Hero
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 3,932
- 2,832
Katika kutafakari juu ya agenda ya vyama pinzani hapa Tanzania tunapoelekea Uchaguzi, nimewaza na kawazua bila kupata majibu juu ya yale yanayojiri kwenye vyama vyenyewe na kile wanachojaribu kushinikiza kifanyike!
Katika yote vifanyavyo hivi vyama vinajaribu kuhadaa watz kama mtakavyoona kwenye clips hapo chini!
Dai la tume huru ya uchaguzi: hiki kiini macho kimekuwa agenda kwa vyama hivi hasa baada ya kukosa agenda mbadala itakayoweza pambanishwa na Ccm iliyojizatiti kwa kujibu vijiagenda vyote vilivyokuwa vikiwapa kiki ktk awamu zilizopita!
Hivyo kwa sasa hawana agenda yenye mashiko ya kuipinga CCM! Uhalisia kwenye vyama vyao ni kinyume kabisa, huko hakuna utaratibu uliowazi na huru katika kuendesha chaguzi zao wenywe, na ndio maana kila kukiwa na uchaguzi ktk vyama hivi lazima malalamiko yatokee ya namna viongozi wao wa juu wasivyoruhusu huo uhuru wa vijitume vyao vya uchaguzi, lakini viongozi hao hao ndio wanahadaa watz kutaka kushinikiza tume huru.
Ingekuwa ni jambo la hekima kama wangeanza kuonyesha uwepo wa tume huru kwenye chaguzi zao za vyama kabla ya kunyooshea kidole tume yetu ya taifa ya uchaguzi ambayo inao uhuru kwa kiasi kikubwa hata kuliko kwenye vitume vya vyama vyao ambavyo havina uhuru hata kidogo! Anachosema na kutaka Zito au Mbowe ndio kinachotekelezwa na vijitume vyao vya uchaguzi!
Kwa maana hiyo, hawa watu hawana hadhi ya kuomba tume huru ya taifa ya uchaguzi zaidi ya hii iliyopo yenye uhuru wa kutosha usio holela!
Jambo jingine ni uhuru wa kujieleza: hiki kiini macho cha akina Mbowe na Zito ni cha kitoto sana. Hawa jamaa kila kukicha wanaitisha news conference bila kubugudhiwa na mtu, wanamwaga poroja zao, mwisho wa siku wanasema hawana uhuru wa kujieleza! Huu nao ni ujuha!
Ukirudi kwenye vyama vyao, wajumbe na wanachama wao hawaruhusiwi kuhoji mienendo ya viongozi wao hasa wa juu, na wakifanya hivyo ki ndakindaki wanashughurikiwa!
Sasa hawa kina Mbowe na Zitto wanapata wapi ujasiri wa kudai vitu ambavyo wao wenyewe hawawezi kuwapatia wanachama wao? Huu nao ni unafiki kupindukia!
Ngoja niishie hapa, tazameni wenyewe ticktak na faulo zinazochezwa huko kwenye vikundi vya kihuni vinavyojipanga kusaka ruzuku!