Eti "Siye tunaingia Mpaka Ndani Kukagua Mahabusu/Magereza" - Mwenyezi Mungu anawaona Mawakili wa Serikali

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,445
2,000
Kweli kabisa, Unaweza ukapigana vita vyako vizuri ila baadaye watoto na wajukuu wako wakapigwa ile mbaya! Mahita Junior tunamwona, na umri wake yule sijui atastaafuje? Amwombe Mungu sana!
Hakuandaliwa vyema nini😅 au hajapikwa vizuri?
 
Vonix

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
2,855
2,000
Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!
Ni wajivuni tu lakini kimaslahi wako chini sana hushinda kesi kwa nguvu ya dola na hoja zao huwa ni dhaifu sana.
 
Shetemba

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
759
1,000
Ila Leo nimamini wale jamaa wana roho mbaya sana. Mnooooo yaani.
Mtuhukiwa kujieleza tulikuwa tazara na si Central wao wanalazimisha isiwe hivyo na mapolisi. Dah, kweli ishi uyaone ya walimwengu.
Hv pale wangeacha tu Jaji aaamue kama ipo sawa au lah wao wanapoteza nini
IKO siku
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
Nchi hii tuna safari ndefu sana.
Nilitegemea mawakili wa serikali wawe washauri wazuri wa DPP kuwa polisi walizuia ugaidi,uhujumu uchumi hivyo hakuna maslahi kwa taifa kuendelea na kesi huku wanamchelewesha jaji akawajibike na kesi zingine.
Meonee?
 
comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
4,700
2,000
Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!
unawatisha?
 
Mtoto wa Shule

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
8,127

Kila siku kulialia. Kama Gaidi Mbowe na wenzake hawana hatia si Mahakama itasema? Mara utasikia Mahakama so huru. Mara Mahakama inatumiwa na CCM na Serikali. Kama ni hivyo, Kibatala, Mtobesya na wenzake wanafanyaGA nini huko Mahakamani? Si wangeenda kulima matikiti ikajulikana?
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!
kaka, niwatetee kidogo hata kama mimi ni wakili wa kujitegemea. zamani kabla sijaondoka huko kwenye mishahara nilikuwa wakili wa serikali. Mawakili wa Serikali huwa wanatembelea magereza kama moja ya kazi zao kabisa, hata mimi nilitembelea sana. tulikuwa tunawasiliana tu na Mkuu wa gereza kuwa aandae watu wake sisi tunakuja kukagua gereza kesho yake, hivyo wakili wa serikali, Hakimu Mfawidhi, RCO na OC CID Sometimes tunaenda, tukifika pale vifuatavyo huwa vinafanyika:-

1. Mahabusu wanapata nafasi ya kutulalamikia kama jalada linachelewa upelelezi, wakili wa serikali atajibu.

2. kama kuna malalamiko dhidi ya Mahakama, hakimu yupo pale atajibu.

3.kama kuna malalamiko dhidi ya polisi, rco na oc cid wapo pale watajibu. etc.

hii huwa inasaidia sana na mawakili wasipoenda gerezani hadi wanajela huwa wanalalamika, kwasababu mahabusu na wafungwa huwa wanaweza kuleta hata fujo kule. anachosema chavula ni kweli wala hajitutumui, kuna maeneo mengine at least kile mwezi huwa state attorneys hasa hao wafawidhi kama chavula, wanatembelea magereza tena yote yaliyopo kwenye mkoa, sio kama sisi mawakili wakujitegemea ambao tukienda pale tunaonana na mteja wetu tu, mawakili wa serikali wakienda pale wanaonana na inmate wote wa gerezani na wanasomewa risala kabisa, na kutembelea hadi kwenye mabweni kukagua. na siohivyo tu wana wajibu pia wa kutembelea na kukagua vituo vya polisi tena kwa kushtukiza ili kuona watu gani wamekalishwa rumande ya polisi bila jalada kuletwa kwao ili mtu apelekwe mahakamani.

