Eti Trump ameomba mazungunzo ya mezani na Korea Kaskazini?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,117
2,000
Kuna taarifa kuwa eti Marekani sasa imeomba kukaa meza moja na Korea Kaskazini kufanya majadiliano badala ya vitisho na ubabe. Kama hii kweli, inamaanisha nini?
 

henry vascos

Member
Jan 2, 2013
45
95
nachojua,wazir wa mambo ya nje wa urusi ndiye aliyeleta ujumbe kutoka NK kwamba wanataka warejee kwenye meza ya mazungumzo akimwambia mwenzake wa mambo ya nje wa US na wakakubaliana iwe hivyo,ila white house imegoma mazungumzo hayo vinginevyo NK waharibu siraha zao zote za nyuklia
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,117
2,000
Mkuu Marekani hawezi Ku retreat kirahisi namna hiyo....
Marekani itayari kuzungumza na Korea Kaskazini
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Korea Kaskazini bila ya kuweka masharti yoyote.


Tillerson lakini amesisitiza wanadhamiria kuishinikiza nchi hiyo kuachana na mpango wake wa nyuklia.

China na Urusi zimelipokea vyema tamko hilo la Tillerson licha ya Ikulu ya Rais wa Marekani kuonekana kutilia shaka mtizamo huo baada ya kutoa taarifa kuwa mtizamo wa Rais Donald Trump kuihusu Korea Kaskazini haujabadilika.

Licha ya kuwa msemaji wa Ikulu ya Rais wa Marekani - White House, Sarah Sanders kutosema moja kwa moja maoni ya Trump ni yapi, Rais huyo katika kipindi cha nyuma amenukuliwa akisema Waziri wake wa mambo ya nje anapoteza muda kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini.

Kremlin inafurahishwa na matamshi ya tija ya Tillerson

Nchini China, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lu Kang, amesema China ina matumaini kuwa Marekani na Korea Kaskazini zitachukua hatua za tija kuelekea mazungumzo ya moja kwa moja yatakayopunguza mzozo katika rasi ya Korea.


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UN

Nchini Urusi, msemaji wa Ikulu ya Rais ya Kremlin Dmitry Peskov amewaambia wanahabari kuwa matamshi ya tija kama aliyoyatoa Tillerson yanawafurahisha zaidi kuliko cheche za maneno na vitisho ambavyo wamekuwa wakisikia hadi sasa, na mtizamo huo mpya wa Marekani unapokelewa vyema.

Huku Tillerson akisisitiza umuhimu wa kuwepo mazungumzo kati ya nchi yake na Korea Kaskazini ili kuutatua mzozo wa kinyuklia, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameapa kulifanya taifa lake lenye nguvu zaidi kinyuklia na kijeshi duniani.

Trump ameahidi kuwa Kim hataruhusiwa kufanikisha malengo yake ya kuunda silaha za kinyuklia zilizo na uwezo wa kushambulia Marekani. Marekani imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza juhudi za kidiplomasia za kuitenga Korea Kaskazini na kuukwamisha uchumi wa taifa hilo kupitia vikwazo.

Maafisa wa Korea kaskazini hawakuonesha kuwa tayari kwa mazungumzo

Hapo jana katika hafla mbili tofauti, Trump alionya kuwa juhudi hizo za kuiadhibu Korea Kaskazini zitaendelea hadi pale bomu la kwanza litakapodondoshwa. Hata hivyo amesema milango ya mazungumzo na Korea Kaskazini iko wazi zaidi wakati huu kuliko kipindi cha nyuma, akilegeza msimamo wake mkali aliokuwa nao kuhusu nchi hiyo.


Korea Kaskazini inataka iwe nguvu kuu ya zana za Nyuklia duniani

Jeffrey Feltman mkuu wa masuala ya kisiasa wa umoja wa Mataifa ambaye ameizuru Korea Kaskazini hivi karibuni amesema maafisa wa nchi hiyo wamemueleza kuwa ni muhimu kuepusha vita lakini hawakupendekeza bayana kuwa tayari kwa mazungumzo.

Mwishoni mwa juma lililopita, Feltman alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Ri Yong- Ho na naibu wake Pak Myong Kuk katika ziara hiyo ya kwanza kufanywa na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini humo tangu mwaka 2011.

Mwandishi: Caro Robi/afp

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
 

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,037
2,000
Mkuu asante kwa kunijuza aiseh....But nadhani ni economic interest ya marekan,huenda wanahofia kupoteza economic power wakipigana na hawa wakorea wa kaskazini
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,117
2,000
Mkuu asante kwa kunijuza aiseh....But nadhani ni economic interest ya marekan,huenda wanahofia kupoteza economic power wakipigana na hawa wakorea wa kaskazini
Ni mwiko kabisa kuanzisha vita na mtu ambae hujui vizuri uwezo wake halisi. Intelejensia ya Marekani haina taarifa kamili na muhimu kuhusu nguvu na technolojia ya kivita ya North Korea mpaka sasa. Kim anawachinja kabisa watu wote anaohisi kuwa watavujisha siri za kijeshi za Korea Kusini, hata kama awe baba yake mzazi.
 

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
2,037
2,000
Ni mwiko kabisa kuanzisha vita na mtu ambae hujui vizuri uwezo wake halisi. Intelejensia ya Marekani haina taifa kamili kuhusu nguvu na technolojia ya kivita ya North Korea mpaka sasa. Kim anawachinja kabisa watu wote anaohisi kuwa watavujisha siri za kijeshi za Korea Kusini, hata kama awe baba yake mzazi.
Mkuu hii hatari nyingine...Kim a.k.a mapanki hana mchezo katika hili
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,730
2,000
Nani aharibu silaha? ili kuwa mfano wa kuigwa usa aanze yeye kuharibu hayo madude yake siyo wenzake waharibu yeye abakize yake ghalani kwani ni pipi hizo Kim Komaa hakuna kuharibu ukijaribu tu umeisha
 

Nalendwa

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,505
2,000
Not so fast!, - Friday Dec 15, 2017 - UN

"North Korea must earn its way back to the table"~ Rex Tillerson

..During Friday's specially convened UN Security Council meeting to discuss North Korea's nuclear program, Tillerson clarified that "a sustained cessation of North Korea's threatening behavior must occur before talks can begin. North Korea must earn its way back to the table.."
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,672
2,000
North Korea ni karata ya ushindi uchaguzi wa 2020 ndio maana Trump amewaweka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom