Eti ni Haki yake Maalim Seif Kutibiwa nje ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti ni Haki yake Maalim Seif Kutibiwa nje ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhosni, Mar 26, 2011.

 1. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Amesema hivyo mbele ya waandishi wa habari aliporudi kutoka ulaya na India kutibiwa yeye na familia yake. Kwamba ni wajibu wa serikali kutibu viongozi nje ya nchi ili wawe na afya njema waweze kuhudumia wananchi.

  ITV Habari
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Eeh, bwana eee! Ni yaki yake. Mwache naye atulie kwenye kivuli baada ya kusota juani kwa miaka mingi.
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ni kweli
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Duh sasa viongozi wote wakibeba familia si itakuwa balaa?
  maana najua hapo Maalim lazima ana wake si chini ya wawili watoto ...
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwanini wasijenge hospitali hapa tutibiwe wote?

  Kumbe wanasiasa wanaumwa sana eh?Maana wakipata nafasi tu serikalini ndo haoo kutibiwa!

  Hivi ni lini mara ya mwisho nimesikia kiongozi be it raisi au wabunge wanaumwa wakaenda kutibiwa muhimbili au bugando,kcmc nk?

  Hizi hospitali ndo maana huduma mbaya maana wao hawatibiwi huko
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  Sisi Mwananyamala wao Ughaibuni! Dr. Slaa Muhimbili, sasa natambua kuwa hayuko nasi, whoever is not with us is with them. CCM NEW CADRE
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Jamani, mfumo mzima ni mbovu...Tusimlaumu maalim peke yake, of course kwa mujibu wa katiba yuko entitled!!
  Nadhani angekuwapo nchini toka mwanzo angeshaenda zake Samunge!
   
 8. D

  Dopas JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kimsingi hakuna tatizo kutibiwa popote kulingana na uwezo wa mtu. Tatizo la Maalim nadhani ni lugha aliyotumia kueleza hiyo airport Zenj haikuwa nzuri. Ni tatizo la namna ya kufikisha ujumbe. Alichopaswa pale airport ni kutoa shukrani kwa mwenyezi Mungu na wananchi wote wa Zenj kwa kumwombea apone. Badala yake alianza kutamba. Nadhani alivyozungumza inakera.
   
 9. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Lakini mbona yeye alikuwa akiponda wenzie wasitibiwe nje akisema ni mis-useful ya resource na katika kampeni zake alikuwa akisema kinachotakiwa ni kuimarisha sekta ya afya ili hata viongozi watibiwe kulekule zenj, yameishia wapi haya! SIYAAASA SIHASA!!!?
   
 10. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Si aende kwa babu Loliondo? Ulaya kuna nini mbona wenzie wanakufa tu huko-asiogope na aende tu loliondo hakuna dola kule only 500 kwishney, mbona akina shehe shamsi wanapitapita huko
   
 11. I

  I LOVE U Member

  #11
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haki yake kama viongozi wengine wanavyo tibiwa
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Kwa uwezo upi? ANATUMIA KODI ZETU
   
 13. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Zenj sekta ya afya haijawa imara mkuu.
   
 14. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Zenj ni nchi inayojitegemea na mipaka yake inatambulika kimataifa, mimi siijui sijawahi kuisoma katiba yao kama ambavyo sijawahi kuisoma katiba ya taifa langu nilipendalo TANGANYIKA nina ya tanzania tu.

  Watajua wao na nchi yao...
   
 15. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao ndio viongozi wa Afrika baada ya kuonjeshwa umakamu wa rais na lugha amebadili imekuwa ni haki yake kutibiwa nje sababu yeye ni kiongozi, Wa TZ tuamke tatizo si chama yaani CCM,CDM.CUF.TLP,NCCR, nk tatizo la TZ ni uongozi, je tuna viongozi bora wanaojali maslahi ya taifa na jamii nzima ya waTZ, majibu kichwani mwetu huo ndo upande wa pili wa SEIF
   
 16. s

  shadhuly Senior Member

  #16
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hahaa ndo siasa hiyo kila mtu anatafuta mkate.wacha ale nchi alichokitaka amepata.niliwahi kumsikia prof lipumba akishutumu ccm kwa viongozi wake hata wakiumwa mafua tu wanakwenda nje,kulikoni seif?so life style hata cdm wakipata watakwenda hamna shaka huo ndo ukweli.
   
 17. R

  Rangi 2 Senior Member

  #17
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunahitaji uzalendo katika nchi hii. Miaka 50 ya uhuru wa bendera sasa inatosha.
  Watanzania tuweke misingi imara ya taifa letu kwa kuhakikisha kuwa katiba inatungwa upya na kuweka misingi imara ya demokrasia, maadili ya uongozi, uwajibikaji na haki sawa kwa wote....vinginevyo tutatumia miaka mingine 50 kwa malumbano..
   
 18. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Wacheni unafikii,,maalim kwa mara yake ya kwanza mimi kufahamu kuwa anasumbuliwa baada ya siku ya maridhiano baina ya ccm na cuf zanzibar,aliumwa sana alilazwa kule muhimbili au munabisha ?

  Hali yake haikuwa nzurii,alienda india kwa sababu mambo ya afya india ni mazuri na wana madoctor wazuri sana,sasa nawaambia kuwa india huwenda watu binafsi binafsi wala sio viongozi,,na gahrama zao sio kubwa hivyoo inategemea na ugonjwaa,,,

  Ni haki yale kuenda popote pale,yule maalim seif alikuwa waziro kiongozi toka abudu jumbe alipokuwa rais,na seif ni mstaafu wa serikalii,analindwa kiserikali hata kabla ya kuingia madarakani tena ,,kwa hiyo lazima mueleweee,,
   
 19. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Afya uzeeni ni gharama sana hapa tz. Ni gharama za afya ndo zilimfanfa mrema ale matapishi yake, akakosa aibu, akampigia jk debe badala ya mgombea wa chama chake
   
 20. only83

  only83 JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ni haki ya kila mtanzania siyo yake peke yake.........................................
   
Loading...