Eti "Mtandao unaoongoza Tanzania"!

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Salaam,
Natumaini wana jamii ni wazima wa afya,kwangu mimi ni mzima na buheri wa afya.
Eti huo usemi hapo juu ni wakweli?
Kama nikweli inamana wanawateja wengi kuliko kampuni za simu zote hapa nchini.
Lakini jambo lililonisukuma niandike posti hii ni kuwa,kama wanaongoza basi wangeongoza na kulipa Kodi,na Wangekuwa wanaongoza kwenye kuchangia pato la taifa kuliko air tel.
Sasa tujiulize ni mtandao unao ongoza kwa kipi nchini Tanzania??

Kiukweli Vodacom ndo mtandao wenye wateja wengi sana wakifuatiwa na Airtel kisha Tigo, kisha Zantel then TTCL then Sasatel na wa mwisho ni BOL.
Kwa kulipa kodi siwezi kulisemea kwakuwa yawezekana kabisa kwa namna wanavyoendesha biashara zao sheria ikawafanya walipe kodi kiduchu. Lakini pia tuna sheria za kipuuzi sana zinazotoa mwanya kwa majizi kukwepa kodi.
All in all Vodacom ina lead kwa customer base

Mtandao unaoongoza kwa wateja hali kadhalika mtandao unaoongoza kwa kukwepa kodi
Nchi ya kitu kidogoooo,TRA wamewekwa sawa maisha yanaendelea nadhani iyo slogan itabidi waiondoe

"Vodacom mtandao unaoongoza Tanzania kwa kukwepa kodi" Kazi ni kwako!

ulitegemae ROSTAM kulipa kodi?wakati yeye kaja toka iran kuja kuchuma kwa wana bongolala

Sijajua wanaongoza kwa lipi? kama unatumia modern ya voda huku manyara imekula kwako, kwani haipiti nusu saa network inakata, mara siku mbili nzima hamna network.

Ila kwa matumizi ya simu za mkononi hilo silipingi, napinga kwenye mambo ya internet wako nyuma vibaya, wanapigwa bao mpaka na tigo. na hapa navyoandika hivi vimaandishi vichache, imekata mara mbili.

Salaam,

Natumaini wana jamii ni wazima wa afya,kwangu mimi ni mzima na buheri wa afya.

Eti huo usemi hapo juu ni wakweli?

Kama nikweli inamana wanawateja wengi kuliko kampuni za simu zote hapa nchini.

Lakini jambo lililonisukuma niandike posti hii ni kuwa,kama wanaongoza basi wangeongoza na kulipa Kodi,na Wangekuwa wanaongoza kwenye kuchangia pato la taifa kuliko air tel.

Sasa tujiulize ni mtandao unao ongoza kwa kipi nchini Tanzania??

Ndiyo inaongoza kwa kuwaibia wataje!

mkuu hapa bongo kila mtu anamaslahi na kitu anachofanya ndio maana kwenye list ya vinara walipa kodi kampuni za madini ambazo ni kubwa haipo hata moja sasa basi kulingana hali ilivyo hawa jamaa wa vodafone wao wanalipa kodi sauzi na hapa wanatusaidia kutoa huduma ya simu sawa mkuu..

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom