Eti walitaka kuandamana kumpongeza Muungwana...

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
kwa kipi hasa alichokifanya!? :confused:
Hawa wanafiki wa CCM kwa kujibaraguza!! Mbona hawajaandamana kumpongeza Slaa aliyeibua uozo mkubwa ndani ya BOT uliosababisha wizi wa mabilioni ya shilingi!? Mbona hawajaandamana kumpongeza Zitto kwa kuibua uozo mkubwa kuhusiana na mkataba wa Buzwagi ambapo yote aliyosema yalikuwa kweli tupu na mkataba ambao hauna manufaa yoyote kwa Watanzania?


JK azima maandamano CCM

na Waandishi Wetu
Tanzania Daima

RAIS Jakaya Kikwete amezima maandamano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyokuwa yafanyike kwa ajili ya kumpongeza kwa hatua yake ya kutengua uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu, (BoT), Daudi Balali.
Maandamano hayo ya CCM yalipangwa yafanyike nchi nzima kwa siku tofauti ambapo Mkoa wa Dar es Salaam na Lindi, ilipanga kufanya maandamano hayo juzi.

Habari kutoka ndani ya CCM, zinasema kuwa Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, awali hakuwa na taarifa ya kuwapo kwa maandamano.

Vyanzo vyetu vya habari vya kuaminika vimesema CCM iliamua kufanya maandalizi hayo kimya kimya bila kumjulisha rais kutokana na hulka yake ya kukataa kuandaliwa maandamano, hafla au mapokezi ya kishindo na tayari alishazima maandamno ya aina hiyo siku za nyuma.

"Safari hii pia chama kimejiandaa, lakini dakika za mwisho akapata taarifa hizo, akapiga 'stop', akaamuru yasifanyike na hataki kusikia kitu kama hicho, basi tumeshindwa na hatutafanya tena maandamano, maana bwana mkubwa hayataki..," chanzo chetu cha habari kilisema.

Kwa mujibu wa habari hizo, Mkoa wa Dar es Salaam tayari ulishakamilisha maandalizi ya maandamano hayo ambayo yangeishia katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba na kufuatiwa na hotuba za pongezi na hatimaye Rais mwenyewe angezungumza na wanachama wa CCM.

Maandamano hayo mbali ya kuwa na hotuba, yangesindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kundi la burudani la CCM, Tanzania One Theater (TOT) na makundi mengine.

Mkoani Lindi nako, taarifa zinasema kuwa, baadhi ya maofisa waandamizi wa chama hicho walisafiri hadi Lindi kushiriki maandamno hayo, lakini hayakufanyika kutokana na Rais Kikwete kuyapiga marufuku.

Akizungumzia hali hiyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Barongo alikiri kuahirishwa kwa maandamano yaliyoandaliwa na mkoa wake.

Alisema maandamano hayo yaliahirishwa baada ya mgeni rasmi aliyetarajiwa kuwapo siku ya maandamano (juzi), kuwa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 44 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Kweli tulikuwa na maandamano, lakini tumeyaahirisha hadi hapo tutakapokaa na kupanga tena, kwa kuwa mgeni rasmi ambaye tulikuwa tumemwandaa alikuwa kwenye sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar," alisema Barongo.

Hata hivyo, Barongo alipobanwa kutaka ataje jina la mgeni rasmi ambaye kukosekana kwake kumesababisha kuahirisha maandamano hayo, alikataa katakata kumtaja.

"Mgeni rasmi unataka kumjua wa nini? Haina haja, kwani maandamano si yameahirishwa? Hayo mengine yatakuwa na mgeni rasmi mwingine…." alisema Barongo.

Aidha, Barongo alikana kuwa Rais Kikwete ndiye aliyezima maandamano hayo kwa madai kuwa Kikwete hakuwa na taarifa ya kuwapo maandamano hayo.

Vyanzo zaidi vya habari vilisema kuwa hii ni kawaida kwa Rais Kikwete kuzima maandamano, kwani alishazuia kufanyika maandamano ya kumpongeza pale alipotunukiwa tuzo ya Leon Sullivan na wafanyabiashara wa asili ya Kiafrika waishio nchini Marekani, kwa kukubali mkutano wao ufanyike Arusha Juni mwaka huu.

Pia Rais Kikwete alikataa kufanyiwa hafla ya kupongezwa hivi karibuni baada ya mkutano mkuu wa CCM Dodoma, ambapo alichaguliwa kwa kura nyingi za ndiyo kwa ajili ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Wiki iliyopita, Rais Kikwete alitengua uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Ballali na kumteua Profesa Beno Ndulu kuwa gavana mpya.

Rais Kikwete alitengua uteuzi wa Ballali kwa madai ya kukiuka kwa makusudi sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwa ikisimamiwa na Benki Kuu.

Hasira hizo za Rais Kikwete zimetokana na kubainika kuwa kampuni 22 zikitumia hati na nyaraka bandia au zikiwa hazina usajili halali, zililipwa zaidi ya sh bilioni 133 na BoT kupitia akaunti ya EPA.

Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alitoa agizo la miezi sita kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, Mkurungenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuhakikisha wanachunguza na kuwachukulia hatua wahusika wa ubadhirifu huo wa kihistoria.