usilolijua ni kama usiku wa giza.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Mbona ziko nyingi
majority ya wanasheria wazuri unaowafahamu, walikuwa mawakili wa serikali, walipopata uzoefu wakaacha kazi wakaenda kufungua ofisi zao binafsi. na kwenye criminal, hakuna expert anayewazidi hao wanasheria au wale waliowahi kufanya huko. ukweli mchungu.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Yaani Mawakili wa Serikali ni kujitutumua kama vile nchi hii ni ya kwao. Leo huyo Chakula sijui Chavula kawaambia Mawakili wa Utetezi baada ya kuonesha kuwa huwa wanaruhusiwa kwenda kuonana na wateja wao Magerezani kuwa eti wao wanaingia ndani na hata kukagua mahabusu lakini sio mawakili binafsi. Yaani yote hiyo ni kuonesha tu kuwa wapo juu ya Sheria na kuwaonesha Mawakili wa Utetezi kuwa "inferior". Yaani hawa watu hawa wamejaa roho mbaya ile mbaya wanasahau kuwa kuna maisha baada ya kesi na hata baada ya kustaafu kazi. Kesi hizi hutunzwa kama precedents - wanakomaa sana sana kwa kitu ambacho hakipo. Hapo hamna ugaidi - Chavula na Kidando kumbeni kuwa kila nafsi itaonja mauti na mtaacha tu watoto na wajukuu huku duniani!
mkuu, uwezo kwenye kesi za criminal hao mawakili wa serikali wapo juu sana kuliko wa kujitegemea na hao wanaoendesha kesi ya mbowe zaidi ya wanne ni viongozi wafawidhi ya mikoa na wilaya. nawajua, niliwapokea kazini baadaye nikawaacha huko serikalini.

ukienda gerezani, treatment anayopata kibatala au ninayopata mimi kama wakili wa kujitegemea na wao ni tofauti, wao ni serikali wanapigiwa hadi saluti.

pia ukitaka kujua tofauti yao na wengine ambao hawajapitia kweney ofisi zao, angalia hii application amefanay Advocate Hekima mwasipu dhidi ya Makonda, nilitamani sana makonda ashitakiwe, lakini mwasipu ameweka application yenye nyaraka zote batili hadi hati ya mashtaka hajui kabisa kuandaa, ni batili, everything pale ni batili . huo ndio ulinganisho mnatakiwa kuufanya.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Ni wajivuni tu lakini kimaslahi wako chini sana hushinda kesi kwa nguvu ya dola na hoja zao huwa ni dhaifu sana.
amini usiamini, kwenye criminal state attorneys wako bora kuliko mawakili wa kujitegemea. labda kwa mawakili ambao walishawahi kuwa state attorneys. huu ndio ukweli mchungu. mfano pekee angalia application ya makonda aliyoandaa Hekima Mwasipu...hata law school student hawezi kuandaa vile.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,067
2,000
Hata Mimi ningependa kuwajua hawa nyoka,please mwenye picha
hata ukiwajua huna uwezo kuwafanya chochote ndugu yangu. nenda nyumbani kwako kale chakula ukakojoe ulale. usijiingize kwenye matatizi wakati huna wa kukutetea.
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
mkuu, uwezo kwenye kesi za criminal hao mawakili wa serikali wapo juu sana kuliko wa kujitegemea na hao wanaoendesha kesi ya mbowe zaidi ya wanne ni viongozi wafawidhi ya mikoa na wilaya. nawajua, niliwapokea kazini baadaye nikawaacha huko serikalini.

ukienda gerezani, treatment anayopata kibatala au ninayopata mimi kama wakili wa kujitegemea na wao ni tofauti, wao ni serikali wanapigiwa hadi saluti.

pia ukitaka kujua tofauti yao na wengine ambao hawajapitia kweney ofisi zao, angalia hii application amefanay Advocate Hekima mwasipu dhidi ya Makonda, nilitamani sana makonda ashitakiwe, lakini mwasipu ameweka application yenye nyaraka zote batili hadi hati ya mashtaka hajui kabisa kuandaa, ni batili, everything pale ni batili . huo ndio ulinganisho mnatakiwa kuufanya.
Du! Kama wewe mwenyewe unakiri umetoka huko umewaacha sasa sijui ulistaafu au imekuwaje mpaka uko private! Sasa kwa maana hiyo ukipata kesi ukabishane nao utaiacha?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom