Uchaguzi 2020 Eti ‘tunataka Tume huru’ wakati chaguzi za vyama vyenu hazina huo uhuru, wanafiki wakubwa!

Umejenga hoja ifuatayo:

  1. Ndani ya vyama hakuna uhuru
  2. kwenye Tume ya Uchaguzi hakuna uhuru.
  3. Kwa hiyo, kukosekana kwa uhuru katika Tume ni jambo halali.

HAPANA! Makosa mawili hayazalishi haki.

Huwezi kusema kuwa kwa vile ndani ya vyama hakuna uhuru basi kukosekana kwa uhuru katika tume ya Taifa ni jambo halali.

That is primitive naive and nonsensical reasoning....
yaani jamaa anaona ni vema kuondoa kero kwa kutumia kero.
wakati huo ni ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko Kigoma wanasema kuwa ukweli hauwezi kuungua hata kama ukipitishwa kwenye tanuru la moto. Tafuta kina zito wakupe exact quotation, mie najua kifipa. Karibu sumbawanga!
Mama Amon, upooo! Aaaaah, umeadimika saaana!
 
Dai la tume huru ya uchaguzi: hiki kiini macho kimekuwa agenda kwa vyama hivi hasa baada ya kukosa agenda mbadala itakayoweza pambanishwa na Ccm iliyojizatiti kwa kujibu vijiagenda vyote vilivyokuwa vikiwapa kiki ktk awamu zilizopita!
Madai yao ni sahihi. Rejea point 10 za Maalim Seif. Halafu sidanganye watu kuwa ccm imejibu ajenda za wapinzani. Kupunguza tu umaskini imewashinda, kutenengeneza ajira mpya imeshindwa. Imejibu baadhi lakini sio zote. Tuwe wakweli
 
Madai yao ni sahihi. Rejea point 10 za Maalim Seif. Halafu sidanganye watu kuwa ccm imejibu ajenda za wapinzani. Kupunguza tu umaskini imewashinda, kutenengeneza ajira mpya imeshindwa. Imejibu baadhi lakini sio zote. Tuwe wakweli
Unasubiri sitatuliwe kwa asilimia 💯! Unautimamu was akili ww kweli!? Yaani asiwepo mtu asieajiriwa, asiwepo maskini ndio useme Magu ni jembe! Hata Mungu mwenyewe ameacha maskini na matajiri kuwepo ktk dunia na hi ndio inafanya umaana was maisha!

Tunaposema Magu ni baba lao tunafananisha na watangulizi wake na pia agenda zilizokuwa zinawapa shavu wapinzani uhuni! Magu ameifanyia haki nafasi ya urais! Mungu azidi kumbariki, kumuongoza, na kumlinda yy binafsi na serikali ya awamu ya tano na Tz kwa ujumla!
 
Unasubiri sitatuliwe kwa asilimia 💯! Unautimamu was akili ww kweli!? Yaani asiwepo mtu asieajiriwa, asiwepo maskini ndio useme Magu ni jembe! Hata Mungu mwenyewe ameacha maskini na matajiri kuwepo ktk dunia na hi ndio inafanya umaana was maisha! Tunaposema Magu ni baba lap tunafananisha na watangulizi wake na pia agenda zilizokuwa zinawapa shavu wapinzani uhuni! Magu ameifanyia haki nafasi ya urais! Mungu azidi kumbariki, kumuongoza, na kumlinda yy binafsi na serikali ya awamu ya tano na Tz kwa ujumla!
Kaifanyia haki? Miaka minne ya fedha kuanzia 2016/2017 mpaka 2019/2020 (mpaka mwezi April 2020) hajatekeleza bajeti ya serikali hata kwa asilimia 70. Kaishia 66, 67, na 66.8. Acheni kelele. Someni documents za bajeti kwa kuanzia. Usipige tu makelele hapa JF
 
Vipi CCM mbona mmechapisha fomu moja ya Uenyekiti vipi kina sumaye hawautaki uenyekiti?
 