Wengi walimpongeza Kikwete kwa hatua hiyo, lakini wachache wakihoji uhalali wa rais kutengua uteuzi wa Ballali badala ya kumfukuza kazi.
 
1.Mambo ya North Korea noma. Wengine ni kujikomba, wengine ni kukosa kazi, wengine ni kukosa dira na muelekeo kama alivyosema marehemu Kolimba.


2.Kwa nini Kikwete anakataa maandamano? Dhamiri inamsuta.Inataka mtu awe Stalin kweli kweli kukwiba mimilioni yote halafu kuangalia mijitu lukuki inaandamana juani kukupongeza.Muungwana ana uso wa haiba.

3.In any case the tragi-comic continues, tumeumia.
 
Hizo ni propaganda tupu mkuu, kwa sababu kwa wasioelewa ni dhana tu ya kujiweka sawa kisiasa on both side, kuanzia rais mpaka CCM yenyewe, do not buy into it mkuu maana the whole thing ni pure PR nonesense!
 
Hooooyooooo,

ccm wamechemsha na wamejua kuwa wamechemsha. Kama umemsikia mama meghji kwenye interview na bbc eti anadai kuwa yeye ndiye aliamuru ukaguzi wa BOT ufanyike wakati this witch ndiyo alidhalilisha hoja ya DR Slaa kuhusu BOT.

Unafiki kwa kiwango cha juu sana na wanataka pongezi bila kuzifanyia kazi. Hata Vasco Da Gama angekubali hayo maandamano ila kwa vile Balali bado yuko hai basi jamaa ana wasiwasi maana hajui lini 60 minutes au BBC itarusha story ya Balali
 
mijitu mizima ovyooooooooooo
yani kweli usilolijua ni sawa na usiku wa kizaaaaaa kabsaaaa

ndio yale yaleeeee eti jk amtimua kazi balali wakati mwenyewe alishastaafu zamaniiii??

yaan tusipofunguka macho wa tz tujiandae kuzidi teseka..

wenyewe wanazidi tafuna nchi nyie eti mtembee juani na kuimba na kuimba kumpongeza mwenyewe yuko na wanawake zake if not wachawi wake mikoani huko akila bata na kuongeza charge
 
Mimi sielewi bwana sijui ukishakuwa CCM unazibwa fahamu zote, I really have no idea. Inawezekanaje watu waweze kufikiri tofauti kiasi hicho na watanzania wengine? yaani kama vile wanaishi mbingu ingine kabisa. Sitashangaa na wale jamaa zetu wa Londo nao wakaandaaa ya kwao na Balozi akawa mgeni rasmi. Tutaona mengi kuelekea 2010.
 
Mimi sielewi bwana sijui ukishakuwa CCM unazibwa fahamu zote, I really have no idea. Inawezekanaje watu waweze kufikiri tofauti kiasi hicho na watanzania wengine? yaani kama vile wanaishi mbingu ingine kabisa. Sitashangaa na wale jamaa zetu wa Londo nao wakaandaaa ya kwao na Balozi akawa mgeni rasmi. Tutaona mengi kuelekea 2010.

Kitila,

sababu nimeziorodhesha hapo juu.Kuna wanaojikomba (kina Barongo na viongozi wa CCM wanao-organize maandamano) kwao hao hizi ni nafasi za kujionyesha loyalty yao na ku-network kisiasa regrdless of the issues.Kama Waziri Kiongozi wa Zanzibar kaweka kwenye resume yake fact kwamba aliwahi kuwa MC shughuli ya wedding ya Salimuni Amri (inawezekana kabisa ikawa moja ya milestones zake katika "the art of social climbing") itakuwa kitu kikubwa kama maandamano ya kumpongeza mkulu wa kaya tena?

Kuna wale wasio na kazi na wanaotumia itikadi ya "bendera hufuata upepo" na "if you can't beat them join them" hawa ni pamoja na viongozi wa CCM maskani na vijana wa vijiweni wanaoweza kupozwa kidogo wakaingia kwenye maandamano.

Halafu kuna wale wasio na dira wala muelekeo, wao wawekee mdundiko tu kwenye maandamano wataufuata mpaka Jangwani kwa "mob psychology" tu.

Mimi sioni watu makini wenye integrity wakishabikia charade hii.Ndiyo maana hata mkulu wa kaya mwenyewe kashituka.Maana kaona asije kuwapa watu makini hasira bure.
 
Mimi sielewi bwana sijui ukishakuwa CCM unazibwa fahamu zote, I really have no idea. Inawezekanaje watu waweze kufikiri tofauti kiasi hicho na watanzania wengine? yaani kama vile wanaishi mbingu ingine kabisa. Sitashangaa na wale jamaa zetu wa Londo nao wakaandaaa ya kwao na Balozi akawa mgeni rasmi. Tutaona mengi kuelekea 2010.
Upo sahihi Prof Kitila
 
Mimi sielewi bwana sijui ukishakuwa CCM unazibwa fahamu zote, I really have no idea. Inawezekanaje watu waweze kufikiri tofauti kiasi hicho na watanzania wengine? yaani kama vile wanaishi mbingu ingine kabisa. Sitashangaa na wale jamaa zetu wa Londo nao wakaandaaa ya kwao na Balozi akawa mgeni rasmi. Tutaona mengi kuelekea 2010.
Unalamba matapishi yako
 
Back
Top Bottom