Eti ni kweli kwamba mtu akizinduka Mochwari huwa anauliwa ili kulinda kibarua?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,252
21,345
Naombeni Tujuzane wadau!

Pamoja na vipimo vya madakitali kuwepo: Nasikia kuna wakati huwa vinadanganya!

Madakitali nao kwa namna moja au nyingine saingine hupitiwa na kukosea kwa kuidhinisha Mtu kufariki.

Eti ni kweli Inapotokea bahati nzuri mtu akazinduka mochwari nasikia huwa wanamalizia ili kulinda vibarua vya walioidhisha!

Nasikia mgonjwa anaezinduka humaliziwa kwa sindano au Rungu la kichwa chap!!

Je; ni kweli?
 
Hahah dunia inamengi sana iache tu. Kama ni mrembo nasikia jamaa wanakula nyapu wakishatosheka wanakurudisha ulikotoka.
 
Nilisimuliwa story za mortuary na jamaa mmoja aliyekuwa Mortuary attendant Muheza hospital ilibidi nivunje urafiki naye.
Tulikutana jeshini miaka fulani.
Alinisimulia jinsi walivyokuwa wanatoboa kichwa kwa misumari ili kuipa mwanya sindano ya kuhifadhi mwili. Miili mingine ilikuwa inafika imekauka viungo havinyooki basi anaipiga rungu mpaka viungo vinakubali sheria. Walikuwa wakiuza maji ya kuoshea maiti. Sometimes wachawi walikuwa wanawapooza pesa ndefu ili wanyofoe kinyama cha marehemu.
 

namuonea huruma mshana jr kwani amekuwa kimbilio la kila kesi humu..

baba mashana pumzika kwanza ni zamu ya wengine sasa kuitwa badala yako

yawezekana jamaa hata akifa (samahani,) afu ikatokea mgogoro humu na ataitwa
N.B yawezekana akaja maana mshana kwa ulozi aisee sio pouwa inasemekana jf haidukuliwi na vipepeo kisa uwepo wa huyu Mpare wa bandarini
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom