Eti Tanzania kuondoka katika kundi la nchi maskini ifikapo 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Tanzania kuondoka katika kundi la nchi maskini ifikapo 2015

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by John W. Mlacha, Oct 22, 2012.

 1. J

  John W. Mlacha Verified User

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Naibu Katibu Mkuu Mtendaji Ofisi ya Rais Kamisheni ya Tume ya Mipango, Bw. Clinfford K. Tandari ameayasema hayo kwenye majadiliano yaliyohusu Utekelezaji wa Mpango wa Istanmbuli kwa nchi maskini maarufu kama LDGs. Mkutano huo ulifanyika nchini ya Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa. Alipopata nafasi ya kuchangia utekelezaji wa Mpango huo ( Istambul Plan of Action) Bw. Tandari pamoja na mambo mengine, alisema Tanzania imekwisha kuuingiza mpango huo katika Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa Kila Miaka Mitano , lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania inaondoka katika kundi la nchi maskini na kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati ( Middle Income Countries), ikifikapo mwaka 2015. Akabainisha kwamba ili kufikia hatua hiyo, Serikali imejiwekee vipaumbele kadhaa ambavyo vimeainishwa katika Mpango huo wa Miaka mitano. Akavitaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni Kilimo na Usalama wa Chakula, uboreshaji wa huduma za Elimu, Afya na huduma za maji na usafi wa mazingira, maendeleo ya miundombinu ikiwamo ya barabara, reli, bandari na huduma za nishati. Akavitaja vipaumbele vingine kuwa ni usawa wa kijinsia na uwezeshashi pamoja na kujenga mazingira bora ya biashara na ushindaji wa kibiashara. Katika hatua nyingine Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Rais Kimisheni ya Mipango alieleza kwamba Tanzania ingeweza kufikia lengo lake la kutoka katika kundi la nchi maskini na kuwa kundi la nchi ambazo uchumi wake ni wakati kabla hata ya mwaka 2015 ikiwa tu washirika wa maendeleo ya kichumi watatekeleza ahadi zao za kuisaidia Tanzania zikiwamo zile walizotoa miaka mingi ya nyuma na ambazo hazijatekelezwa hadi sasa. Hata hivyo akasema Tanzania imejidhatiti katika kuhakikisha kwamba inaboresha makufanso ya mapato yake ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kodi na kuibua vyazo vipya vya mapato ili kuziba pengo litokanalo wa wadau wa maendeleo kushindwa kutekeleza ahadi zao
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  kituko kingine.....hawa viongozi JK anawatoaga wapi?
   
 3. n

  nummy JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 589
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayetaka kuondoka huko, bora tuwape madini yote, dhahabu,tanzanite, rubi, almasi, uranium, na wanyama ili sisi tubakie masikini ili tuwe tuna enda kuomba msaada
   
 4. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  kwan miaka 50 tulikuwa wap au tunaamin kwenye miujiza
   
 5. f

  filonos JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  ilipo fika mwaka 2002!!....kulikua na ahadi kama hiyo kua ifikapo 2013 ..kila MTANZANIA atakunywa maji Safi mpaka hii leo hata dalili hakuna hiyo ilikua ni Ahadi ya Selikari ya Awam ya 3 kwahiyo hizo na ahadi za MAKABRASHA 2 ziponyingi hizo
   
 6. M

  MJM JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni kweli haya makabrasha yapo mengi sana huko wizarani. Kwahiyo tumebakiza miaka miwili na kidogo kuhama umaskinini! Sijui watakuwa wamebaki kina nani huko?. Ninavyojua mipango yao wanaweka leo miaka mitano ijayo wanafanya kidogo kisha wanachelelea kama zuzu utadhani wametoa mifukoni mwao kumbe ni kodi zetu.

  Pointi niliyoipata ni kutofikia malengo ya kuhama kenye umaskini kabla ya 2015 kutokana na washirika wa maendeleo kutokutimiza ahadi zao. Kwa hili naikubali serikali ya Tanzania na halina ubishi ila najiuliza "Tunapanga kuondoka katika umaskini kwa kutegemea kuomba!" Kumbe Matonya (RIP) hakuwa kwenye kundi la maskini ila tu waliokuwa wanadondosha sarafu kwenye kikombe hawakumwezesha.

  Kwa mawazo haya ya viongozi wetu safari ni ndeeefu sana
   
 7. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,534
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Siku zote huaga najiuliza,hivi ukiwa kiongozi uwezo wa kufikiri unashuka?
   
 8. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Wonder the same thing mkuu, yaani sijui huwa wanagawa wapi akili zao wakianza uongozi aisee!
   
 9. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Vote this to enter in new Seven Wonders of the World
   
 10. S

  Savannah JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli ni aibu kwa JK na watu wake aliowateua
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ndiyo, Tanzania itaondoka kwenye kundi la nchi maskini kwenda kwenye kundi la nchi maskini saaana hapo mwaka 2015. Vinginevyo kama huyu jamaa anamaanisha CCM kung'oka ili ujambazi inaofanywa ufutike na pesa iliiyokuwa ikiibiwa itusogeze mbele. Vinginevyo chini ya CCM hii hii tutazama zaidi wanangu.
   
 12. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  Tanzania ikitoko uko zitabaki zipi?
   
 13. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  alikuwa anajufurahisha au anataka kufurahisha umati, umaskini tangu lini ukaondoka bila mipango na utekelezaji wa hiyo mipango. rushwa uzembe uvivu wa kufikiri na uroho wa kutafuna pesa za mali za watanzania kamwe hazitatutoa katika umaskini. na uraisi kama wa vasco na viongozi wenzake, utajiri tanzania ni ndoto za alinacha
   
 14. J

  John W. Mlacha Verified User

  #14
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Definetly they have my vote. wakishakaa ndani ya ma vx yao wanajua kuwa wanancho wote ndio wanavyoishi kama wao
   
 15. J

  John W. Mlacha Verified User

  #15
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Maana yake hakutakuwa na nchi maskini duniani tena . Which is impossible
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ameona mbali kwa kuwa chadema itashika nchi 2015,tusimbeze!
   
 17. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  kama rwanda imetupita! then hakuna possibility ya cc kuendelea tena! itabaki historia! hii yote ni kutokana na kuwa na rais DHAIFU, poor us!
   
 18. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  inaweza kuwa ya kwamba kufika 2015, wananchi wengi watakuwa wameathiriwa na umaskini na kufikia vifo vya masikini wote, hivyo miongoni mwa watakaobaki hatakuwemo maskini.
  Yamkini ifikapo2015 tanzania si katika nchi masikini bali katika nchi zenye kuchukiza kwa umaskini na matatizo.
  Au itakuwa haimo katika nchi zinazopimwa.
   
 19. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Huyo Msemaji alikuwa anongea KISWAHILI; KIINGEREZA au KISWA-ENGLISH???

  Sababu SIDHANi alisema hivyo...
   
 20. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,534
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Inawezekana AC za vx zinawaharibu ubungo na kushusha uwezo wa kufikiri,huyu si wa kwanza na wapo watafuata kwa kauli za kijinga kama hizi wakiamini wananchi ndizo wanazozitaka.
   
Loading...