Eti serikali kupiga marufuku uuzwaji nje malighafi?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375
2,000
Labda mimi sijaelewa lakini nimesikia eti serikali inafikiria kupiga marufuku uuzwaji nje malighafi? nashindwa kuelewa kama kweli serikali inafikiria hili.

Hii itakuwa ni "mistake" kubwa sana na ni maamuzi yasiyo na tija bali kuwaongezea watanzania umasikini. sio swala la mtu kukaa chini na kusema malighafi zikiuzwa nje watanzania wanakosa ajira hivyo jawabu ni kupiga marufuku malighafi kuuzwa nje. nashindwa kusema hii ni fikra ya aina gani maana inaweza kutafsirika nimetukana.

ki msingi serikali inatakiwa kufikiri kibiashara. bidhaa zinazokwenda nje zinafuata soko lililopo nje. kama kuna mnunuzi ananunua kahawa ghafi huwezi kupakia kwenye makopo ukampelekea akanunua. na kama soko tunaloweza kulipata la nje kwa sasa ni la kahawa ghafi basi ukipiga marufuku uuzwaji wa kahawa ghafi nje unaua kilimo cha kahawa kwa wakati huo maana waliokuwa wakinunua kahawa ghafi yenu hawaji kuanzisha kiwanda kwenu bali watahamia kwingine wanakoweza kupata kahawa ghafi.

watanzania tuna matatizo makubwa sana katika kupanga. wataalamu wanaopanga mipango ya maendeleo wanatakiwa kutoa "detailled development plans". tunatumia wahumi wanatoa skeleton za mipango ya maendeleo nadhani ndio chanzo cha haya.

tuzuie sukari kutoka nje basi serikali inakimbilia kupiga marufuku bila kuandaa programu ya uzalishaji wa ndani kutosheleza mahitaji na matokeo yake ni kuleta tatizo la sukari.

sasa bado tuko kwenye mambo yaleyale eti kupiga marufuku uuzwaji malighafi nje? ni kweli ili tupige hatua za maendeleo tunatakiwa kuuza nje bidhaa si malighafi lakini haya ni mabadailiko yanayotakiwa kufanyika kibiashara. tafuta masoko ya kuuza finished goods nje na kuweka mazingira ya watu kuzalishia hapa na kupeleka nje.

lakini itakuwa ni makosa makubwa serikali kupiga marufuku uuzwaji wa malighafi nje ikidhani hiyo ndio njia ya kuhamasisha ujenzi wa viwanda hapa kwa maana biashara haiendi hivyo. ukiwazuia waliokuwa wakinunua kwako watanunua kutoka nchi nyingine na waliokuwa wakiuza huko inawezekana hawana soko la finished goods.

mambo yote yanatakiwa yaendelee sambamba, kujenga viwanda ndani na kuendelea kuuza mazao ghafi nje kwani itatoa soko pana zaidi kwa kilimo. pale tu itakapobainika kuwa ndani kuna kiwanda kinakosa malighafi kutokana na malighafi hizo kupelekwa nje ndio serikali wala isipige marufuku bali icheze na viwango vya kodi kutoa profit margin kwa wanaouza ndani kupata faida zaidi.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Viwanda tunavyo 52,000 according to Mwijage...
Sehemu zote za kufyatulia matofali ni VIWANDA.
Usiwe na wasiwasi Mkuu.
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,392
2,000
Magufi akiweza kupiga marufuku uuzwaji wa malighafi nje na akatekeleza hilo kwa 100% hata mimi nitamuunga mkono siku hiyo hiyo maana hii itakuwa na + impact kwenye uchumi provided ameweka mazingira, miundo mbinu na technilojia ya kufanikisha hilo
 
Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,289
2,000
Labda mimi sijaelewa lakini nimesikia eti serikali inafikiria kupiga marufuku uuzwaji nje malighafi? nashindwa kuelewa kama kweli serikali inafikiria hili.

Hii itakuwa ni "mistake" kubwa sana na ni maamuzi yasiyo na tija bali kuwaongezea watanzania umasikini. sio swala la mtu kukaa chini na kusema malighafi zikiuzwa nje watanzania wanakosa ajira hivyo jawabu ni kupiga marufuku malighafi kuuzwa nje. nashindwa kusema hii ni fikra ya aina gani maana inaweza kutafsirika nimetukana.

ki msingi serikali inatakiwa kufikiri kibiashara. bidhaa zinazokwenda nje zinafuata soko lililopo nje. kama kuna mnunuzi ananunua kahawa ghafi huwezi kupakia kwenye makopo ukampelekea akanunua. na kama soko tunaloweza kulipata la nje kwa sasa ni la kahawa ghafi basi ukipiga marufuku uuzwaji wa kahawa ghafi nje unaua kilimo cha kahawa kwa wakati huo maana waliokuwa wakinunua kahawa ghafi yenu hawaji kuanzisha kiwanda kwenu bali watahamia kwingine wanakoweza kupata kahawa ghafi.

watanzania tuna matatizo makubwa sana katika kupanga. wataalamu wanaopanga mipango ya maendeleo wanatakiwa kutoa "detailled development plans". tunatumia wahumi wanatoa skeleton za mipango ya maendeleo nadhani ndio chanzo cha haya.

tuzuie sukari kutoka nje basi serikali inakimbilia kupiga marufuku bila kuandaa programu ya uzalishaji wa ndani kutosheleza mahitaji na matokeo yake ni kuleta tatizo la sukari.

