Eti UVCCM imeshinda chaguzi vyuo vyote vya elimu ya juu

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Nilikuwa namsikiliza dada fulani anaitwa Ester Bulaya katibu wa uhamasishaji uvccm na mbunge radio tbc. alipoulizwa mbona uvccm wame lose ground akasema hapana tumeshika vyuo vyote hata juzi mgombea wetu ameshinda federation udom amemshinda mgombea wa chadema. nikajiuliza kumbe uongozi wa vyuo ni wa tiketi ya chama? kazi ipo
 
ibange yule dada alipewa tu kama sadaka.angejulikana ni wa ccm asingepata.na wamempa mana watu wenye upeo majina yao yalikatwa katika hatua za mwanzo japokua walichukua fomu na kuzirejesha kwa wakati.
 
Ndo maana nape kaenda dodoma?
Ngoja tutaona hizo serikali kama zitamaliza 1yr.
 
Nilikuwa namsikiliza dada fulani anaitwa Ester Bulaya katibu wa uhamasishaji uvccm na mbunge radio tbc. alipoulizwa mbona uvccm wame lose ground akasema hapana tumeshika vyuo vyote hata juzi mgombea wetu ameshinda federation udom amemshinda mgombea wa chadema. nikajiuliza kumbe uongozi wa vyuo ni wa tiketi ya chama? kazi ipo
 
Hao ndo CCM bwana mchana wanadai siasa vyuoni ni marufuku na usiku wanapiga kampeni
 
Kwan uyo ni mbunge au dada msosi wa wazee? Dadavua kwanza.
 
Hapa issue ni simple, UDOM andaeni mikutano miwili mmoja ya cdm na mwingine wa magamba siku hiyo moja. Cdm wapeni ule ukumbi mbaya na magamba wapeni sehemu nzuri kabisa halafu muwaite Nape na Lema kuja kuhutubia kila mtu upande wake.
Mtajua ni cdm au magamba ndo wenye UDOM.
Pia waruhusini magamba walalete hata wanafunzi wa nje kwa malori.

Nadhani hii itamaliza ubishi wa nani ni bingwa zaidi.

Fanyani hivyohivyo vyuo vyote na hata shule za msingi na secondary
 
Lakini nijuacho mie kuhusu uchaguzi wa vyuo vya elimu ya juu ni kwamba pale UDOM kampeni zilitawaliwa sana na UDINI, ukristu na uislamu na hatimaye upande mmoja ukashinda, UKRISTU. Hata hivyo udini huo ulikuwa na msukumo wa vyama vya siasa tena vyama vikuu hapa Tanzania. Fanyeni uchunguzi mtagundua hili.

Juzijuzi ukafuata uchaguzi katika chuo kikuu cha Ardhi hapa Dar es salaam. Kama ilivyokuwa UDOM, ARDHI napo kukatawaliwa na udini, lakini wale walioshinda dodoma hapa ARDHI wakajikuta wakidondoka na hivyo upande wa pili kushinda kuanzia nafasi ya uraia na makamu wake, UISLAMU. Mbaya zaidi hapa Ardhi Rais akafanya uteuzi wa WAZIRI MKUU na bahati mbaya akamteua mfuasi wa dini yake pia. kuona hivyo bunge la ARDHI likakataa kumuidhinisha waziri mkuu huyo na hadi ninapoandika post hii waziri mkuu huyo alikuwa hajaidhinishwa na bunge limeweka ngumu kwa kisa cha UDINI.

Pa,oja ma udini, inadaiwa pia siasa ziliingizwa tangu mapema sana pale UDOM na ARDHI lakini agenda ya udini ikachukua kasi kuliko siasa licha ya kuwepo kwa msukumo wa siasa hata katika huo udini. Hii ni hatari kwa taifa letu.

ONYO: Uchaguzi wa DARUSO uko kwenye maandalizi makali sana kwa sasa na wanasiasa wameshavamia kambi huko tayari. Pia UDINI umeingia huko. Sie wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao hatuna mrengo wa chama chochote na TUCHUKUE HATUA!
 
ibange yule dada alipewa tu kama sadaka.angejulikana ni wa ccm asingepata.na wamempa mana watu wenye upeo majina yao yalikatwa katika hatua za mwanzo japokua walichukua fomu na kuzirejesha kwa wakati.

Nahisi kama you have missed the point. Kwani Ester Bulaya ni mbunge wa chama gani na waliompa ubunge ni wa chama gani?? na hao waliokatwa ni chama gani unaowasema wewe?? Hebu jipange upya uiweke vizuri huja yako then uilete maana kama uko Msamvu na unaelekea dodoma, basi mwenzetu unafuata Iringa Road now!!!!!

Jumamosi nlikuwa chuo cha Mipango Dodoma,kulikuwa na uchaguz wa serkal ya wanafunzi,siasa za vyama zilitawala live,aende akaulize ni nani alishinda sasa,hataamini kilichotokea!!people's power
 
Nahisi kama you have missed the point. Kwani Ester Bulaya ni mbunge wa chama gani na waliompa ubunge ni wa chama gani?? na hao waliokatwa ni chama gani unaowasema wewe?? Hebu jipange upya uiweke vizuri huja yako then uilete maana kama uko Msamvu na unaelekea dodoma, basi mwenzetu unafuata Iringa Road now!!!!!

Mkuu me naona wewe ndio umepotea mchangia hoja hapo juu alikuwa anamlenga huyo mgombea wa UDOM na c Ester Bulaya kama ulivyoamini wewe huo ushabiki punguza basi na usome uelewe ndipo ukurupuke!
 
Back
Top Bottom