Ktk kutafakari juu ya agenda ya vyama pinzani hapa Tz tunapoelekea ujaguzi, nimewaza na kawazua bila kupata majibu juu ya yale yanayojiri kwenye vyama vyenyewe na kile wanachojaribu kushinikiza kifanyike!

Ktk yote vifanyavyo hivi vyama vinajaribu kuhadaa watz kama mtakavyoona kwenye clips hapo chini!

Dai la tume huru ya uchaguzi: hiki kiini macho kimekuwa agenda kwa vyama hivi hasa baada ya kukosa agenda mbadala itakayoweza pambanishwa na Ccm iliyojizatiti kwa kujibu vijiagenda vyote vilivyokuwa vikiwapa kiki ktk awamu zilizopita!..
Vipi ujapata taarifa fomu imeprintiwa moja,mkiambiwa chama ni Mali binafsi ya familia muelewe
 
Awamu zilizopita mbona haikuwa fomu moja,jamaa hawezi bila kubebwa
Kizuri kinajiuza! Magu kwa ccm ameshauzika na kuadimika! Hawawezi kufanya makosa kulipoteza jembe lao lililosababisha upinzani wapotezane! Jezea Magu we?
 
Kuwa na tume mpya ya uchaguzi ambayo inategemewa kuwa huru ita maanisha kufanya marekebisho ya katiba. Hata kama unaweza kusema kwamba muda hautoshi kufanya marekebisho hayo inabidi tu angalie vikwazo vingine ambavyo ni vikubwa zaidi kama vile gharama, usalama wa nchi haswa katika kipindi hiki cha uchaguzi na majidiliano ambayo yataji tokeza bungeni yasiyo na tija na matokeo chanya.

Nafikiri suluhisho ni kufanya tathmini ya tume yetu ya uchaguzi ili ku fahamu kama ina weza kusimamia uchaguzi ulio wa huru na haki tuki wahusisha wahusika wote.
 
Iko huru kutangaza mshindi, haiko huru kuonyesha mshindi amepatikanaje.
Rejea majibu ya Damian Lubuva alipobanwa kuhusu matokeo akajibu "mimi natangaza matokeo ninayoletewa"
Acheni unafki. Wabunge zaidi ya mia moja waliingia bungeni kupitia tume ipi? Upinzani wa kipindi hiki umekosa Sera.
 
Kizuri kinajiuza! Magu kwa ccm ameshauzika na kuadimika! Hawawezi kufanya makosa kulipoteza jembe lao lililosababisha upinzani wapotezane! Jezea Magu we?
Jembe kwa nguvu ya wanufaika.
Kipi chema kafanya zaidi ya propaganda.
:Ameuwa uchumi
: Hawezi tatua shida ya ajira
: Kashindwa kuwalinda watz dhid ya wasiojulikana
:Kaumiza Makundi yote kwenye Jamii
:Katuharibia diplomasia yetu
:Anawakomoa watumishi kwa kuwanyima haki zao.
:Amebomoa utaifa wetu
:Amesababisha wengi wamekimbia ukimbizini.
Amewasomesha watu namba ili awatawale
Mtu yeyeto mwenye akili timamu hawezi rudia makosa.
Afai kuongoza watu labda wanyama.
Angekuwa anakubalika hofu ya nn kuprint fomu moja.Nje ya kubebwa hawezi shinda chochote hata ubunge alibebwa na si jitihada binafsi za hoja.
Hayupo kwa ajili ya kutatua shida za watz Bali kupambana na watu.Wasiotaka kumuabudu wako ndani uhujumu wenye chapa the same mistake wako nje sababu ni waimba kwaya wazuri
 
Hustahiri wewe ata kujibiwa, ati nyie wananchi, sema sisi matahahira wa uvccm, hakuna mwenye akili nzuri aweza kuunga mkono uharo huu wako.
Sisi wananchi tunajua hii tume ni huru kwa mujibu wa katiba ya JMT ibara ya 74(7) na hufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni.
 
Back
Top Bottom