajaoa watoe michango yao kwani iko siku wataingia huko
   
 18. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Dunia tambala bovu kila pahala pamechanika,anzia nyumbani hadi ofisini loh Mungu okoa hii dunia yako!!
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Michelle nakubaliana na wewe kabisa inabidi kuwa tayari kwa kila jamboa ingawa mungu hapendi watu kuachana ,
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Siamini pia kama watu wanapenda kuachana. Ila maji yakizidi unga wafanye nini dada?
   
Loading...