Elections 2010 Eti Sitta ataka uspika, asema anafaa, Kweli ataliweza hilli Bungo La 10

Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,173
708
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Tanzania lililomaliza muda wake, Samuel Sitta, ana hamu ya kuliongoza Bunge lijalo hivyo anatarajia kujaza fomu kesho kukiomba Chama Cha Maja sorry Mapinduzi (CCM), kimpitishe agombee uspika.

Kutoka Habari leo la leo
 
anatumix na ujuha wake wa ulafi wa madaraka. tunasubiri matokeo ya urais yatangazwe yeye anatutoa huko
 
Hafai kuongoza bunge lijalo kwani ni kigeugeu sana. Watanzania hivi sasa hatuhitaji spika substandard. Leo anaonekana anawatetea wanyonge na kesho anageuka ghafla na kuanza kuwatetea mafisadi. Yeye abaki kuwa mbunge wa kawaida. Tena huu ni ushauri unaolenga kulinda heshima yake
kwani bunge la safari hii litakuwa moto. Hakutakuwa na porojo porojo.
 
Hafai kabisa - kwa jinsi alivyozima issues kama RichMonduli na Meremeta na kutumiwa na JK. Alianza vizuri lakini amemalizia vibaya.
 
Ni afadhali Sitta, angalau ni zimwi likujualo, kuliko Kinana aliyeandaliwa na CCM kama asante kwa kazi nzuri ya Mchakachuo.
Chedama pia wamshauri Dr. Slaa atupe karata yake kwenye uspika, japo idadi ya wapinzani ni ndogo, naamini Sauti ya Mungu, itawaingia baadhi ya WanaCCM kuacha unafiki na kumchagua Dr. Slaa kulinyoosha bunge tupate katiba mpya.
 
Mkuu Pasco, kwa bandiko hili ni wazi umeyakubali matokeo ya kura ya uraisi?
 
Vita ya Uspika ndani ya CCM ni mwendelezoo mzuri wa kuwatoa katika uongozi wa umma..Kuhusu DR SLAA kugombea uspika bado sijaaafikii sana..
 
Kuna taarifa kwamba, baada ya kuona Lowassa na Chenge hawatafaa kupewa Uspika wa Bunge badala ya Sitta, mkakati mpya ni kumuongeza Kinana katika list hiyo hapo juu pamoja na msindikizaji, Philip Marmo, aliyepoteza Ubunge. Ndio maana Kinana na Makamba wamefanya vikao na waandishi kwa siku moja lakini maeneo tofauti, wote wakionyesha CCM imeshashinda na sasa wanatafuta Spika. Kinana alitamba CCM kupata ushindi wakati Makamba alitangaza kutolewa fomu za Uspika. Sitta ajiangalie, hawa jamaa hawajamsamehe, bado wana usongo naye sana, asingerudi nyuma.
 
Kweli tumekwisha, huyo msomali apewe uspika? Si unaona nchi yetu anavyoigeuza somalia? Hakika usomali hautamwisha kwenye damu hata kama amekaa tz miaka 40. Yeye ndiye kampeni meneja wa ccm, hivyo ndiye mwenye mipango yote ya ushindi wa ccm. Mipango ya uchakachuaji, kupiga mabomu yote ni yake. Hakika sasa tumegeuka somalia.
Mungu waTZ tumekukosea nini?
 
Nyie waacheni tu maana hawafikirii kuwa TZ ya sasa sio ya october 31 tena....... Nimeshuhudia mengi ila naomba wampe. I would like them to keep Dr. Slaa more busy.
 
Maamuzi ya CCM bwana huwa yananikwaza ,wanaweza ata wakampa Lowasa
 
hii Tanzania yetu na katiba ya zamani ndiyo inatuletea matatizo, rais anamchagua speaker wa bunge... hii lazima ifanyiwe kazi kuwe na kura wabunge wamchague speaker bila kujali chama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom