Eti Wanataka Tumpongeze Rais John Pombe Magufuli... Sasa Tumpongeze kwa Lipi Hapa?!

Dah! Halafu hii mada unajua nimeidandia tu manake siku kadhaa hata hapa nyumbani JF sijatokea na kufahamu what’s really going on!!!

Eti nimesikia mzigo huu wa Mheshimiwa Paul Makonda ni msaada kutoka kwa Diaspora wa Tanzania waishio Marekani… ni kweli, au?! Bro wangu anadai wao Diaspora wa US wanavyopenda sifa, lazima wangepiga mapicha na mzigo kabla ya kuupakiza kwenye meli!!! Sasa anahoji, je nyie wenzangu ambao mmefuatilia hili sakata tangu kitambo, mmeshawahi kuona hayo mapicha picha?!
Bwana weee! Pengine hii makitu ina tentacles kibao! Leo nimesikia kuna sugar inatolewa au itagawanywa bure, yani buuure! Halafu nasikia mnada wa makitu ya RC Dar unadoda, mwisho labda huo mzigo nao utagawanywa buuuree! Kwahiyo shhhhh! 'Tulia' kama una shule mwnng.
 
Watetetzi wa JPM wanapotaka eti Rais apongezwe!!
Kwenye hili la Makonda, kiukweli JPM anastahili pongezi kwa kitendo tuu cha yeye kama rais wa nchi, kujitokeza hadharani na kumbembeleza Makonda akalipe kodi kama wengine!. Hili tuu peke yake ni kubwa na la kustahili pongezi.

Na ikithibitika ni kweli makontena yana sofa, na zilikuwa zipelekwe shopping malls, atakachofanya rais, ni kumbeleleza Makonda arisign kwa hiyari yake, na hapa pia sio tuu JPM atapongezwa, bali pongezi zaidi zitamiminika kwa Makonda.

Kumpongeza JPM ni kuonyeshea tuu kuwa sisi tuu watu wa shukrani, yaani appreciation, hata nyumbani, msichana wa kazi kaajiriwa kumsaidia mama kupika, kupika ni kazi yake, analipwa mshahara, lakini ukila ukashiba, unatoa pongezi chakula kitamu, kisha unamshukuru.

Hata ndani, kama umeoa na kulipia mahari, hiyo mahari ni kulipia huduma, ukihudumiwa vizuri, unapongeza na asante unatoa, wakati kila kitu umegharimia wewe.

Kwa jinsi Makonda alivyo, anayoyasema, anayoyatenda na anavyo behave, kitendo tuu cha JPM kumsema hadharani, kinastahili pongezi!.

P.
Rejea
Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!. - JamiiForums
 
Kama ndivyo basi nakubaliana na wewe kwa 100%! Na labda niseme jambo moja... kwa silika yangu mimi si miongoni mwa washindwao kupongeza pale panapostahili kupongeza! Ni kutokana na silika yangu hiyo ndiyo maana tangia mwanzo wa mjadala huu nilishaamua kupongeza pale anapostahili kupongeza!!

Hapo juu nimesema sioni la kumpongeza Mheshimiwa Rais John P. Magufuli! Lakini Wahenga si walisema “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni”?!!

Hapa natoa haki! Angalau kwa hili nakupongeza Mheshimiwa Rais! Nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukiri hadharani kwamba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda ni FRAUD!

Nampongeza Mheshimiwa Rais wa JMT kwa kuthibitisha hadharani kwamba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda alikusudia au bado anakusudia kukwepa kulipa kodi!!

Ikiwa hadi sasa bado Makonda yupo madarakani, basi sina budi kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kufanya kazi na Mkwepa Kodi manake hatimae hivi anajidhihirisha wazi yeye ni mtu wa aina gani! Hapa Mheshimiwa Magufuli anadhihirisha moyo wa upendo alionao kwa watu wa aina yote hata wale waliodhihirika kwamba ni Wakwepa Kodi wanaotaka kuiibia serikali?!

Hata wale Slow Learners, hatimae hivi sasa watauona upendo huu wa Mheshimiwa Rais… upendo kwa watu wote hata kwa WAHUJUMU WA UCHUMI!

Sakata la Makontena ya Makonda ni la tangia February 2018!!! Kwa maana nyingine, JPM alishafahamu kwamba Makonda ni mkwepa kodi toka miezi kadhaa iliyopita! Lakini pamoja na yote hayo, bado Rais ameendelea kufanya kazi na Mkwepa Kodi kwa miezi yote hiyo!!

