Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Inaelezwa kwamba kupuuzwa kwa mila na desturi na maadili ya kidini kumechangia sana kuharibu tabia za vijana ikiwa ni pamoja na mambo ya urafiki, uchumba hadi ndoa. Ndio maana uchumba umegeuzwa kuwa ndiyo nafasi pekee ya vijana kukutana kwenye majumba ya starehe na hatimaye kufanya ngono. Na hapo ndipo unapokuja kugundua kwamba hata zile ndoa za kimila za kale zinazohusisha Kisarawanda, ili kuthibitisha kama bi harusi hajawahi kushiriki tendo la ndoa yaani kama bado ni Bikira, hazipo tena.
Utathibitishaje wakati hata kabla ya uchumba binti keshazipoteza zamani. Na ndio maana siku hizi hata ndoa zimeonekana kama zimepitwa na wakati. Vijana rijali tena wakiwa na siha nzuri hawako tayari kuoa tena, na badala yake wamekuwa wakiwabadilisha mabinti watakavyo.