Eti ni kwanini ndani ya BIBLIA hakuna simulizi za utani Wala mzaha, tunapata fundisho Gani?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
22,314
34,693
Salaam,Shalom!!

Enyi Wana wa Mungu msomao BIBLIA, ni wapi umewahi kusoma simulizi yoyote yenye utani au mzaha?

Yaani ukakuta Mungu akimtania Nabii wake, au Nabii alifanya mzaha Kwa wafuasi wake?

Hii mizaha na utani wafanyayo watumishi wa Mungu wa Leo wakiwa madhabahuni wanaitoa wapi?

Wana wa Mungu mnapata wapi ujasiri wa kutaniana na kufanyiana mizaha, wapi mmejifunza haya, mmesoma andiko lipi?

Ikiwa unapenda kurudisha mahusiano na Mungu au unapenda kumpa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala hii.

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

Karibuni 🙏
 
(Mathew 5:37)

Ndio yenu iwe ndiyo, na hapana yenu iwe hapana.
 
(Zaburi 1:1)

Heri mtu yule ambaye hakuketi barazani pa wenye mizaha.
 
Sio kila kitu lazima kiandikwe kwenye biblia ndio ujue kilifanyika, mizaha au utani ni lifestyle tu au ni kama burudani ila inategemea ni wapi unaleta huo utani.

Mitume na manabii na hata Yesu unataka kusema walikua hawacheki hata kidogo?
 
Kucheka ni LAZIMA kutokane na utani pekee?
 
Vitabu vya kisayansi havina utani, vya hisabati na kanuni zake, tafiti mbalimbali vivyohivyo, Zaidi na Zaidi BIBLIA itakuwaje na utani?.
 
Utani ulichanganywa yakawa mafumbo..eti narisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbingu.

1000056576.jpg
 
Kucheka ni LAZIMA kutokane na utani pekee?
Hapana, lakini tukumbuke walikuwa ni binadamu pia kwahiyo waliishi kama binadamu wengine,

Sitaki kuamini maisha yao yote yalijengwa kwenye uSerious muda wote, hata kama hawatanii wao basi walitaniwa na kufurahi maisha yakaendelea.
 
Salaam,Shalom!!

Enyi Wana wa Mungu msomao BIBLIA, ni wapi umewahi kusoma simulizi yoyote yenye utani au mzaha?

Yaani ukakuta Mungu akimtania Nabii wake, au Nabii alifanya mzaha Kwa wafuasi wake?

Hii mizaha na utani wafanyayo watumishi wa Mungu wa Leo wakiwa madhabahuni wanaitoa wapi?

Wana wa Mungu mnapata wapi ujasiri wa kutaniana na kufanyiana mizaha, wapi mmejifunza haya, mmesoma andiko lipi?

Karibuni 🙏
Utani (pranks/jokes) na maigizo vyote hivyo ni dhambi.
 
Wanasema wangeandika vyote billiards isingetosha ila Maria na magdalena walivyokkutana wakiwa wajawazito vitoto vilicheka tumboni anyway sina uhakika
 
Utani ulichanganywa yakawa mafumbo..eti narisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbingu.

View attachment 3180708
Huo Si utani,

Nothing is impossible with God,

Lisilowezekana Kwa WANADAMU, Kwa Mungu kinawezekana.

Ngamia anaweza kupenya ktk TUNDU la sindano Mungu akitaka iwe Inakuja, kama ambavyo Bikra alichukua mimba na akazaa mwana.
 
Back
Top Bottom