Amini amini nawaambia, ni wale tu wenye moyo wa upako ndio wanaoweza kuwakingia kifua Viongozi wa Umma Wakwepa Kodi kwa muda wote huo!!!

Hebu tumnukuu Rais Magufuli:

"...Sasa ukichukua makontena kule. Umezungumza labda na watu wengine au na wafanya biashara. Unasema una makontena yako halafu ukasema ni ya walimu! Wala hata shule hazitajwi! Maana yake nini? Maana yake si unataka utumie Waalimu ulete haya makontena. Utapeleka shule mbili tatu ndizo zitapewa na mengine unaenda kuyauza upeleke kwenye shopping mall!”

Je, Mheshimiwa Rais ameropoka? Ukiangalia hiyo nukuu utaona wazi kwamba Rais Magufuli anatuambia Watanzania kwamba Paul Makonda anatumika na wafanyabiashara kuihujumu nchi kupitia kodi!!! Btw, hiyo shopping mall ni ipi?! Ni ile ile ya wale wale waliomwekea Makonda fenicha ofisini au kuna nyingine?!

Hivi ni Mtanzania gani anaweza kushindwa kuuona ujasiri huu wa Mheshimiwa Rais kwa kuweza kuendelea kufanya kazi na mtu ambae ameshathibitisha kwamba anataka kuliibia taifa?! Ni mara ngapi ameshafanya hii michezo huko nyuma?!

Ni huu ujasiri wa Mheshimiwa Rais ndio unaonifanya nimpongeze!!!
 
Pole sana ndugu yangu kwa post yako imelenga kumshambulia mtu muache mkuu wetu afanye kazi maana Utapata taabu sanaaaaaaaa
 
Eti at least amekemea!! Amekemea nini?! Mtu ameshajidhihirisha wazi kwamba analiibia taifa na rais anafahamu kwa miezi kadhaa sasa halafu unadai eti amekemea wakati bado yupo madarakani?!

Kuhusu watu wangapi awamu zilizopita walikuwa hawalipi kodi sio mjadala bali mjadala unahusu Kiongozi wa Umma kukwepa kodi!! Wafanyabiashara wanafahamika kwa kukwepa kodi... walikuwa wanakwepa awamu zilizopita na hadi leo wanaendelea kukwepa!!

Issue iliyopo mezani ni Kiongozi wa Umma kuthibitika kuwa mkwepa kodi!!!
Hivi wewe kijana huwa unatoa wapi busara za kiwango cha juu namna hii ilhali wewe uko chini ya miaka 35?
 
Acha kubeti!!

Hata magu akihamia chadema aapokelewa tu na shangwe kibao!
Kama anauthubutu fanye hivyo kesho! Awe na uhakika wanaompongeza mpaka wnamuunga mkono kwa kujiuzulu na kumshangilia watampa kura za kutosha kumrudisha ikulu.

Mwenye masikio na asikie.
Hivi wewe ndugu yangu maneno ya maana namna hii na hekima hii umeitoa wapi,kama sio mtumishi wa Mungu wewe?
 
Kwa nionavyo Mimi Kauli ya Rais imefunga mjadala wa makontena.
Bottom line is kila mtu anayowajibu wa kulipa kodi.
Wewe kila mtu humu jukwaani anakufaham kwa ujinga sidhani kama kuna mtu atakutilia maani kauli zako,wewe ni sehem ya tatizo.samahani kama lugha yangu itakukwaza.
 
Pole sana ndugu yangu kwa post yako imelenga kumshambulia mtu muache mkuu wetu afanye kazi maana Utapata taabu sanaaaaaaaa
Unajua maana ya kumshambulia mtu?!

Kuna popote nilipozungumzia issue za Magu na familia yake?

Kuna popote nilipozungumzia issue za Magu na marafiki zake?

Kuna popote nilipozungumzia issue ya Magu ndugu zake?
 
Atleast amekemea. Hiv ww unajua awamu zilizopita watu wangapi walikuwa hawalipi kodi pale bandarini

Sent using Jamii Forums mobile app
Hathari ya afya kudumaa kwa watoto 60% tz .sio mwili tuu ni pamoja na akili na madhara hayaishi ataa ukikuwa na kupata lishe bora .kwa hiyo jitafakari huko kundi lipi kabla ujatoa wazo lako kwa jamii ya 60% waliodumaa akili na mwili na 40% wenye akili Kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom