Elections 2010 Eti Sitta ataka uspika, asema anafaa, Kweli ataliweza hilli Bungo La 10

Sidhani kama hizi habari ni za kweli kwa sababu moja ya matunda ya uchaguzi huu ni umeidhoofisha hiyo Kamati Kuu ya CCM na hivi sasa haina jeuri tena chini ya uenyekiti wake wa JK kucheza na masuala ya ufisadi...............hata dola ina mipaka ya kuwabeba....usifikiri uchaguzi ujao CCM itabebwa na NEC na Idara ya usalama wa taifa na kutulazimisha mrithi wa JK atutawale kwa mabavu kama JK alivyotudhulumu haki yatu ya kimsingi ya kujichagulia viongozi wetu...........................
 
Wakuu habari za uhakika zinasema mzee Samweli Sitta hatapitishwa vikao Vya juu CCM kuwa mgombea wao wa u spika. chanzo cha habari cha kuaminika kabisa ni kwamba Lowassa na Rostam wamefanya mpango ili sitta apingwe hata na mama Makinda ambae amewageuka wenzake akina SITTA.

Mama huyu amegombea kwa shinikizo na kwa kufuata maelekezo ya akina Rostam ili Spika aanguke halafu bunge lipitie tena ile richmond na kumsafisha Lowassa. Lowassa pia atagombe urais mwaka 2015 baada ya kusafishwa na bunge la spika ama chenge ama Makinda.

Heshima kwako Somoche,

Mbona bandiko lako limekaa kikampeni au wewe ni mpiga debe wa Sitta ?.Mkuu Mama Anna Makinda ana haki ya kugombea Uspika ameshapata uzoefu mkubwa kama naibu spika sioni sababu za msingi zitakazomzuia kupanda ngazi.Isitoshe bunge letu litakuwa na wanawake wengi this time pengine huo ni mtaji mkubwa wa Makinda.

Sidhani kama CCM iliyopelekwa puta kwenye uchaguzi itakubali Chenge agombee uspika hii itakuwa ni sawa na kuwakejeli waTanzania.Kikwete kasema wazi wataangalia ni sababu zipi zilizookosesha CCM kura nyingi bila shaka anajua wazi kitendo cha kuwakumbatia wanaCCM wachafu ni moja ya sababu kubwa iliyopunguza kura zake na CCM kwaujumla.
 
Picha hii inafanana na kama vile kweli..Sitta ni fisadi anayeuma na kupuliza hivyo angalau wakimchagua watakuwa wamewapooza kundi la wapiganaji na bado pia watakuwa na control naye kwa mambo kadhaa wa kadhaa, Makinda yeye ni rahisi kuburutwa na mafisadi kwani tulishamuona walivyotaka kuiteka na kuimaliza inshu ya Richmond fastafasta wakati Six akiwa safarini US...lakuvunda.....yote yawezekana

Ila kwa hapo juu penye red mbona sio kitu kigeni na ilishajulikana na ikaongelewa sana hapa JF tena zamani sana na wengine kama Mkjj wakaomba kama kweli EL anaamini kuwa hakukuwa na ufisadi basi aende mahakamani akajisafishie huko na sio bungeni tena
 
Gama nitajie jina la hawa wagombea waliojitokeza ambaye anampiku Mheshimiwa Samweli Sitta................jibu ni kuwa hayupo..............

Pamoja na kujiita ni mzee wa "standard" mhe. Sita hakuonyesha attribute hiyo kwa vitendo. Mjadala wa Richmond alilazimisha uishe kienyejienyeji tu huku watanzania wengi wakiwa na kiu ya kujua hatua madhubuti zitakazochukuliwa na serikali kuwawajibisha wahusika. Kwa hilo tu, mimi binafsi simpendi kwani ameonyesha kuwa maamuzi yake mengi yanategemea interest yake na siyo ya jamii. Watanzania wapo wengi tu wanaoweza kushika nafasi hiyo na nchi ikasonga mbele bila wasiwasi.
 
CHENGE: NATAKA USPIKA ILI NITIBU MAJERAHA YA WENGINE BUNGENI

Mh. Andrew Chenge, Mbunge mteule wa Jimbo la Bariadi Mashariki na Mwanasheria mkuu wa zamani wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga SeaView leo, ambapo amesema ana nia ya kugombea Uspika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliongeza kuwa, ameamua kugombea Uspika wa Bunge ili aweze kusimamia na kutibu majeraha ambayo yamesababishwa na uongozi uliopita kwa wengine
 
for the first time in the past few weeks, nimesoma thread yenye arguments zenye lengo la kujenga. big thanks to mtanzania, rutashubanuma, gosbertgoodluck and all who contributed to this post.

maana nilishachoka kusoma malumbano yasiyo na mising yeyote.
cheers guys
 
CHENGE: NATAKA USPIKA ILI NITIBU MAJERAHA YA WENGINE BUNGENI

Mh. Andrew Chenge, Mbunge mteule wa Jimbo la Bariadi Mashariki na Mwanasheria mkuu wa zamani wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga SeaView leo, ambapo amesema ana nia ya kugombea Uspika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliongeza kuwa, ameamua kugombea Uspika wa Bunge ili aweze kusimamia na kutibu majeraha ambayo yamesababishwa na uongozi uliopita kwa wengine

Refer Red:

Ni nini huyu bwana anachokiita ni majeraha?

Mtu yeyote mwenye akili timamu...anatambua kuwa Haki na kweli ilifanyika.... That is all!
 
Mimi naomba wampe uspika Chenge na uwaziri mkuu wampe Lowasa maana ndiyo itakuwa mwisho wao (CCM)..
hapo umesema vyema.huo ndo utakuwa mwisho wa ccm. sipati picha wakikaa mle mjengoni, wakigeuka huku wanamwona Mrema, wakienda huku wanamwona Mbowe, huku yuko zito, huku yuko lema, mara nyerere, watu wenye magwanda wamejaaa, mara mdee, mnyika ndo anaenda kumaliza hasira zake za kuibiwa kura mwaka 2005, patakuwa hapatoshi. bunge la mwaka huu tunatakiwa kumshukuru Mungu kwakweli, hata kama wameiba kura za urais na kupanga matokeo ya majimbo kadhaa, rungu hili hili tulilopewa tunatakiw akulitumia.
 
Mimi nadhani sitta bado ni kiongozi mzuri. Ni spika aliyeruhusu serikali ya chama chake kukosolewa bungeni bila kujali kama serikali hiyo itapoteza imani kutoka kwa wanachi. Bila sitta siajabu madudu ya serikali iliyopita tusingeyajua. Bunge lililopita limejenga imani kwa wanachi kuwa linaweza kusimamia utendaji wa serikali. Kimsingi nimesoma kwenye magazeti majina ya watu waliochukua fomu za uspika kupitia ccm sijaoni kati yao mwenye uwezo aliouonyesha sitta kwenye bunge lililomaliza muda wake. Nakubali wapo watazania wengine wenye uwezo wa kuwa spika, lakini spika atakayewekwa kwa maslahi ya kuhakikisha serikali haikosolewi bungeni ni hatari kuliko raisi aliyeingia madarakani kwa kura za kuchakachuliwa.
 
Heshima kwako Somoche,

Mbona bandiko lako limekaa kikampeni au wewe ni mpiga debe wa Sitta ?.Mkuu Mama Anna Makinda ana haki ya kugombea Uspika ameshapata uzoefu mkubwa kama naibu spika sioni sababu za msingi zitakazomzuia kupanda ngazi.Isitoshe bunge letu litakuwa na wanawake wengi this time pengine huo ni mtaji mkubwa wa Makinda.

Sidhani kama CCM iliyopelekwa puta kwenye uchaguzi itakubali Chenge agombee uspika hii itakuwa ni sawa na kuwakejeli waTanzania.Kikwete kasema wazi wataangalia ni sababu zipi zilizookosesha CCM kura nyingi bila shaka anajua wazi kitendo cha kuwakumbatia wanaCCM wachafu ni moja ya sababu kubwa iliyopunguza kura zake na CCM kwaujumla.

JK si mkweli maana alikuwa Kilimanjaro do you remember what he said wakati anamuombea Mramba kura ?Yale maneno leo hawezi kugeuka akasema vinginevyo na upungufu wa kura .
 
je inawezekana anaitaka hiyo nafasi ili aweze kulipizia kisasi kwa yote,hata kwa dawa nadhani hawezi kuwa spika wa Bunge..
Kikwete tunamwona tu kama mjinga lakini ukweli ni kwamba kipindi hiki cha pili ni lazima atakuwa mkali mno wala hatambeba mtu yeyote maana anajua Uraisi tayari kesha ukwaa.Kwa hiyo si ajabu mafisadi wengine wengi tu wakaendelea kuburuzwa mahakamani,yetu macho..na kama hata lifanya hilo basi wahesabu mwisho wa utawala wa CCM 2015:smile-big::bowl::rip:
CHENGE: NATAKA USPIKA ILI NITIBU MAJERAHA YA WENGINE BUNGENI

Mh. Andrew Chenge, Mbunge mteule wa Jimbo la Bariadi Mashariki na Mwanasheria mkuu wa zamani wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga SeaView leo, ambapo amesema ana nia ya kugombea Uspika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliongeza kuwa, ameamua kugombea Uspika wa Bunge ili aweze kusimamia na kutibu majeraha ambayo yamesababishwa na uongozi uliopita kwa wengine
 
Sasa kama Chenge anasema atayatibu majeraha si inaeleweka,kwani fisadi si anautetea ufisadi.kwa hiyo yeye anapingana na vita ya mafisadi.Litakuwa kosa kubwa sana kumpitisha yule.CC inaweza kurubuniwa si unajua zuzu JK alimpa nafasi RA kuingia CC,hivyo hapo ni kununuana tu.Jk simtofautishi na wale machifu wa zamani waliopewa vipande vya nguo wakakabidhi nchi kwa wakoloni.
 
Sura mpya ya Chenge? Sina matatizo na wagombea wengine wote waliochukua fomu, mimi nina tatizo na Chenge na km sura mpya ni Chenge basi CCM itakuwa haitutendei haki.

Unategemea CCM ikupe haki! Je ilikufanyia haki kwenye uchaguzi? Chenge ndiyo spika wako na Lowasa waziri mkuu. Hii ndiyo haki CCM itakayokupa
 
Nakuunga mkono crashwise,naomba chenge ashinde uspika na lowassa uwaziri mkuu..hapo itakuwa ni kazi rahisi tu kwa chadema kuchukua dola 2015!
 
Kaka Ngongo nadhani umekuwa hufuatilii myeneno ya viongozi wajuu wa CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao Bwana JK....kitu nachoweza kukwambia kamati kuu ya CCM ikiongozwa na huyo bwana ni HOSTAGE wa kundi la mafisadi wa chache..na usitegemee wana ubavu wa kuwapinga.....pliz reffer kauli za huyu Bosss( not leader ) kipindi cha kampeni akiwakampeni hao mafisadi uliosema atawatema.....
so usitegemee CCM inaubavu wa kuwazuia hao mafisadi, so sitashangaa TETESI hizi zikiwa ni za kweli....
.
:doh:

:bowl::bowl:CCM na MAFISADI DAMU DAMU-MPAKA KIFO KIWATENGANISHE
:bowl::bowl:
 
Leo TBC1 imemwonyesha mama Anna Abdallah mwanasiasa mkongwe ambaye bado ana hamu ya kurudi bungeni na kuwa spika akilalama dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiwatupia madongo wapinzani wa Samweli Sitta katika nafasi ya uspika...........................

Akionekana ni mwenye jazba, Mama Anna Abdallah alihoji ni demokrasia ipi hiyo inayohalalisha kuondoa ushindani kwenye nafasi nzito kama hiyo ya Uspika na akawataka wote wanaowabeza wapinzani wa Sitta kuacha mara moja kuingilia haki yao ya kidemokrasia kushiriki katika kugombea nafasi yoyote ile iliyowazi................

Vile vile alitoa kauli ambayo inaweza kutafsiriwa kuwa ni ya kutoa vitisho dhidi ya wote wenye kilimilimi dhidi yao kuwa hoja hizo tajwa zinalenga kuleta mifarakano ndani ya CCM..............Lengo hapo ni kuwafanya wachambuzi wa siasa kuhofu kuonekana ni chanzo cha mifarakano ndani ya chama hicho ambacho hivi karibuni kimejivunia umaarufu wa kuwa pango la mafisadi........

Hata hivyo uchunguzi wangu nilioufanya wa kina umebaini ya kuwa Mama Anna Abdallah siyo tishio kwa Mheshimiwa Samwel Sitta ila anatumika kumpunguzia kura na kumwezesha mwana-CCM mwingine kuibuka kidedea.............na hivyo kupunguza kasi ya vita dhidi ya ufisadi ndani ya hili jumba la malumbano ya kihoja............kweli kabisa ni KIGUMU CHAMA CHA MAFISADI.................
 
Hivi vibibi vya dizaini hii ni nini kipya ambacho vinafikiri vinaweza kufanya? Haviendi kulea wajukuu tu... Tunataka mawazo mapya bwana!
 
Huyu Mama nafikiri haijui Demokrasia vizuri, kama angekuwa anaijua yeye pamoja na CCM wasingeweanyima wananchi demakrasia yao ya kuchagua Rais, nafasi ambayo ni nyeti sana kuliko zote, kwa kuchakachua inaonyesha ni kiasi gani demokrasia isivyoheshimiwa. Na ni wazi kuwa anasingizia demokrasia lakini ndani yake ni mpango wa kumg'oa Sitta. HATUDANGANYIKI
 
7th November 2010

headline_bullet.jpg
Jina lake kuishia kamati kuu
headline_bullet.jpg
Sitta awajibu: Haki itanibeba

Baada ya kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukivuruga na kusababisha mivutano ya kimakundi ndani ya chama hicho na kukigharimu kupoteza viti vingi vya ubunge wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita, imeibuka vita nyingine mpya ya kuwania Uspika wa Jamhuri ya Muungano, hali ambayo inaelezwa itazidi kukiweka pabaya.
Vita hiyo inaelezwa kuendeshwa na kundi la watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, ambalo limeanza mikakati mizito kuhakikisha linamwangusha Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta, ili asiweze kupitishwa na chama kuwania nafasi hiyo kwa mara ya pili..
Sitta ambaye alikuwa ni Spika wa Bunge lililopita, alionyesha msimamo mkali katika bunge hilo la tisa dhidi ya mafisadi, hali ambayo ilimjengea maadui wengi wa kisiasa, ambao wameapa kuhakikisha kuwa hakamati tena nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Sitta, Mbunge Mteule wa Jimbo la Urambo Mashariki, tayari ameshachukua fomu za kutaka kuwania tena nafasi hiyo kwa mara ya pili kupitia CCM, huku akikabiliwa na upinzani kutoka kwa aliyekuwa Naibu wake, Anna Makinda, Mbunge Mteule wa Bariadi Andrew Chenge, Mbunge Mteule wa Kongwa, Job Ndugai, Mwanasiasa mkongwe, Kate Kamba na Mbunge Mteule Viti Maalum (CCM) Anna Abdallah.
Wengine ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Stephen Deya, Mjumbe wa Baraza la Vijana mkoa wa Pwani, Mohamed Nyundo, Luteni Mstaafu Benedict Lukwembe na Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza, Salum Kingulilo.
Wakati joto la kindumbwe ndumbwe hicho likizidi kuongezeka, duru za kisiasa ndani na nje ya CCM zimedokeza kwamba chama hicho tawala kwa mara nyingine kitaingia katika hatari ya mpasuko mkubwa unaotokana na vita ya makundi yanayotokana na kashfa ya mkataba wa kifisadi wa Richmond.
Vita hiyo mpya inaelezwa inayahusu makundi pinzani ndani ya CCM ambayo kila moja linajaribu kujiwekea mazingira ya ushindi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hali hiyo kwa mara nyingine inakiweka chama hicho njiapanda, baada ya hivi karibuni kuadhibiwa na wananchi katika majimbo kwa kupoteza wabunge wengi na mgombea wake wa Urais, Jakaya Kikwete, kupata ushindi wa jasho kutokana na chama kugubikwa na makundi yanayohasimiana.
Habari ambazo NIPASHE Jumapili imezipata, zinasema kundi la watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, linatumia kila aina ya mbinu kuhakikisha jina la Sitta linaishia Kamati Kuu (CC) kutokana na kuhofu linaweza kupenya na kuwasulubu tena bungeni endapo atakuwa Spika.
Genge hilo linalodaiwa kuongozwa na watu wenye fedha chafu, limekuwa likimtumia kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa CCM (jina linahifadhiwa), kuwashawishi wanachama wakongwe na wenye nguvu ndani ya chama hicho ili wagombee, lakini lengo mwisho wa siku waanguke na Sitta kubakia mgombea wao wanayemtaka.
Inaelezwa kuwa mbinu inayotumika ni kuwashawishi baadhi ya wanachama wakongwe kujitokeza kuwania Uspika, lakini baadaye majina yao yatakatwa CC pamoja na la Sitta, ili kuonyesha kuwa kulikuwa hakuna njama zozote za kumhujumu Sitta, utetezi ukiwa hata vigogo wengine wazito nao pia wameanguka.
NIPASHE Jumapili, lilipomuuliza Sitta jana kama anafahamu kuwepo kwa mkakati huo, alikiri kuufahamu na kueleza kuwa unatekelezwa kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa CCM wasio waadilifu.
"Nalifahamu vizuri sana jambo hilo. Ni mkakati maalum ambao umeandaliwa lakini kwa bahati mbaya unashirikisha watendaji wakuu ndani ya CCM", alisema.
Alifafanua kuwa mpango uliopo ni kuweka majina mengi ya watu watakaowania uspika, lakini baadaye majina hayo yatakatwa likiwemo lake, ili kuonyesha kuwa hata vigogo wengine waliokuwa wakiwania majina yao yamekatwa hivyo hakuna uonevu.
Hata hivyo, alisema atazishinda njama hizo ambazo ameziita kuwa ni ovu, kwani wananchi wanajua utendaji na uadilifu wake katika kulitumikia taifa kwa moyo wake wote.
"Nimepata habari baadhi ya wagombea wenzangu wanajinadi kuwa wameamua kujitosa kuwania uspika baada ya kuelezwa kuwa jina langu litakatwa. Mimi nasema historia inaonyesha magenge ya uhalifu siku zote hayashindi na uamuzi wa mwisho utakuwa ni wa wananchi, wafanye wafanyavyo lakini hawawezi kuishinda nguvu ya wananchi na mwisho wa siku wataumbuka", aliongeza kusema.
Sitta, alisema wabaya wake wamekuwa wakimchafua kuwa ndiye amesababisha nyufa ndani ya CCM kutokana na kuruhusu mijadala huru ndani ya bunge.
"Nazushiwa na kuhusishwa na kuharibika kwa kila kitu kuanzia Mamlaka ya Makao Makuu Dodoma (CDA) wakati nikiiongoza, hivi kweli ningekuwa mtu mbaya baada ya CDA ningeteuliwa kuwa Waziri wa Sheria?" alihoji.
Alisema ameamua kuingia katika kinyang'anyiro hicho akiamini kuwa haki itatendeka, hivyo hahofii njama zinazofanywa ambazo zipo nje ya utaratibu halali wa kumpata mgombea.
Hata hivyo, duru zaidi za kisiasa zinasema, mkakati huo pia unasukwa Zanzibar na kusimamiwa na mmoja wa mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Habari hizo zinasema, katika mkutano uliofanyika visiwani humo juzi, mmoja wa vigogo wa CCM, aliweka bayana msimamo huo wa mafisadi akisema Sitta ni mtu hatari hapaswi kurudi.
Mkakati huo unasimamiwa na vigogo watatu, akiwemo waziri mmoja mwanamke, ambao wameapa jina la Sitta halitapita Kamati Kuu.
Tayari waziri huyo mwanamke ambaye mara nyingi amekuwa akitoa kauli tata katika suala la ufisadi na kuzusha mijadala mizito, amekuwa akitamba kwa kuomba ushawishi kuhakikisha wanamshughulikia Sitta.
Tayari kuna mpango wa kumshawishi mwanasiasa mwingine mkongwe kutoka Kanda ya Ziwa ambaye ameshindwa katika kinyang'anyiro cha ubunge Jumapili iliyopita, kuhakikisha naye anachukua fomu na wakati wowote kuanzia kesho kama atakuwa amekubali atafanya hivyo.
Imebainika kwamba, hata mmoja wa waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ambaye ni mwanasiasa mkongwe, alipigiwa simu na kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa CCM, akiwa mkoani kwake ambako alikuwa akikarabati nyumba yake akilazimishwa kuchukua fomu hiyo.
Vyanzo vyetu hivyo vya habari viliongeza kwamba, awali mwanasiasa huyo alijenga hoja kwamba hawezi, lakini kiongozi huyo wa CCM alimwambia alikuwa akipingana na msimamo wa chama na fomu hiyo ilikuwa tayari.
Mbunge Mteule wa Peramiho, Jenista Mhagama, yeye amejitosa kuwania nafasi ya Naibu Spika iliyokuwa ikishikiliwa na Makinda bunge lililopita.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILi
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom