eti ni kweli?ili mpira wa tanzania ukue ni lazima timu za simba na yanga zife?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
si maneno yangu,bali nimemnukuu mojawapo wa makocha wa vpl,kama ilivyokuwa kenya kwa afc leopards na gormahia na huku lazima iwe hivyo ndio tupate mafanikio kisoka.kuna ukweli wowote?
 
Hapana. tunazo changamoto nyingi Sana za kimfumo na uendeshaji wa soka letu toka ngazi ya chini hadi ngazi ya juu. yanga na simba zikifa na mpira umekufa. inatakiwa kuwe na timu kama Tatu nne tofauti ziweze kutoa ushindani kwa hizi timu mbili. mfumo wa ligi za chini urudishwe. ligi ya Taifa. umitashumta na umiseta. vpl haina hadhi ya kusajili wachezaji kutoka nje. Wachezaji wa ndani wangetosha na hapo tungepata timu ya Taifa bora. ligi yako ina wachezaji wa kigeni Wengi Sana wakati wewe wanaocheza ligi za nje hawafiki watano unategemea kuvuna nini timu ya Taifa
 
Simba na Yanga zina marefa wao,TFF ya sasa ni Yanga.Hapo isitegemee timu yenye uwezo kuchukua kombe.Pamoja na matatizo tuliyonayo,uyanga na usimba ni jipu.
 
Timu hizi kongwe zibinafishishwe kwa matajiri wenye pesa ya kusajili wachezaji wakubwa.Ili hata watz wachache watakao cheza humo wakue kimpira.Hapo hata ukikosa mapro bado ligi yako itakua bora na kuzalisha timu bora ya taifa.soka la vijana liwe na ligi angalau kila mkoa uwe na timu ya vijana.
 
...Timu hizo zinatakiwa ziji -modernise na vibabu vyao vyote vikae kando!, / vinaendekeza ushirikina tu.
 
Hapana. tunazo changamoto nyingi Sana za kimfumo na uendeshaji wa soka letu toka ngazi ya chini hadi ngazi ya juu. yanga na simba zikifa na mpira umekufa. inatakiwa kuwe na timu kama Tatu nne tofauti ziweze kutoa ushindani kwa hizi timu mbili. mfumo wa ligi za chini urudishwe. ligi ya Taifa. umitashumta na umiseta. vpl haina hadhi ya kusajili wachezaji kutoka nje. Wachezaji wa ndani wangetosha na hapo tungepata timu ya Taifa bora. ligi yako ina wachezaji wa kigeni Wengi Sana wakati wewe wanaocheza ligi za nje hawafiki watano unategemea kuvuna nini timu ya Taifa
Wachezaji wa nje wanaleta changamoto hivi sasa Kuna Wachezaji wangapi wa nje Vpl? Tatizo ni mfumo wa uendeshaji wa ligi angalia kombe la ligi ni upangaji matokea tu bado tusingizie wachezaji wa nje! Tanzania hatuna football academies mpira ni taaluma, mchezo ya shule za msingi imekufa, umiseta hoi, shimvuta sijui kama ipo tena. Timu hazina ufadhili wa maana mishahara shida, kuna matatizo mengi mno wacha wengine waje wajazie.
 
Simba na Yanga zina marefa wao,TFF ya sasa ni Yanga.Hapo isitegemee timu yenye uwezo kuchukua kombe.Pamoja na matatizo tuliyonayo,uyanga na usimba ni jipu.
wewe inaonekana ni mdau mkubwa wa michezo,yaani unapiga mule mule.
 
Back
Top Bottom