Eti Takukuru wameanza kufanya uchunguzi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Takukuru wameanza kufanya uchunguzi!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jibaba Bonge, Jul 20, 2011.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza uchunguzi wake juu ya madai hayo ya Wizara ya Nishati na Madini kuzichangisha taasisi zilizo chini yake fedha kwa ajili ya kufanikisha bajeti hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema jana kwamba tuhuma hizo ni nzito na tayari taasisi hiyo imeanza kuzichunguza.Alisema taasisi yake inafanya uchunguzi kwa umakini na kwamba kila anayetuhumiwa atapewa nafasi ya kujitetea na kusisitiza kwamba ofisi yake inalichukulia suala la nishati ya nchi kwa uzito mkubwa."Tumeshaanza uchunguzi... jambo zito kama lile hadi Bunge linaahirishwa unafikiri tunaweza kuliacha hivihivi? Suala la nishati tunalichukulia ‘very serious'. Tutafanya uchunguzi wetu na tutaona matokeo baada ya kukamilika," alisema.
  Source :Mwananchi

  Kwa jinsi nianavyo muelewa Dr.Hosea; matokea ya uchunguzi yatakuwa ' Hakuna uthibitisho wa kutosha kuonyesha kulikuwa na vitendo vya rushwa na na fedha zilizoingizwa kwenye akaunti hiyo zilikuwa na miradi jiolojia'.
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa kama uchunguzi utakuwa hauna ushahidi wa kutosha kumpeleka mtu mahakamani unataka asemeje? Facts lazima ziendane na Vifungu husika vya Sheria na kama kutakuwa na mifarakano (conflicts) katika vitu hivyo viwili basi haiwezekani mtu kupelekwa mahakamani!
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Sawa tumekubali TAKUKURU waingie na kufanya uchunguzi lakini HOSEA asije na majibu yake mepesi ya kukosa ushahidi.Ushahidi huu hapa
  1. Barua iliandikwa kwa taasisi zote za Nishati na MADINI
  2. bARUA IMESAINIWA NA Jairo na imeandikwa kwa reference number za file husika-watu wako waone file
  3. Pesa zimeingizwa kwenye account iliyotajwa
  4. Pesa zimetolewa zote kwenye account iliyotajwa na kwa muda mfupi
  5. aNGALIENI KAMA MATUMIZI HAYA YALIPITISHWA NA BUNGE mwaka jana
  Short of that tunataka kusikia Mawaziri husika, makatibu husika na wakurugenzi wa taasisi husika wanaingizwa kwenye mkondo wa sheria.HOSEA USITULETEE HABARI ZAKO NYEPESI AS IF HUJAENDA HUNA UZOEFU NA KAZI YAKO
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tanzania ukifanikiwa kuiba hela nyingi upo salama maana utalindwa sana na serikali/viongozi, lakini ole wako uibe kidogo hawakucheleweshi, kama unabisha jaribu uone
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pia ataje ni Sheria ipi imevunjwa! Facts lazima ziendane na vifungu vya Sheria, otherwise mtu ataonekana hana hatia!
   
 6. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hivi Takukuru wapo? Kesi za aina hii wao walitakiwa wawe wa kwanza kuzishughulikia kabla ya kufika hata bungeni. Kwa Takukuru naondoa SHILINGI!
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa kufanya uchunguzi wakati watuhumiwa wakiwa bado kwa ofisi haina mantiki.

  Kama wako serious wawasimamishe kazi haraka sana wanao tuhumiwa wote ili kuhakikisha kuwa hawaharibu ushahidi.
  La sivyo wataenda takukuru pale na kutoka na chai nzito na kuzima ushahidi..

  Eh Tz Tz NAKUPENDA KWA MOYO WOTE!
   
 8. m

  mhondo JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kama issue iliibukia bungeni kwanza na Takukuru hawakuwa na taarifa nayo inawezekana vipi wao waishughulikie kabla ya kufika bungeni?
   
 9. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa kama mama Beatrice Shellukindo kakimbilia kwanza Bungeni wao wangemzuia?
   
 10. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  TAKUKURU-TAasisi ya KUpokea na KUla RUshwa
   
 11. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mkuu, ni huyu huyu Hosea aliye i-clear scandal ya Richmond lakini tume ya Bunge ikagundua madudu mengi, ni yeye huyo huyo alimclera Chenge halafu SFO na ubalozi wa uingereza wakakanusha. Sasa hapa reliability ya Hosea iko wapi? Sana sana waishia kukamata wamachinga wanaowahonga mgambo wa jiji shs 500 na kutangaza kwenye media zote kuwa wamekamata wala rushwa! naweza kuwa nakujibu kumbe wewe mwenyewe ndiye Hosea! Hata hivyo habari ndiyo hiyo na ujumbe umefika.
   
 12. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Thibitisha
   
 13. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Mimi siamini Takukuru kabisa.

  hawa sio ndio walimsafisha Chenge?
   
 14. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,281
  Trophy Points: 280
  TAKOKURU ni aina flani ya CBO tu- ipo pale ili watu flani wapate ajira tu.
   
Loading...