sasa bado tuko kwenye mambo yaleyale eti kupiga marufuku uuzwaji malighafi nje? ni kweli ili tupige hatua za maendeleo tunatakiwa kuuza nje bidhaa si malighafi lakini haya ni mabadailiko yanayotakiwa kufanyika kibiashara. tafuta masoko ya kuuza finished goods nje na kuweka mazingira ya watu kuzalishia hapa na kupeleka nje.

lakini itakuwa ni makosa makubwa serikali kupiga marufuku uuzwaji wa malighafi nje ikidhani hiyo ndio njia ya kuhamasisha ujenzi wa viwanda hapa kwa maana biashara haiendi hivyo. ukiwazuia waliokuwa wakinunua kwako watanunua kutoka nchi nyingine na waliokuwa wakiuza huko inawezekana hawana soko la finished goods.

mambo yote yanatakiwa yaendelee sambamba, kujenga viwanda ndani na kuendelea kuuza mazao ghafi nje kwani itatoa soko pana zaidi kwa kilimo. pale tu itakapobainika kuwa ndani kuna kiwanda kinakosa malighafi kutokana na malighafi hizo kupelekwa nje ndio serikali wala isipige marufuku bali icheze na viwango vya kodi kutoa profit margin kwa wanaouza ndani kupata faida zaidi.
Elimu yako ni darasa la ngapi mkuu? Au ulisoma kama Mbowe?
Wazungu waliosonga mbele kimaendeleo hawauzi malighafi na wewe watetea Tz iuze malighafi nje, je tutajitegemea lini? Fikiria in deep usifikirie juu juu kama akina Lema au Akina Malisa kisha unaibuka tu kama unatoka chooni.
Kuuza malighafi unapoteza pesa nyingi sana mfano ukiuza mpunga utapoteza pumba 2, ukiuza Magogo utapoteza wood scraps ambazo pia zina KAZI zake. Ukiuza ng'ombe utapoteza ngozi, pembe, mifupa,mbolea nk.
 
Tatizo letu tanzania ni kuwa na wataalamu waliojaza theory kichwani hakuna practical na hiyo inawafanya kuwa ignorant mbali na kuwa na vyeti vikubwa.

unajiita mtaalamu unasema eti serikali ipige marufuku kuuza malighafi nje?

tutapata faida yes kwa kuuza finished goods nje lakini mapinduzi haya ni ya kujenga viwanda vitake over uuzaji wa malighafi nje.

ki msingi wataalamu wa tanzania tunachokifanya ni "gambling" kucheza kamali kwenye maisha ya watu.

biashara ni faida nani asiyetaka kama kuna soko la kuuza bidhaa zilizo kwenye makopo nje akapata faida zaidi anganganie kuuza mali ghafi?

sisi ni vipofu tuliojaa theory tu hatuwezi kuona kesho.

mtu akitazama kitabu kinasema kuuza nje processed goods basi anadhani ukitunga sheria kusema bidhaa zinazouzwa nje ziwe processed unapata faida?????

kama huna soko la kahawa iliyosindikwa nje leo hii ukipiga marufuku kuuza kahawa ghafi nje aoutomatically unaua kilimo cha kahawa nchini. hakuna mkulima ataendelea kulima kahawa, kuhudumia mashamba yao kwa soko finyu la ndani akisubiri eti soko la nje la kahawa zilizosindikwa likipatikana ndio wapate faida.

maisha ya wakulima wa leo wa leo wanaotegemea kilimo cha kahawa unayaweka wapi?

kinachoweza kufanyika ni kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kusindika kahawa hapa hapa na kuvipa motisha kwa bidhaa zinazouzwa nje. pale tu unapokuwa umejenga uwezo wa kuprocess mazao yote ya ndani ndipo labda unaweza kuzuia kuuza ghafi nje lakini bado kwa true leader bado atasema kama wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kuhudumia masoko ya ndani na ziada ikauzwa nje ni upuuzi kuzuia soko hilo.

umasikini wa kwanza unatokana na fikra.

sisi ni wazembe wa kufikiri, mtu akiwaza jambo moja katika jambo lenye mambo kumi basi anaridhika na kukimbia kutekeleza na akikutana na tatizo ndio anarudi kuwaza.

makosa hayo hayo tumeyafanya kwenye sukari, badala ya kupanga mpango wa kuongeza uzalishaji wa sukari wa ndani kutosheleza soko kwa kuwashirikisha wazalishaji na tukajua baada ya miaka miwili uwezo wetu wa kuzalisha utakuwa 80% ya mahitaji hivyo vibali vitatolewa kwa 20% kujazia , baada ya miaka 5 uzalishaji wetu utakuwa 100% kwa wakati ndio ndio tutazuia kabisa uingizaji wa sukari.

lakini kwa kusikiliza vipofu wanaokwenda kuangalia kuzuia kunasaidia viwanda vya ndani huku hawaoni uzalishaji wa sasa ukoje wala mipango ya kuongeza uzalishaji ikoje wanasiasa walikurupuka na kuzuia.

tukifanya maamuzi kama hayo kwa wakulima hakutatokea kaosi ya kama ya sukari kufanya serikali ije na mipango ya dharura bali kilimo kitakufa kabisa maana wakulima wataacha kuzalisha na kuanzisha viwanda vyenyewe itakuwa ndoto.
 
ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,375
2,000
kafanye biashara kwanza uachane na kazi ya kuajiriwa utaelewa ninachokisema.

wafanyabiashara wa kaliakooo waliomaliza darasa la saba wanaweza kulitambua hili vizuri kuliko wenye degree mnaopekua vitabu tu.
 
Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,083
1,500
Inaonekana tutakuwa tunatumia meno kuchakata bidhaa kuwa finished goods, si muliambiwa mtalimia meno? vinginevyo ni ndoto ya mchana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom