Eti "Siye tunaingia Mpaka Ndani Kukagua Mahabusu/Magereza" - Mwenyezi Mungu anawaona Mawakili wa Serikali

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Du! Kama wewe mwenyewe unakiri umetoka huko umewaacha sasa sijui ulistaafu au imekuwaje mpaka uko private! Sasa kwa maana hiyo ukipata kesi ukabishane nao utaiacha?
sijastaafu, hata miaka 40 sijafika. nimetoka kwasababu sipendi mshahara nilianzisha law firm yangu binafsi. upo hapo? nikipata kesi wengi ninao bishana nao tunajuana kwasababu nimefanya nao kazi, wengi wao nawajua ubora wao na udhaifu wao. na tunaheshimiana. tukiwa mahakamani ni vita tu muraa, ila tukitoka tunasalimiana kama ndugu.
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
mkuu, uwezo kwenye kesi za criminal hao mawakili wa serikali wapo juu sana kuliko wa kujitegemea na hao wanaoendesha kesi ya mbowe zaidi ya wanne ni viongozi wafawidhi ya mikoa na wilaya. nawajua, niliwapokea kazini baadaye nikawaacha huko serikalini.

ukienda gerezani, treatment anayopata kibatala au ninayopata mimi kama wakili wa kujitegemea na wao ni tofauti, wao ni serikali wanapigiwa hadi saluti.

pia ukitaka kujua tofauti yao na wengine ambao hawajapitia kweney ofisi zao, angalia hii application amefanay Advocate Hekima mwasipu dhidi ya Makonda, nilitamani sana makonda ashitakiwe, lakini mwasipu ameweka application yenye nyaraka zote batili hadi hati ya mashtaka hajui kabisa kuandaa, ni batili, everything pale ni batili . huo ndio ulinganisho mnatakiwa kuufanya.
Umeandika vizuri lakini ulivyomalizia sikubaliani nawe kabisa! Nina sababu nyingi sana sana ila sitaki kuji-expose kupita kiasi
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
sijastaafu, hata miaka 40 sijafika. nimetoka kwasababu sipendi mshahara nilianzisha law firm yangu binafsi. upo hapo? nikipata kesi wengi ninao bishana nao tunajuana kwasababu nimefanya nao kazi, wengi wao nawajua ubora wao na udhaifu wao. na tunaheshimiana. tukiwa mahakamani ni vita tu muraa, ila tukitoka tunasalimiana kama ndugu.
Mawakili wa Serikali sometimes huacha liende tu, ni tofauti sana na unapomtetea mtu asiadhibiwe au asilipe tozo kubwa kwenye civil cases
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
amini usiamini, kwenye criminal state attorneys wako bora kuliko mawakili wa kujitegemea. labda kwa mawakili ambao walishawahi kuwa state attorneys. huu ndio ukweli mchungu. mfano pekee angalia application ya makonda aliyoandaa Hekima Mwasipu...hata law school student hawezi kuandaa vile.
Sijui utajificha wapi hiyo application ikipita!
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Umeandika vizuri lakini ulivyomalizia sikubaliani nawe kabisa! Nina sababu nyingi sana sana ila sitaki kuji-expose kupita kiasi
nilipomalizia kwa application ya makonda? ukweli mchungu, siku nikisikia makonda ameshitakiwa na amekuwa convicted, nitachinja jogoo mkubwa nitamla. lakini alitakiwa ashitakiwe na mawakili wa serikali na sio private, kwasababu private prosecutor ana limited opportunity hata kukusanya nyaraka za ushahidi. pia, state attorneys wapo vizuri sana kweney criminal kwasababu hiyo ndio kazi yao hawana nyingine, kila siku wanadili na criiminal hivyo wangeprosecute vizuri sana.

nashauri mawakili wakitakaa kufanya kitu cha criminal, mchukue wakili wa serikali au wakili aliyewahi kupitia serikalini mpeleke hata baa tu akushauri, hata kisirisiri. kulika kujianika.
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
kaka, niwatetee kidogo hata kama mimi ni wakili wa kujitegemea. zamani kabla sijaondoka huko kwenye mishahara nilikuwa wakili wa serikali. Mawakili wa Serikali huwa wanatembelea magereza kama moja ya kazi zao kabisa, hata mimi nilitembelea sana. tulikuwa tunawasiliana tu na Mkuu wa gereza kuwa aandae watu wake sisi tunakuja kukagua gereza kesho yake, hivyo wakili wa serikali, Hakimu Mfawidhi, RCO na OC CID Sometimes tunaenda, tukifika pale vifuatavyo huwa vinafanyika:-

1. Mahabusu wanapata nafasi ya kutulalamikia kama jalada linachelewa upelelezi, wakili wa serikali atajibu.

2. kama kuna malalamiko dhidi ya Mahakama, hakimu yupo pale atajibu.

3.kama kuna malalamiko dhidi ya polisi, rco na oc cid wapo pale watajibu. etc.

hii huwa inasaidia sana na mawakili wasipoenda gerezani hadi wanajela huwa wanalalamika, kwasababu mahabusu na wafungwa huwa wanaweza kuleta hata fujo kule. anachosema chavula ni kweli wala hajitutumui, kuna maeneo mengine at least kile mwezi huwa state attorneys hasa hao wafawidhi kama chavula, wanatembelea magereza tena yote yaliyopo kwenye mkoa, sio kama sisi mawakili wakujitegemea ambao tukienda pale tunaonana na mteja wetu tu, mawakili wa serikali wakienda pale wanaonana na inmate wote wa gerezani na wanasomewa risala kabisa, na kutembelea hadi kwenye mabweni kukagua. na siohivyo tu wana wajibu pia wa kutembelea na kukagua vituo vya polisi tena kwa kushtukiza ili kuona watu gani wamekalishwa rumande ya polisi bila jalada kuletwa kwao ili mtu apelekwe mahakamani.

usilolijua ni kama usiku wa giza.
Unapotosha sana! Hata mawakili wa kujitegemea wana haki hiyo. Wanakutana na wateja wao na wanaongea sana tu. Hawa watu wanategemeana na ndiyo maana kwenye kesi za mauaji inapotokea mshtakiwa hana uwezo wa wakili, Serikali huteua wakili wa kujitegemea akamsimamie huyo mtu kwenye kesi husika. Unachofanya ni kutaka kuwapandisha chati tu hao watu wakati si hakimu wala wao wakipata keshi hutetewa na mawakili wa kujitegemea. USIPOTOSHE kwani ninaamini hata wewe ukipata kesi ya jinai inayokulipa Zaidi lazima utajitutumua ikibidi na kusoma kwa bidii ili ushinde ujijengee jina naupate mahela. USIPOTOSHE andika kilichopo moyoni tu!
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Mawakili wa Serikali sometimes huacha liende tu, ni tofauti sana na unapomtetea mtu asiadhibiwe au asilipe tozo kubwa kwenye civil cases
inategemeana na aina ya kesi mzee, kama kesi ina maslahi au la. kuna baadhi ya kesi huwa wanapewa hata hela ili wasikaze, au wasikate rufaa, kuna mengi huko, tumetoka huko. ila kwenye kesi yenye maslahi ukiona wameamua kukukazia, utajuta.
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
inategemeana na aina ya kesi mzee, kama kesi ina maslahi au la. kuna baadhi ya kesi huwa wanapewa hata hela ili wasikaze, au wasikate rufaa, kuna mengi huko, tumetoka huko. ila kwenye kesi yenye maslahi ukiona wameamua kukukazia, utajuta.
Hamna kitu. Inategemea sana na Jaji husika wala sio mawakili.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Unapotosha sana! Hata mawakili wa kujitegemea wana haki hiyo. Wanakutana na wateja wao na wanaongea sana tu. Hawa watu wanategemeana na ndiyo maana kwenye kesi za mauaji inapotokea mshtakiwa hana uwezo wa wakili, Serikali huteua wakili wa kujitegemea akamsimamie huyo mtu kwenye kesi husika. Unachofanya ni kutaka kuwapandisha chati tu hao watu wakati si hakimu wala wao wakipata keshi hutetewa na mawakili wa kujitegemea. USIPOTOSHE kwani ninaamini hata wewe ukipata kesi ya jinai inayokulipa Zaidi lazima utajitutumua ikibidi na kusoma kwa bidii ili ushinde ujijengee jina naupate mahela. USIPOTOSHE andika kilichopo moyoni tu!
wakili wa kujitegemea akienda pale gerezani anaongea na mteja wake tu. wakili wa serikali anaandaliwa ukumbi au open space wafungwa na mahabusu wote wanakaa chini, pale mbele anakaa yeye, hakimu, rco, na Mkuu wa gereza. niambie kama privilege hizo wakili wa kujitegemea atapata. mimi mwenyewe binafsi nilishawahi kukagua sana magereza na hiyo ni lazima inatolewa report kabisa kupelekwa kwa boss wao dpp kila wakati, umetembelea magereza mara ngapi, umetembelea na kukagua vituo vya polisi gani na lini etc. wapi napotosha sasa? hujui unachoongea, uliza kwa mwanajela yeyote atakuambia.
 
If you argue a lot with a ..... he will bring you to his level and beat you!
 
Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
804
1,000
unawatisha?
Sio kuwatisha,Bali haki ifuatwe
Wao kama mawakili wanalazimishaje njia ovu za Polisi ziwe kweli,Gaidi unamfunga kitambaa usoni toka moshi hadi Dar.Ni sheria au utashi wa mtu.
Magaidi wa ukweli unasafiri nao kwa gari moja tu.
Magaidi unapata mda wakuwanunulia MO energy.
Tuache kulazimisha tuhuma kwa kuwa humpendi mtu fulani
 
EddyC4

Member
Jul 19, 2021
35
125
Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!
Ipo siku Karma itawalipa na ita wakumbusha kuwa mja tupu huondoka tupu. Duniani tunapita tuu.
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
Sio kuwatisha,Bali haki ifuatwe
Wao kama mawakili wanalazimishaje njia ovu za Polisi ziwe kweli,Gaidi unamfunga kitambaa usoni toka moshi hadi Dar.Ni sheria au utashi wa mtu.
Magaidi wa ukweli unasafiri nao kwa gari moja tu.
Magaidi unapata mda wakuwanunulia MO energy.
Tuache kulazimisha tuhuma kwa kuwa humpendi mtu fulani
Hakika!
 
Biggs

JF-Expert Member
May 3, 2014
1,071
2,000
Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!
Ulimbukeni na kujiona wako juu ya kila kitu kumbe njaa tuu zinawasumbua maana hata wao deep down wanajua wanachokifanya ni totally Immoral & Inhuman.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom