eti wakuu hii ni kweli?

jamiif

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
2,413
990
habari za leo ndugu zangu!
jamani, jana nilikuwa na marafiki zangu sasa katika maongezi tukajikuta tunaongelea ishu ya wivu wa kimapenzi kati ya wanaume na sisi wanawake, ni nani huwa wana wivu zaidi? sasa hapo tulikuwa wadada watatu na wakaka wawili, wao wanadai eti sisi ndio tuna wivu kuliko wao..ila kiukweli jamani mimi kwa upeo wangu, naona kama wanaume wana wivu wa kimapenzi zaidi kuliko sisi wanawake..sasa jamani kwa experience zenu tu au kama kuna karesearch kalifanyika kwa namna moja au nyingine, ebu tueleweshane hapa ndugu zangu. Karibuni sana!
 
Asikwambie mtu,wanaume wana wivu dadangu.
Mwingine mwenye roho ndogo,hakutambulishi hata kwa rafiki zake.
 
umeona ee!!! mi nashangaa wenyewe hawakubali lakini ukweli naona ni huo...wanaume wivu uko juu aisee!!!
Asikwambie mtu,wanaume wana wivu dadangu.
Mwingine mwenye roho ndogo,hakutambulishi hata kwa rafiki zake.
 
habari za leo ndugu zangu!
Jamani, jana nilikuwa na marafiki zangu sasa katika maongezi tukajikuta tunaongelea ishu ya wivu wa kimapenzi kati ya wanaume na sisi wanawake, ni nani huwa wana wivu zaidi? Sasa hapo tulikuwa wadada watatu na wakaka wawili, wao wanadai eti sisi ndio tuna wivu kuliko wao..ila kiukweli jamani mimi kwa upeo wangu, naona kama wanaume wana wivu wa kimapenzi zaidi kuliko sisi wanawake..sasa jamani kwa experience zenu tu au kama kuna karesearch kalifanyika kwa namna moja au nyingine, ebu tueleweshane hapa ndugu zangu. Karibuni sana!

wanawake
 
hata kesi nyingi nilizowahi kusikia zinazohusiana na wivu wa kimapenzi, utakuwa mwanaume ndio anapiga au hata kuua mkewe au mgoni wake...jamani wanaume ebu tuelezeni imekaaje hii?mbona mkiliwa vyenu mwapagawa ila nyie kula vya wenzenu aah, shwari tu....au kwenye mahusiano, ewe mwanaume unatembea tu na wadada nje ya uhusiano wako, ila mpanzi wako akijaribu tu au ukisikia tu kuwa ana uhusiano na jamaa mwingine basi unakuwa mbogo!!why? kwa nini?
 
SISI Wanaume wivu upo,lakini wanawake wana wivu na roho ya ukatili pia.!
Yafuatayo yanaleta wivu kwa pande zote:
[1].Wakati mwingine inategemea mapenzi yanaelemea wapande gani,labda mwanaume anampenda sana mwanamke, au mwanamke anampenda sana mwanaume.!!!!
[2],inawezekana mwanaume una mwanamke mwenye mvuto,na inategemea ulimpata katika mazingira gani,
[3]tena hata life style mnayoishi inaweza kuongeza wivu;mambo yakutoka kwenda viwanja vya starehe,uvaaji.!!!,eti asiongee na mtu,utahisi kuna neno la mapenzi limepita.
[4].wewe upo na super star,lazima uwe na wasiwasi wa kujulikana kwa mwenzio,unahisi kuchukuliwa na wengine.!!!
 
Back
Top Bottom